Hivi biashara ya mayai ya kware iliishia wapi jamani?

Hivi biashara ya mayai ya kware iliishia wapi jamani?

Hii biashara ilivuma sana hasa ikihusisha na nguvu za kiume na watu walipiga hela sana kwa kuanzisha ufugaji wa kware na kuuza mayai yake lakini sasa naona kimyaa. Watu wakianza kuvumisha kitu hasa kukihusisha na nguvu za kiume kinapata soko sana. Akiibuka mtu leo na kusema mayai ya nyoka yanaongeza nguvu za kiume msako mkali utaanza kutafuta mayai ya nyoka popote mashimoni na mapangoni na ukitaka watu waanze kufuga nyoka tangaza kuwa mayai yake yanaleta nguvu za kiume
Ila wazee mayai ya kware ni kweli yanatibu. Mke wa staff mwenzangu alikuwa na severe ucleus, alitibiwa kwa kunywa mayai ya kware
 
Ukisema kinyesi cha mtot aliyezaliwa tarehe 29/2 ya kila mwaka inaongeza nguvu za kiume itakuwaje? Maan ni baada ya miaka kadhaaa
Watoto wote watakaozaliwa siku hiyo watatekwa
 
Serikali iliyapiga malufuku kupitia Wizara ya Afya. jamaa yangu mmoja alipiga hela hatari.
 
Sasa hivi tuna GLOBAL ALLIANCE, vijana wanaichangamkia kama zuzu aliyepewa glasi badala ya Almasi.
 
Kikombe cha yule babu TAPELI ,aliye waingiza KING hata WATAALAM, WAJUZI WA MAMBO WALIOBOBEA, UMESHA SAHAU????

Hata huyu aliingia kingi.....??

images.jpeg
 
Sasa hivi tuna GLOBAL ALLIANCE, vijana wanaichangamkia kama zuzu aliyepewa glasi badala ya Almasi.
hii kitu utasikia "one million,, two million",, hahahaaa daah, jamaa ni wezi sijawahi ona,

Kweli mtu utoe laki5 na 60 zen unapewa package ya dawa za kienyeji na dawa za meno ukauze,, halafu mtu na akili zake timamu nae anaenda, na anakuja kukushirikisha fursa na wew ukapigwe pesa yako duuu…!!!
 
Hii biashara ilivuma sana hasa ikihusisha na nguvu za kiume na watu walipiga hela sana kwa kuanzisha ufugaji wa kware na kuuza mayai yake lakini sasa naona kimyaa. Watu wakianza kuvumisha kitu hasa kukihusisha na nguvu za kiume kinapata soko sana. Akiibuka mtu leo na kusema mayai ya nyoka yanaongeza nguvu za kiume msako mkali utaanza kutafuta mayai ya nyoka popote mashimoni na mapangoni na ukitaka watu waanze kufuga nyoka tangaza kuwa mayai yake yanaleta nguvu za kiume

Umesahau na MAFUTA YA UBUYU
 
Back
Top Bottom