Au Tanzania sanaa ya uigizaji imebakia kua ni kipaji hata kama hujui kusoma na kuandika. Wasanii wetu hawa kiwango chao cha shule kikoje. Au ndio vile ukiwa na matako makubwa na ukajua kutembea na chupi tu na dadies nyingi unakua muigizaji mkubwa?
The Rock ana shahada ya criminology, David Otunga ana Masters degree ya sheria toka Havard university, ni sehemu wa waigizaji wakubwa wenye shule kubwa.
Sijaelewa msingi wa hoja yako ni nini hasa lakini kwa kuangalia hapo kwenye RED, unaonekana lengo lako ni lile la Wabongo wengi kukashifu Bongo Movie or else, sijui suala la makalio makubwa limetoka wapi manake, waigizaji wengi wana maumbo ya kawaida tu!!
Kama suala ni kutembea uchi, ni kundi lipi la wasichana na wadada wa makamo Tanzania hii ambao hawatembei uchi? Bongo Flavor? University students? College students? Secondary school students?! Wadada wa kawaida wa mjini?!
Tukija upande wa hoja yako ya elimu... ni field ipi unayozungumzia! Kwenye GREEN umehoji ikiwa kipaji is all what matters na kwenye BLUE umetoa mfano wa watu wenye shahada za criminology na sheria!!
Hivi huyo mtu wa degree in criminology, anaigiza kwa kutumia degree yake in criminology au ni kipaji tu ndicho kinambeba?! Ningekuelewa mia kwa mia endapo ungetoa mfano wa wenye kiwango cha elimu kwenye masuala ya acting or at least film.
Lakini kuhitimisha, naweza kusema with confidence kwamba hata elimu ya kidato cha nne kwa mazingira yetu inatosha sana kwa mwigizaji. Hata hivyo, haimaanishi kwamba elimu sio muhimu.
Ukilinganisha na waigizaji, watu walio nyuma ya kamera ndio muhimu zaidi kuwa na elimu mzuri hususani kwa directors and screenwriters kwa sababu, ubora (msisimiko) wa filamu unawategemea sana hawa watu kuliko Waigizaji!
Ukiona unaangalia filamu hadi unasinzia, lawama kubwa hapo zinatakiwa kwenda kwa mwandishi na director!! Ukiona filamu imekosa uhalisia, lawama kubwa zinatakiwa kwenda kwa mwandishi na directors na wakati mwingine producer. Ukiona mwigizaji ameboronga, lawama hapo ni kwa director kwa sababu ndie kazi yake kuhakikisha mwigizaji ana-deliver!
Of course, wakati mwingine yapo mapungufu ya kimazingira/location ambayo labda alitakiwa alaumiwe ama location manager or production designer (kama tunao basi) lakini hapo napo director hawezi kukwepa lawama kwa ku-approve sehemu ambayo ama ni irrelevant au hai-reflect uhalisia!
So, kwa waigizaji hao hao wa darasa la saba, endapo wanapata watu wazuri walio nyuma ya kamera, trust me, wanaweza kufanya kazi yenye level za Oscar. Kinyume chake, hata kama waigizaji wote wana shahada ya uigizaji kutoka vyuo maarufu kabisa duniani lakini timu nyuma ya kamera ni ya ujanja ujanja tu, basi filamu itakayotoka hapo itaboa tu kama filamu zingine za Bongo Movie!!!
Swali la msingi ni je, tunao hao watu wazuri nyuma ya kamera?! Kwavile hoja yako ni elimu bila kujali ni degree ya taaluma gani; jibu ni kwamba WAPO wenye degree! Tatizo, siamini kama wote wana passion na filamu... isije kukosa kazi ikawa ndo sababu ya kungia huko na matokeo yake, kwavile majority ya hawa hawajasomea film, basi hata ule ubunifu wa kifilamu pia hawana kwa sababu sio kitu kilicho kwenye damu yao!!!
Hawa watu wa nyuma ya kamera wanatakiwa kuwa na ubunifu wa ziada endapo hawana taaluma ya filamu! Na hata hao wenye taaluma pia wanatakiwa kuwa na ubunifu na ndio maana hata huko Hollywood, sio filamu zote zinakalisha ingawaje na zenyewe zinakuwa zimetengenezwa na watu wenye taaluma ya filamu!!!!