Hivi Bongo Movie kuna mtu ana elimu ya kiwango cha shahada(Degree)?

Mwambie kwamba pia katika jambo kuna exceptions
 
Kwakweli uigizaji wa bongo bdo kizunguzungu
Napenda uzalendo ila sio Wa kuangalia bongo muvie .,maadili tu yenyew ya kitanzania 0
 
Bro chige kazungunza vizuri sana, tusiwalaumu hawa wasanii wa movie bali tunatakiwa kuwalaumu hawa Mwandishi wa story, Director, Editor na Producer. hawa ndio watu muhimu na hawa ndio wanapaswa hasa kusomea kipaji chao ili kuwa wabunifu zaidi na kuwashape waigizaji wetu vizuri.

Mfano waigizaji wengi wa Korea, wamesomea mambo ya sanaa hivyo ndio unatakiwa uwe kipaji+kukiendeleza kipaji chako.

Huwezi kujinadi una degree ya uchumi huku unafanya movie hlf ujitape eti mimi nimeelimika ila nitakuelewa sana kama wewe ni muigizaji hlf una degree ya uigizaji(sijui kama ipo ni mfano)

Sasa kwa hawa wasanii wetu kiwango cha form four si kibaya ila wanapaswa wakasomee kile wanachokifanyia kazi na sio tu chuo cha sanaa Bagamoyo wanaweza kutoka hata nje ya hapo ili kuongeza maarifa zaidi.

Good Luck to them.
 
Kuna yule anajiita Pastor Mayamba, ni classmate wa Joshua Nasari, Nick Mbishi na masela wengine. Na ni graduate wa udsm Sociology, wote wakiwa social policy planning and administration.

Mwingine ni Sajo aliimba na Mhogo mchungu, ni graduate wa Bachelor of Arts in Fine and Performing Arts. Sijui kwa sasa yuko wapi

Halafu katika wale walimbwende, si kuna mmoja alishinda akiwa ni mwanafunzi udsm?
 
sasa na wewe, ukiwa na degree utakuwaje bongo movie? you become a bongo movie baada ya shule kushindwa na akili yako haijawa nzuri sana. mtu mwenye staha na elimu ni vigumu sana kuigiza. the worse thing ni kwamba, akili zetu zinalishwa na watu wasio na elimu na ufahamu mzuri, na ndiyo society tunayoijenga. kuna watu wanaishi maisha ya bongo movie, hawawezi kupita hapo.
 
Unajua mashaka yangu hadi kuuliza hili swali yanatokana na kwamba ijumaa niliwahi kurudi hom, kisha nikajichanganya sebuleni, nikakuta watu wanaangalia hizo sinema za Bongo, kisha nikamuona dogo mmoja nilisoma nae Ordinary Level Secondary school, alikua nyuma yangu darasa moja ila tunafahamiana ingawa ni miaka mingi hatujaonana, nikamuona kwenye hizo sinema, nikashangaa zaidi toka lini huyu dogo ni muigizaji. Huyu dogo ni kilaza kweli kweli, ila sasa ni muigizaji mkubwa. Alifikia form four akapata sifuri.

Anyway, najua hakuna kanuni ya kufanikiwa katika maisha ila nilitaka tu kujua kama kweli hii tasnia ina watu walioenda shule.
 
Degree ni upuuzi tu,,, there are lots of people having degrees and still cannot do a damn thing!!
Uneducated people are very brilliant!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…