Hivi binadamu akiishi milele si maji na hewa na sehemu kubwa ya ardhi vitaisha ili kumtengeneza?

Hivi binadamu akiishi milele si maji na hewa na sehemu kubwa ya ardhi vitaisha ili kumtengeneza?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Habarini. Ukiangalia mwili wa binadamu na wanyama utaona kuwa ni mpangilio tu wa elements ambazo zipo kwenye mazingira tunayoishi. Asilimia zaidi ya 60 ya binadamu anaundwa na Oxygen. Elements zingine zinazofuata ni Carbon, Hydrogen na Nitrogen. Zingine zilizopo kwa uchache ni sodium , potasium, chuma nk.

Angani element inayoongoza kwa wingi ni Nitrogen ikifuatiwa na Oxygen na zinginezo. Ardhi yetu hii(Crust) kwa sehemu kubwa inaundwa na Oxygen, ikifuatiwa na Silicon, aluminium, Iron, calcium nk. katika hizi. Silicon na Aluminium ni kama hazipo mwilini mwa binadamu.

Maji ni oxygen na hydrogen, na yanapatikana kwa wingi mwilini mwa binadamu.

Sasa basi, iwapo binadamu angeishi milele. Yaani kuwe na matrilioni na matrilioni ya binadamu. Si inamaana kuwa maji yote yangetumika kutengeneza binadamu. Oxygen yote hewani na Nitrogen vyote vingetumika kumtengeneza binadamu.

Maji yote tunayoyaona yangekuwa ndani ya miili ya binadamu. Calcium yote ingetumika kuunda mifupa ya binadamu. Chuma chote kingekuwa kwenye damu ya binadamu. Maana binadamu wangekuwa wanaongezeka wakitumia madini haya lakini madini yenyewe hayaongezeki.

Hewa isingekuwa na chochote, ardhi hii ya juu ingelika pakubwa sana, bahari, maziwa na mito vingekauka maana maji yote yangekuwa kwenye miili ya binadamu. Sijui kama tungekubali kushare elements hizo na viumbe wengine?

Bila shaka Mungu hakuumba watu waishi kwenye hii sayari tu. Bila shaka sayari nazo wingi wake ni milele.
 
Mungu hakuumba watu waishi kwenye hii sayari tu
Una miaka mingapi???...sasa km unaamini Mungu kaumba atashindwaje kuumba calcium na essentila elements nyingine za kumfaa binadamu??

hivi nani alikwambia binadamu ana kufa??..... si unamuamini MUngu weye?? au geresha tu! Mungu si mjinga!
 
Una miaka mingapi???...sasa km unaamini Mungu kaumba atashindwaje kuumba calcium na essentila elements nyingine za kumfaa binadamu??

hivi nani alikwambia binadamu ana kufa??..... si unamuamini MUngu weye?? au geresha tu! Mungu si mjinga!
Mkuu umeelewa mada?
 
Back
Top Bottom