blackberryz30
Senior Member
- Jan 21, 2018
- 141
- 197
Nianze kwa kusema siamini katika chama chochote, na nasikitika kwa kila kibaya kinachoendelea katika taifa hili....kama mmoja wa wananchi na mlipa kodi inauma kuwa wamekula kodi zetu kwq miaka yote tangu uhuru hadi sasa na hakuna aliyehangaika nao zaidi ya kuwasema tu....wamenogewa kiasi cha kuona sasa hata kusemwa ni kelele sasa wameamua kuua kabisa wasemaji...sasa hivi ukiagana na nduguyo na mkaonana mkiwa salama ni ajabu na muujiza...na si kwa wanasiasa tu, watoto wanapotea, watu wanavamiwa majumbani kulawitiwa na kuuwawa, wanaotolewa kwenye mabasi na kupotezwa, hospitalini afya hazithaminiwi....yaani ni kama taifa halina uongozi kabisa na mashetani ndio yanatawala...sasa nauliza wadau na mdau je tunasababu ya kuendelea kuwa watiifu kwa serikali hii... ambayo kimsingi bila sisi haiwezi kuwepo, kama ndiyo je ni sababu ipi ya kufanya hivyo...maana uchumi, uhai na mengine yote yanayotuhusu yapo mashakani....!