Hivi Baadhi Ya Watanzania Wa JF (Kenyan Forums) Huwa Na Low Self-Esteem?

Hivi Baadhi Ya Watanzania Wa JF (Kenyan Forums) Huwa Na Low Self-Esteem?

Hii ni Kenyan forum; ikiwa kuna kasoro au uwongo kwa chochote kisemwacho, basi pinga ukizingatia mada iliyopo. Nikija niseme Kenya inatoa maziwa mengi duniani nzima, nipinge kwa data ikiwa unaona ni uwongo. Lakini usije ukasema Tanzania inatoa mchele mingi duniani nzima. Huo ni kutoelewa mada na unadhihirisha elimu duni.

Ziko kasoro nyingi ambazo huwa zinasahihishwa hapa tena kwa takwimu! Kama ni mfuatiliaji mzuri hili halitakuwa geni
 
Ikiwa nia tu ni kuleta ubishi kati wa TZ vs KE, huo ni utoto pia. Lakini, kuna wakati mwingine mada huletwa hapa kwa ajili ya analysis. Kwa mfano, Kama Wakenya, tunaona nini kuhusu uongozi wa Magufuli? Kuna wale ambao wanaisupport na kuna wale ambao wanaipinga. Kama tu vile kwenye Jukwa la Siasa huwa na mada kuhusu uchaguzi wa Kenya na Katiba ya Kenya. Sio eti mnaiponda Kenya, bali ni kuanalyze aina ya katiba na siasa kwa macho ya mtanzania. Ni upuuzi mie kama mkenya kupeleka mada za kikenya kwenye Jukwaa la Kisiasa

Nia sio kuleta ubishi bali ni kuelimishana! Hakuna mtu anaweza kukaa kwa ajili ya kubishana, badala yake ni kuelimishana!

Kama vile mbayo mada ya tz huletwa hapa na wakenya kwa ajili ya analysis, vivyo hivyo na sisi tukileta hapa habari ya tz inakuwa ni kwa ajili ya analysis, iwe nzuri au mbaya! hata za Kenya tunaleta kwa ajili ya hiyo hiyo!
 
Mtu huenda kwenye majukwaa ambayo humfurahisha, ndio sababu hizi jukwa zilikuwa divided. Kilichonileta katika JF, ni Jukwaa la Lugha, na baadaye Jukwaa la Elimu. Nilidhani ya kuwa nitapata majadiliano ambayo yatafanana na zile nyuzi nilizozipata mtandaoni na amabazo zilinileta JF. Kilichoniudhi nilipata wengi tu michango zao ni za kitoto, kana kwamba wachangiaji wa hapo awali walishatoweka. Sub-forum ya kuchekesha ni ya mapenzi.

Kingine ni kuwa wengi hutemebelea majukwaa mengi ya TZ yakiwemo ya kisiasa lakini hatuwezi kucomment kwa kuwa tunajua vizuri sana hatuko informed ukilinganisha na wabongo wenyewe. Sina la kuwafunza kule; ni kujielimisha tu.

Kwenye jukwaa la lugha na elimu, au hata majukwaa mengine, kama unataka kujifunza vitu basi fuatilia threads za zamani kidogo, ie 2006-2014. Hapo utakutana na mijadala iliyoshiba kweli kweli! Wachangiaj wengi wa sasa attitudes zimebadilika hivyo mijadala mingine inakuwa tofauti na ilivyotegemewa!

Kwenye jukwaa la Mapenzi, Chit chat na Udaku huko lazima pakuchekeshe! kiufupi huko tunadema ni stress free zone!

Lakini nakushauri kutembelea jukwaa la JAMII INTELLIGENCE. Kuna elimu nzuri na uchambuzi murua wa masuala mbali mbali! Hutojuta kutembelea huko! Au Great thinkers/The palace uombe kuunganishwa!
 
Wale wanaofanya mataifa haya mawili kushindana hawamo JF. Ni wanasiasa na watu wakubwa wenye kuamsha skyscrapper. Humu JF ni pahala pa kujielimisha na kutafuta njia ya kujindeleza maisha yetu. Haya mabishano ya JF ni ya wananchi wa kawaida ambao kila siku twajiuliza jinsi tutakavyolipa kodi ya nyumba na karo. Haina maana mie kujigamba kuhusu skyscrapper ambazo hata kazi ya mjengo sipati.

Asante Kwa mchango wako. Nitakwenda kule nipeleke malamishi yangu kuwa TZ news zibaki kwenye Jukwaa la kisiasa au Biashara.

Ni kweli, Lakini sisi kama watu wa mataifa hayo hatuwezi kuacha kujadili mambo yanayotokea kwenye haya mataifa, na ikiwezekana inakuwa njia nzuri ya kufikisha ujumbe kwa hao wanasiasa.
 
Nia sio kuleta ubishi bali ni kuelimishana! Hakuna mtu anaweza kukaa kwa ajili ya kubishana, badala yake ni kuelimishana!

Kama vile mbayo mada ya tz huletwa hapa na wakenya kwa ajili ya analysis, vivyo hivyo na sisi tukileta hapa habari ya tz inakuwa ni kwa ajili ya analysis, iwe nzuri au mbaya! hata za Kenya tunaleta kwa ajili ya hiyo hiyo!
.,habari za Ke humu, watz kazi ni kupinga with biased facts, kuponda wakishindwa ni matusi, e.g, njaa, kibera, chokora., na ile percentage katika shida hizo ni chache., blind patriotism at play on both sides, hardly sober debates.
 
Mtu akikuponda anakupa challenge urekebishe penye hitilafu!

