Unajua kitu kimoja ambacho niliambiwa na dada mmoja ambaye alikua anafanya kazi kwenye kituo cha kupima na kutoa ushauri nasaha kwamba usimwamini mtu yeyote ambaye huna uhakika wa status ya afya yake, kwa kweli yale maneno yalinikaa sana hadi hii leo nayakumbuka kama nimeambiwa jana,so hata iweje mimi mwanamke ambaye siyo permanent girl wangu huwa sitembei nae bila kutumia mpira, na juu ya yote kila baada ya miezi sita lazima nirudi nipime,huu ugonjwa toka umeniondolea mdogo wangu ndio nimezidi kujitenga nao kabisa,japo bwana mdogo wangu ni kama alitaka tu mwenyewe kwani alikua hataki dawa wala kwenda hospital aliamua tu iwe hivyo na ukamuondoa.