Hivi Bongo hakuna Tax Attorneys na Tax Consultants?

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Wakuu kilio cha kodi na kuhusu TRA kimekuwa kikubwa sana. Hii ni sababu wengi wengi hatujui mambo ya kodi. Huyu Rais amedhamiria kutokomeza mianya yote ya ukwepaji kodi na kukusanya kodi zote.

Ni lazima wafanyabiashara tuwe na elimu ya kutosha ili tusijeonewa mahali. Haiwezekani eti TRA ndiyo wawe wanatupa elimu ya mlipa kodi!

Wako wapi wataalamu wa kodi, wanasheria na waliosomea masuala ya kodi? Wakiandika hata vitabu na kutoa semina za kodi itakuwa poa sana. Mtu unaenda kulipa huku unajua kinachoendelea.

Hata mbinu za kulipa kodi kidogo tutafundishwa. TRA hawawezi kukufundisha mbinu za kukupunguzia kodi.

Wako wapi hawa wataalamu? Chama cha wafanyabiashara hakiwezi Organize mambo haya?
 
Miaka ya nyuma Moro kulikuwa na mhindi mmoja cha pombe sanaa lakini alikuwa balaa kwenye kusaidia wafanyabiashara kwenye mambo ya kodi, kuweka vizuri hesabu n.k.
 
Wapo hawa watunza mahesabu CPA, ambao pia wanaweza kushauri au kuelekea masuala ya kodi. Hivyo ukiona mtaani ofisi wamejinasibu ni Public Accountants, jaribu juuluzia huduma zao.
 
Wapo ila unaanzaje kushitaki serikali hii hasa secta yake nyeti kama TRA. Labda uhame nchi ndyo uwafungulie kesi.
Sio kuishitaki, ila ikibidi inawezekana, kuna mahakama za masuala ya biashara. Lengo ni kuwe na uwiano wa mapato, gharama na kodi. Wafanyabiashara wengi wakitambua haki zao, kutakuwa na mfumo wa haki wa masuala ya kodi.
 
Iyo mahakama ingekuwa mhimili unaojitegemea sio huu ambao upo mfukoni wa magufuli
 
Wakuu kilio cha kodi na kuhusu TRA kimekuwa kikubwa sana. Hii ni sababu wengi wengi hatujui mambo ya kodi. Huyu Rais amedhamiria kutokomeza mianya yote ya ukwepaji kodi na kukusanya kodi zote.

Ni lazima wafanyabiashara tuwe na elimu ya kutosha ili tusijeonewa mahali. Haiwezekani eti TRA ndiyo wawe wanatupa elimu ya mlipa kodi!

Wako wapi wataalamu wa kodi, wanasheria na waliosomea masuala ya kodi? Wakiandika hata vitabu na kutoa semina za kodi itakuwa poa sana. Mtu unaenda kulipa huku unajua kinachoendelea.

Hata mbinu za kulipa kodi kidogo tutafundishwa. TRA hawawezi kukufundisha mbinu za kukupunguzia kodi.

Wako wapi hawa wataalamu? Chama cha wafanyabiashara hakiwezi Organize mambo haya?
Certified Public Accountants wapo wengi wanafanya hizi kazi za tax consultations.

Law offices nyingi siku hizi zina lawyers ambao wamespecialize kwenye masuala ya kodi.

Wapo wengine wameandika mpaka vitabu kwenye masuala ya kodi.

Kiufupi all corporate lawyers wanatoa pia services kwenye masuala ya kodi.

Je utaziweza gharama za kuwa na hao tax consultants ??
 
Chukua initiative mwenyewe usome tax laws na decided cases
Sheria hazisomwi kama Riwaya hasa za kodi hatajua chochote sana sana atajikuta amekuwa mjuaji tu badala ya mjuzi.

Atafute mwanasheria hata kama ni junior anayezijua sheria za kodi atamsaidia kwenye mambo yake badala ya kujisomea mwenyewe tu
 
Wakuu kilio cha kodi na kuhusu TRA kimekuwa kikubwa sana. Hii ni sababu wengi wengi hatujui mambo ya kodi. Huyu Rais amedhamiria kutokomeza mianya yote ya ukwepaji kodi na kukusanya kodi zote.

Ni lazima wafanyabiashara tuwe na elimu ya kutosha ili tusijeonewa mahali. Haiwezekani eti TRA ndiyo wawe wanatupa elimu ya mlipa kodi!

Wako wapi wataalamu wa kodi, wanasheria na waliosomea masuala ya kodi? Wakiandika hata vitabu na kutoa semina za kodi itakuwa poa sana. Mtu unaenda kulipa huku unajua kinachoendelea.

Hata mbinu za kulipa kodi kidogo tutafundishwa. TRA hawawezi kukufundisha mbinu za kukupunguzia kodi.

Wako wapi hawa wataalamu? Chama cha wafanyabiashara hakiwezi Organize mambo haya?
nahiyo ndio changamoto TRA hawana kitengo chakuwawezesha wakusanyaji kodi kujua ni sh ngapi wa chukue kwa nani ndio mana watu walikuwa wanalalamika kodi haieleweki, ni kutokana biashara zetu hazina mssimamo leo umepata 100 kesho 50 keshokutwa 30 sasa tukisema tukukate 100 kwa mwaka au tukukate kwa asilimia hakuna anaejua umeingiza sh ngapi kwasababu miamala haiko kwenye mfumo wa kibenki ni mangi anasubiri akijaza pesa yake akaongeze mzigo. na ndio changamoto kwenye ukusanyaji mapato lakini nafikiri serikali inalifuatilia hata waziri ametoa tamko leo.
 
Back
Top Bottom