Hivi BOT na TCRA wako wapi hizi riba za mikopo ya Tigo na Airtel?

Hivi BOT na TCRA wako wapi hizi riba za mikopo ya Tigo na Airtel?

Kwa hiyo nisiuze nikalipe madeni ya wakulima na mbegu nisubiri mkimaliza kujenga kiwanda?
Sasa tutafanyaje mkuu wakati nambari wan ndo kashasema Tanzania ni ya viwanda??

Enzi za Kilimo kwanza zimeshapita mkuu.
 
Sasa tutafanyaje mkuu wakati nambari wan ndo kashasema Tanzania ni ya viwanda??

Enzi za Kilimo kwanza zimeshapita mkuu.
Hehe, sorry brother niliquote vibaya.
 
Wanajukwaa habari, nimekuwa nikijiuliza, hizi taasisi za serikali mbona ziko kimya sana, wakati.ndizo.zenye jukumu la kumlinda mlaji wa mikopo hii ya kwenye simu kutoka tigo na airtel ambao kiukweli wanamwibia mteja. Tigo ukikopa shilingi 120,000/= kwa siku 21 unatakiwa urudishe shilingi 144,600/= ambayo hii ni sawa na riba ya 27.3% kwa mwezi au 328% kwa mwaka, jamani huu ni wizi, hata kama hii mikopo risk yake ipo juu.

Airtel wao ukikopa shilingi 136,000/= utatakiwa urudishe shilingi 161,092/= baada ya siku 21 ambayo ni sawa na riba ya 24.6% kwa mwezi au 320% kwa mwaka.

Kidogo afadhali ni voda ambao wao wanakopesha kwa mwezi, ukikopa shilingi 46,000/= utalipa shilingi 50,140/= baada ya mwezi mmoja, hii ni sawa na riba ya 9% kwa mwezi au 108% kwa mwaka. Japo hii iko juu ila ni nafuu ukilinganisha na mitandao mingine.

Kwa hili naomba BOT na TCRA waingilie kati kulinda haki ya mteja, badala ya kuyaacha haya makampuni ya simu yakiwaibia wateja

Nawasilisha.
Lakini wakati wa kukopa si ulikubali masharti na vigezo lawama za nini Kama ulikuwa unajua gharama ziko juu kwa nini ulijiunga mpaka unaweka password ulikuwa hujui kwamba ni asilimia ishirini na moja acheni mambo ya ajabu kama kitu huwezi unaacha na sio umeshakopa unakuja hapa kulalamika tu pasipo sababu.
 
Risk kweli kubwa nilikopa laki pumbavu tigo, wanakukata ribw bado ela ya kutolea, nimewadhurumu mpk leo cwalipi
 
Acha usumbufu, USIKOPE!
Wewe ndiyo unajua faida na hasara, achana nao kama riba kubwa nenda VICOBA
 
Sema wanasaidia, Lakini Airtel Money ndo wezi , Mimi wananikopa laki saba lakini baada ya wiki tatu unarudisha riba 185,000 , VODA hao angalau lakini Mkopo wao ni pesa kidogo mimi wananikopesha mwisho laki nne,
Kama wewe ni mfanyabiashara, tena wa jati au mkubwa, it makes sense, lakini kama ni mfanyakazi, mwalimu kama mimi, ninayetegemea kulipa kwa kutumia mshahara hizi riba ni kubwa sana wajameni
 
Back
Top Bottom