Hivi aliyekuja na utaratibu wa mahafali kabla ya mitihani ni nani?

Hivi aliyekuja na utaratibu wa mahafali kabla ya mitihani ni nani?

EvilSpirit

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2017
Posts
10,576
Reaction score
16,644
Wakati mtihani wa kumaliza elimu ya msingi ukikaribia nimekuwa naona shule kadhaa zikifanya mahafali kabla watoto hawajafanya mitihani nakumbuka enzi zetu tulikuwa tunafanya pepa kisha mahafali.

Yaani unasheherekea kumaliza halafu ndio unamaliza.
 
Kuepusha vurugu za kijinga wakati wa mahafali ndio sababu kuu ili nidhamu ichukue mkondo wake

Kwani kuna kipindi wakati wa mahafali kulikuwa kunatokea vitendo visivyo vya kiungwa ikiwemo walimu kula kipigo cha mbwa koko na walikuwa hawana namna ya kumpata mwanafunzi.
Hivyo ikaamuliwa iwe kabla ya pepa ili kuwadhibiti
 
Ni utaratibu tu, kuna baadhi ya shule wanafanya baada ya mitihani pia.
 
Sio nchi nzima wanafanya mahafali kabla ya mtihani.
huu utaratibu ni wa Shule na Shule.
Sisi huku 99% mkoa wetu wa Tabora mahafali baada ya kumaliza mtihani s.k.a Kumaliza shule
 
Swali lako linafanana na mnyamwezi mmoja aliyeuliza kwamba hivi nani aliyekuja na utaratibu wa kutoa cheti cha ndoa na kufanya sherehe za harusi kabla ya tendo la ndoa kufanyika?
 
Kuepusha vurugu za kijinga wakati wa mahafali ndio sababu kuu ili nidhamu ichukue mkondo wake

Kwani kuna kipindi wakati wa mahafali kulikuwa kunatokea vitendo visivyo vya kiungwa ikiwemo walimu kula kipigo cha mbwa koko na walikuwa hawana namna ya kumpata mwanafunzi.
Hivyo ikaamuliwa iwe kabla ya pepa ili kuwadhibiti
Hili ndio jibu tosha
 
Back
Top Bottom