Mind u, sio watz wanaopenda tu, wakenya wanaongoza! Fuatilia mijadala vizuri
 
yaani umesema ukweli kabisa mkuu...watanzania wengi huwa na tabia ya kuleta habari zisizohusu kenya humu ili muradi tu wazue debate na matusi kati yao na wakenya....mara nyingi wanaleta tz news kwa Kenyan news and politics....pia wana tabia ya kuleta habari mbaya toka Kenya humu...sijui wana ugonjwa ipi hawa...mtu ana rauka 6AM kutafta habari za Kenya toka Google kisha anaruka makusudi zile za good news akisaka zile mbaya mbaya...pengine ni unemployment na inferiority complex....lol!...

mkenya akileta habari za skyscrapers Nairobi, mtanzania analeta habari za Kibera....mkenya akileta za uchumi, mtz analeta za cooking data....yaani ni tabia mbaya sana...inaonyesha kuwa watz wengi wanashuku maendeleo yao na kuskilia Kenya wivu....I mean, is it difficult to say congratulations Kenyans for the development? Must you now bring tanzanian news in this forum so that you feel better?

ila pia siwezi walaumu sana sababu Wakenya wachache sana ndio huwa wanaenda kule ktk jukwaa la siasa ama thread zingine za kitz...wengi hawajishugulishi...sasa ni lazma walete Kenyan News ndio wapate replies za wakenya...

watz hawa ndio wanahusika zaidi
Geza,Kilam,Mwanzi, Mulisaa...ila kuna wengi tu wana tabia hizi za kitoto...
Uchokozi tuu...[emoji15]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ndio ungejiangalia kwenye kioo kabla ya kuleta hoja kama hii, huu mchezo mchafu ulianzishwa na nyinyi wakenya mkifikiri Watanzania watalaza damu.

Umeingia humu juzi unasema huu mchezo ulianzishwa Na Wakenya.
 
Umeingia humu juzi unasema huu mchezo ulianzishwa Na Wakenya.
He he heeeeee! Usishangae huyo unayesema kaja juzi alikuwepo kabla yako

[emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124]
 
Tatizo wengi ni VILAZA na ndio maana wanakimbilia huku...
kama mtu na diriki kusema Dar ni moja kati ya miji misafi Afrika na kwenda mbali akidai Dar>Nairobi ni dhahiri huyo mtu ni mpenda sifa toka mtaa wa Lumumba.
It's okay kutetea nchi yako popote pale, it's not okay kutetea uongo kuhusu nchi yako popote pale.
 
Uliona list ya miji michafu africa mwaka huu?
 
Bado unazungumzia hiyo list!?!?
Mi nazungumzia reality mkuu.

We unefanya research ..au unajua kufanya research ..au unawakosoa waliofanya research ..maana research hutumia pesa nguvu na muda .na pia haijafanywa na wa Tz
 
We unefanya research ..au unajua kufanya research ..au unawakosoa waliofanya research ..maana research hutumia pesa nguvu na muda .na pia haijafanywa na wa Tz
Mimi nimeishi Dar huu mwaka wa Ishirini, so nikisema Dar chafu nina uhakika na ninacho kisema.
Kujua kama sehemu ni chafu au safi unahitaji sense organs tu, huitaji kua genius kulijua hili.
Dar ni chafu sasa wewe ungana na hao watu wa nje wakati mimi mkaajaiwa eneo husika nimeona hili jiji ni chafu.
 
Tatizo wengi ni VILAZA na ndio maana wanakimbilia huku...
kama mtu na diriki kusema Dar ni moja kati ya miji misafi Afrika na kwenda mbali akidai Dar>Nairobi ni dhahiri huyo mtu ni mpenda sifa toka mtaa wa Lumumba.
It's okay kutetea nchi yako popote pale, it's not okay kutetea uongo kuhusu nchi yako popote pale.
Wewe mtu wa chadeko hii ndo Nairobi wewe.
garissa-market-in-the-somali-district-of-eastleigh-nairobi.jpg
image.jpg
images-10.jpeg
 
Mimi nimeishi Dar huu mwaka wa Ishirini, so nikisema Dar chafu nina uhakika na ninacho kisema.
Kujua kama sehemu ni chafu au safi unahitaji sense organs tu, huitaji kua genius kulijua hili.
Dar ni chafu sasa wewe ungana na hao watu wa nje wakati mimi mkaajaiwa eneo husika nimeona hili jiji ni chafu.
Wewe umekuja Dar sisi tumezaliwa Dar na Nairobi tumeishi pia. Niye ndowale watu mkifika mjini mnajifanya kuujua sana kuliko wenyeji. Nairobi wakikuonyesha hizi gari za uchafu na kufanya usafi wa jiji za kisasa. Mimi nahama JF wakikuonyesha au hata wewe ukinionyesha. Tutajua jiji lipi chafu au safi.
IMG_2394.jpg
IMG_2623-1.jpg
FB_IMG_1499837744235.jpg
FB_IMG_1499837759189.jpg
FB_IMG_1499837799580.jpg
FB_IMG_1499837713913.jpg
FB_IMG_1499837728281.jpg
FB_IMG_1499837810201.jpg
FB_IMG_1499837702800.jpg
IMG_20170605_184850.jpg
IMG_20170605_184802.jpg
 
Tatzo watanzania wanapenda siasa hewa wana maneno mengi mdomoni na always wanaongea vitu ambavyo hawana proof navo ndo maana pia wengi wanakurupuka kufanya publication za infomation ambazo ni za uongo kuhusu serikali na mambo ya binafsi....
Mm kama partly tanzanian, partly kenyan wa tanzania umbea na utoto mwingi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom