Hivi Arsenal hawaogopi? PSG hii si ya mabishoo wanaotembea uwanjani

Hivi Arsenal hawaogopi? PSG hii si ya mabishoo wanaotembea uwanjani

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Hivi kweli Arsenal F.C. hawaogopi? 😅

Hii si ile PSG ya Lionel Messi, Neymar na vibes za Paris nights, hii ya sasa ni tofauti kabisa. Hakuna show nyingi, hakuna kutembea uwanjani. Hawa wanakaba kama wamekosewa hela 😭

Arsenal wana mpira mzuri, lakini PSG ya sasa ina njaa ya ubingwa kuliko likes za TikTok.
Kesho si mechi ya majina makubwa, ni mechi ya nani ana moyo wa kufa na kupona dakika 90.

Na ukiona mashabiki wa Arsenal wanaanza kusema “trust the process” mapema, ujue presha imepanda.

 
Last season Inter Milan alikuwa bora zaidi ya PSG lakini akafungwa. PSG alikuwa bora kuliko Chelsea lakini Chelsea akabeba ndoo.

Mpira haujawahi kutabirika kirahisi dogo.
 
WatApigwa kama ngoma ! Saliba siku hizi ana choma choma, sema Gabriel ana_clear sana makosa yake !

Good enough kule namba mbili hawana mtu wa maana, unajua ni nani wanaenda kukumbana nae ule upande ? Naogopa kutaja..... Ben White hayupo fit, Timber kafanya mazoez siku kadhaa this week, Yes kasafiri na timu lakini sidhani kama kocha atamuanzisha, ni risk! Wacha wapigwe hawa nguchiro (in yule msemaji's voice )
 
Nawaamini sana PSG lakini nikikumbuka vile waliminywa kirahisi na Chelsea kule Marekani kwenye kombe la Dunia la vilabu,siwapi nafasi.
 
Kuna jamaa yangu analia sana kuhusu Arsenal/Arsenane!Mola awarehemu wana Arsenal wote.Aaaamiin;
 
Back
Top Bottom