MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,252
- 8,003
Tunapojiita kua tuna bunge badala ya kufanya kazi ya kuishauri na kuisimamia serikali badala yake linafanya kazi ya kuitetea serikali ni hasara kwa taifa kupoteza mabilioni ya shilingi kuwalipa mishahara.
Mmekaa mnapitisha tozo ambazo ni maumivu kwa Watanzania tena kwa kishindo mnagonga meza. Mmetusaliti wapiga kura wenu kwa kiasi kikubwa na mimi kama kada mkongwe wa CCM ninaomba Mungu 90% ya wabunge msirudi bungeni 2025, mnakula mishahara isiyokuwa stahiki yenu.
Mnaona raha tu mnapitisha kitu mpaka watanzania wanapiga kelele na Mhe Rais anatoa maagizo anaona si sawa, ninyi hamna sifa kabisa za kua wawakilishi. Mlienda kumwakilisha nani Kama mnawageuka wapiga kura wenu?