Hivi Bongo Movie kuna mtu ana elimu ya kiwango cha shahada(Degree)?

Hivi Bongo Movie kuna mtu ana elimu ya kiwango cha shahada(Degree)?

Habari ya jumamosi wakuu.

Najaribu kujiuliza, katika fani hii ya uigizaji Tanzania au maarufu kama Bongo Movie, kuna muigizaji ana elimu ya kiwango cha shahada au zaidi?

Nasikia kwenye Muziki wapo waimbaji wenye shahada moja na kuendelea kama Nick Mbishi kama sijakose anasikia ana shahada ya uzamili(masters degree).

Au Tanzania sanaa ya uigizaji imebakia kua ni kipaji hata kama hujui kusoma na kuandika. Wasanii wetu hawa kiwango chao cha shule kikoje. Au ndio vile ukiwa na matako makubwa na ukajua kutembea na chupi tu na dadies nyingi unakua muigizaji mkubwa?

The Rock ana shahada ya criminology, David Otunga ana Masters degree ya sheria toka Havard university, ni sehemu wa waigizaji wakubwa wenye shule kubwa.

Je Bongo movie hali yao ikoje?

Ahsante.
Wako wengi baadhi ni Dr chain, Mzee chiro na senga[emoji12] [emoji12]
 
Makonde
 
Kuelimika na kutajirika ni vitu viwili tofauti. Ila elimu Mara jitihada inaongeza sana wigo wa kufanikiwa kimaisha. Ukiwa na elimu na ukiteseka kimaisha ujue Kuna baadhi ya nati haziko sawa up stairs.
Namshukuru Mungu.... sina pesa ndeeefu ila alhamdulillah. Lakini sina elimu. Ni msingi tu. Shida ya kutokua na elimu naiona sana. Wawe wabunifu na wafikirifu hawa watu wa bongo movie. Superstars wengi hawakusoma ila wabunifu wapo makini na wameajiri waliosoma.
Mmesahau tatizo moja tu kutokana na mada husika pamoja na post yng. Tatizo hilo ni kwamba KUELIMIKA NA KUWA NA DEGREE NI VITU VIWILI TOFAUTI, JAPO PIA HUTEGEMEANA....!!!

Unaweza ukawa na degree but hujaelimika na unaweza ukawa huna degree ila umeelimika.

Sent from my D5322 using JamiiForums mobile app
 
Au Tanzania sanaa ya uigizaji imebakia kua ni kipaji hata kama hujui kusoma na kuandika. Wasanii wetu hawa kiwango chao cha shule kikoje. Au ndio vile ukiwa na matako makubwa na ukajua kutembea na chupi tu na dadies nyingi unakua muigizaji mkubwa?

The Rock ana shahada ya criminology, David Otunga ana Masters degree ya sheria toka Havard university, ni sehemu wa waigizaji wakubwa wenye shule kubwa.
Sijaelewa msingi wa hoja yako ni nini hasa lakini kwa kuangalia hapo kwenye RED, unaonekana lengo lako ni lile la Wabongo wengi kukashifu Bongo Movie or else, sijui suala la makalio makubwa limetoka wapi manake, waigizaji wengi wana maumbo ya kawaida tu!!

Kama suala ni kutembea uchi, ni kundi lipi la wasichana na wadada wa makamo Tanzania hii ambao hawatembei uchi? Bongo Flavor? University students? College students? Secondary school students?! Wadada wa kawaida wa mjini?!

Tukija upande wa hoja yako ya elimu... ni field ipi unayozungumzia! Kwenye GREEN umehoji ikiwa kipaji is all what matters na kwenye BLUE umetoa mfano wa watu wenye shahada za criminology na sheria!!

Hivi huyo mtu wa degree in criminology, anaigiza kwa kutumia degree yake in criminology au ni kipaji tu ndicho kinambeba?! Ningekuelewa mia kwa mia endapo ungetoa mfano wa wenye kiwango cha elimu kwenye masuala ya acting or at least film.

Lakini kuhitimisha, naweza kusema with confidence kwamba hata elimu ya kidato cha nne kwa mazingira yetu inatosha sana kwa mwigizaji. Hata hivyo, haimaanishi kwamba elimu sio muhimu.

Ukilinganisha na waigizaji, watu walio nyuma ya kamera ndio muhimu zaidi kuwa na elimu mzuri hususani kwa directors and screenwriters kwa sababu, ubora (msisimiko) wa filamu unawategemea sana hawa watu kuliko Waigizaji!

Ukiona unaangalia filamu hadi unasinzia, lawama kubwa hapo zinatakiwa kwenda kwa mwandishi na director!! Ukiona filamu imekosa uhalisia, lawama kubwa zinatakiwa kwenda kwa mwandishi na directors na wakati mwingine producer. Ukiona mwigizaji ameboronga, lawama hapo ni kwa director kwa sababu ndie kazi yake kuhakikisha mwigizaji ana-deliver!

Of course, wakati mwingine yapo mapungufu ya kimazingira/location ambayo labda alitakiwa alaumiwe ama location manager or production designer (kama tunao basi) lakini hapo napo director hawezi kukwepa lawama kwa ku-approve sehemu ambayo ama ni irrelevant au hai-reflect uhalisia!

So, kwa waigizaji hao hao wa darasa la saba, endapo wanapata watu wazuri walio nyuma ya kamera, trust me, wanaweza kufanya kazi yenye level za Oscar. Kinyume chake, hata kama waigizaji wote wana shahada ya uigizaji kutoka vyuo maarufu kabisa duniani lakini timu nyuma ya kamera ni ya ujanja ujanja tu, basi filamu itakayotoka hapo itaboa tu kama filamu zingine za Bongo Movie!!!

