Habari ya jumamosi wakuu.
Najaribu kujiuliza, katika fani hii ya uigizaji Tanzania au maarufu kama Bongo Movie, kuna muigizaji ana elimu ya kiwango cha shahada au zaidi?
Nasikia kwenye Muziki wapo waimbaji wenye shahada moja na kuendelea kama Nick Mbishi kama sijakose anasikia ana shahada ya uzamili(masters degree).
Au Tanzania sanaa ya uigizaji imebakia kua ni kipaji hata kama hujui kusoma na kuandika. Wasanii wetu hawa kiwango chao cha shule kikoje. Au ndio vile ukiwa na matako makubwa na ukajua kutembea na chupi tu na dadies nyingi unakua muigizaji mkubwa?
The Rock ana shahada ya criminology, David Otunga ana Masters degree ya sheria toka Havard university, ni sehemu wa waigizaji wakubwa wenye shule kubwa.
Je Bongo movie hali yao ikoje?
Ahsante.