Hivi ni vitu visivyotambulika vinavyopaa au kudondoka kutoka angani. Vitu hivi vinatajwa kuwa na uhusiano mkubwa na aliens na wanasayansi wa Kimarekani.
Hizi UFO zipo za aina mbili. Kuna zinazotoka katika uso wa dunia ambako kuna watu waliostaarabika. UFO nyingine ipo nje ya uso wa dunia inawezekana angani au katika sayari nyingine.
Ukiachilia mbali vimondo unaweza ukaona kitu kinangaa angani na ghafla kikapotea kutokana na spidi yake. Hizo ndizo UFO.
Mara nyingi vitu hivi vimekuwa vikionekana katika rada za duniani akiwemo aliens maarufu waitwao Ashar Sheran na Valiant Thor kutoka Sayari ya Venus.
Inasemekana kuwa nchi zilizoendelea hasa Marekani huwa hawataki vitu kama UFO au hawa aliens wawe na ukjaribu na nchi masikini kwani nazo zitakuwa na nguvu ya kuzifikia au kuzipita kabisa.
Watu wengi hawafahamu kiundani kuhusu UFO. UFO ikipita kwa mdano Dar es Salaam, wakati wa shughuli za mchana inaweza kusababisha taharuki kwa watu na ajali nyingi kwa wakati mmoja.
Katika kutafuta undani juu ya mambo haya, mtunzi na mwandishi mashuhuri duniani, James Hadley Chase kupitia kitabu chake cha Dooms Day Conspiracy alijaribu kuelezea habari za hawa UFO vizuri, namna serikali kubwa zinavyoficha uwepo wa aliens na UFO kwa kuhofia kuzusha hofu kwa raia.
Ukweli utabaki palepale kuwa kuna viumbe wanaoishi nje ya dunia ambao wana teknolojia kubwa kuliko ya binadamu na kinachotokea mara kwa mara ni kwamba huwa vyombo vyao angani vinakuja duniani.
Unakumbuka kile chombo cha aliens kilichodondoka nchini Mexico? Ilisemekana kuwa kilipodondoka tu ndege za kijeshi za Kimarekani zilifika ndani ya muda mfupi ambapo wanasayansi walikibeba na kukipeleka makao yao makuu, NASA. Wanasayansi watano wa Marekani waliowahi kujishughulisha sana na utafiti juu hawa viumbe walifanikiwa kugundua lugha yao.
Mmoja wa wanasayansi hao alipojaribu kuvujisha siri katika vyombo vya habari, wanasayansi hao walipotea katika mazingira ya kutatanisha na hawakuonekana tena.
Nchi kubwa kama Urusi, Marekani, China, Uingereza na Japan zina hofu kubwa juu ya aliens kwamba wakipata nafasi ya kujitanua kiteknolojia hapa duniani itakuwa ndiyo mwisho wa ustaarabu wa binadamu ndiyo maana zinajitahidi sana kuzuia au kujipa wenyewe teknolojia yao ili itakapotokea aliens wakavamia duniani wao wawe tayari wamejiweka vizuri.