Swali la msingi ni je, tunao hao watu wazuri nyuma ya kamera?! Kwavile hoja yako ni elimu bila kujali ni degree ya taaluma gani; jibu ni kwamba WAPO wenye degree! Tatizo, siamini kama wote wana passion na filamu... isije kukosa kazi ikawa ndo sababu ya kungia huko na matokeo yake, kwavile majority ya hawa hawajasomea film, basi hata ule ubunifu wa kifilamu pia hawana kwa sababu sio kitu kilicho kwenye damu yao!!!

Hawa watu wa nyuma ya kamera wanatakiwa kuwa na ubunifu wa ziada endapo hawana taaluma ya filamu! Na hata hao wenye taaluma pia wanatakiwa kuwa na ubunifu na ndio maana hata huko Hollywood, sio filamu zote zinakalisha ingawaje na zenyewe zinakuwa zimetengenezwa na watu wenye taaluma ya filamu!!!!
 
Mmesahau tatizo moja tu kutokana na mada husika pamoja na post yng. Tatizo hilo ni kwamba KUELIMIKA NA KUWA NA DEGREE NI VITU VIWILI TOFAUTI, JAPO PIA HUTEGEMEANA....!!!

Unaweza ukawa na degree but hujaelimika na unaweza ukawa huna degree ila umeelimika.

Sent from my D5322 using JamiiForums mobile app
Mkuu ukiangalia vizuri sijapost kitu tofauti na post yako wala sijaigusa kabisa. Nimeisoma na kuielewa na ina point zake muhimu. Ila ukiangalia nilichoandika nilijibu mtu aliesema kua elimu si kitu na kujutia miaka yake mitatu alioipoteza chuoni.
 
Bongo movie inakabiliwa na changamoto ya ujinga kichwani, yaani shule hamna wanashindwa kupambanua mambo katika serikali ya vichwa vyao ndio maana wanatoa movie hazieleweki hata kidogo. Ni pumba tu, hawa wakina wema sijui nani huko wote hawa Hamna afadhali hata kidgo, maana WENGI WANADHARAULIKA KWA KUONEKANA WAHUNI na vilevile Kwa sasa BONGO MOVIE inaonekana ni tasnia ya uhuni yaani mtu akishaingia bongo movie tayari anaonekana muhuni sababu wote hamna shule kabisa.

Shule ni heshima jamani mkatae mkubali inaheshima yake endapo ukiwa na shule na ukaitumia vizuri
 
Wabongo wanaabudu sana vyeti kuliko maarifa, maarifa yapo vitabuni, Dhana ya kuelumika ni pana sana kuliko kuwa na cheti .Cheti unapata ukikaa darasani na kuhitimu katika muda uliopangwa, Elimu ni kujifunza kila siku. Na kuna njia nyingi za kujifunza. Tatizo la Bongo movie ni waandika scrips na waongozaji, hawa hatuna, muigizaji anaongozwa.
 
Arnold Schwarzenegger
1335466420-celebrity-arnold-schwarzenegger-150x150.jpg

  • College: University of Wisconsin-Superior
    Degree Earned: Bachelor's in Business and International Economics
Dolph Lundgren
upload_2017-10-29_12-51-59.jpeg

  • College: Royal Institute of Technology
    Degree Earned: Bachelor's in Chemical Engineering
hawa ni baadhi ya magwiji wa filamu na bachelor zao mkononi
 
Huyo ni kilaza.

Unajua haya ndio matatizo ya Cocacola kufunga free Wifi milembe, sasa hata machizi wana access na mtandao.

Ndio maana nimempa mifano mingine, kama anadhani Diamond ndie mwenyewe asie na shule mwenye hela, nimempa mifano mingine.

Hoja hapa sio hela, ni shule. Mtu anatoka huko amebanwa na mavi anakuja kuharisha humu.
Ha ha ha ha ha ha! Nimeipenda Sana hasa hapo pakuja amebanwa mavi halafu anakuja kuharisha humu. Hawa ni wale wenzetu ambao hawakusoma shule halafu wanajifichia kwenye migongo ya ambao hawajasoma tena wachache mno wenye mafanikio!
 
Mawazo ya kijinga na kimasikini. Mawazo ya kukata tamaa ya maisha.

Huwezi ku-ignore umuhim wa shule kisa wewe huna kazi.

Madhumuni ya msingi ya elimu sio kukusaidia upate kazi, ni kukuondolea ujinga na utaahira kichwani mwako, ni kufungua kichwa chako.

Wewe bado hujaenda shule. Rudi shule.
Elimu ya bure kabisa umetoa mkuu humu bahati mbaya wagonjwa wengi
 
Elimu ya bure kabisa umetoa mkuu humu bahati mbaya wagonjwa wengi
Ni wajinga tu wanaweza ku-ignore umuhimu wa shule.

Nimeona hii msanii wa muziki wa Bongo Flava Alikiba akisema ni muhimu msanii kua na elimu ili ufanye mambo yako vizuri.

Rich mavoko pia aliwahi kuwaasa wasanii wenzake kuzingatia umuhimu wa shule.
Screenshot_20171029-141034.png
 
Kama wana hela, hizo degree sio ishu sana. Hela ndo za msingi. Kujisifia degree ni kizamani sn mkuu. Mi mwnyw na elimu yng maisha yananipiga vitasa vya uso kichizi yn. Bora hata ile miaka mi3 ya chuo, ningekuwa nipo kitaa nasaka noti.
Embu nitajie bongo movie mwenye hela.
 
Back
Top Bottom