Pre GE2025 Hivi CCM huwapa nini Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na kupelekea wao kukaa kimya hata pasipobidi?

Pre GE2025 Hivi CCM huwapa nini Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na kupelekea wao kukaa kimya hata pasipobidi?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Na vipi ingekuwa Chadema bila EL kupata nafasi yakugombea, Chadema ikasimamisha mtu wao toka ndani ya chama?

Vyovyote vile, kwa hakika matatizo lukuki ya kiuchumi na kijamii, uchumi ikiwa sababu kuu ndiyo inafaa kutumika kuwaunganisha watanzania ili tuondoe mifumo dhaifu iliyopo sasa.

Tukitumia uchama, udini, ukabila, ukanda tutakuwa tunazunguka duara tu.

Mimi binafsi napenda sana kuona sheria ya mgombea binafsi inakuwepo ili viongozi wa kweli bila kuwa na mfungamano na chama anaweza kuwapatia watu wake plan ya maendeleo iwe ngazi ya mtaa, wilaya, jiji au nchi.

Kudhani watu wanaotoka katika vyama vya siasa pekee ndiyo wanastahili kuwa viongozi si sahihi.
Kwa nguvu ya raisi wa JMT, mgombea binafsi hapana. Labda tupunguze nguvu ya hicho kiti. Pamoja na udhaifu wote ila angalau kichaa akishika nchi chama kinaweza mpa usumbufu wa baadhi ya maamuzi.
 
Hilo ndilo swali huwa najiuliza siku zote.

Wazi huwa yapo mambo mengi ambayo kwa macho ya kawaida kabisa, huhitaji Vyombo vya Dola viikemee Serikali inayoongozwa na CCM kwa kuhatarisha usalama wa Taifa. Ajabu wala hawajishughulishi!

Mbaya zaidi, CCM hutumia sababu ya machafuko kama silaha ya kuwatisha wapenda haki eti Nchi itasambaratika.

Shime wana usalama, wakati umefika muwe upande wa Wananchi wa kawaida. Kuendelea kuilea CCM kama mtoto pendwa ipo siku ulezi huo utazaa haramu.
Ungeshauri hivyo wakati Dictator uchwara alipochafua uchaguzi wa 2020
 
Jeshi lipo kwa ajili ya kulinda raia, amani, mipaka ya ardhi na mali za raia na si jambo lingine.

Uchaguzi u karibu mnoo, Tupe mbadala wa CCM tujipime na kama hatutoshi raia wataamua.

2025-2030 CCM ITAPEWA TENA NAFASI YA KUIONGOZA NCHI YETU.
Hii sio kweli👉Jeshi lipo kwa ajili ya kulinda raia, amani, mipaka ya ardhi na mali za raia na si jambo lingine."
Jeshi lipo kwa ajili ya maslahi ya establishment,sio wananchi,msidanganye watu.

Finally,CCM is not indipensable,ila mmetengeneza mazingira ya kuifanya iwe indispensable,shame on you.
 
Kwa nguvu ya raisi wa JMT, mgombea binafsi hapana. Labda tupunguze nguvu ya hicho kiti. Pamoja na udhaifu wote ila angalau kichaa akishika nchi chama kinaweza mpa usumbufu wa baadhi ya maamuzi.
Mbona marais wa Tanzania wanafanya chochote wanachojisikia na hakuna wakuwazuia?

Mkapa, Kikwete, Magufuli na Samia hawa hawatoki kwenye chama?

Wewe huoni ccm inavyounga mkono kila kitu anachofanya president?

Tukiamua kuwa na mgombea binafsi maana yake lazima tutaona umuhimu pia wa president kuwa na mipaka na si kuwa mfalme.

Kiongozi si lazima atoke ndani ya chama cha siasa.

Mazoea tu hayo.
 
Mbona marais wa Tanzania wanafanya chochote wanachojisikia na hakuna wakuwazuia?
Katiba imewapa nguvu, Chama ni kama ukuta katika hiyo nguvu waliyopewa.
Mkapa, Kikwete, Magufuli na Samia hawa hawatoki kwenye chama?
Wanatoka kwenye chama, na pamoja na nguvu waliyonayo Chama somehow kimewapa ukomo wa maamuzi. Hayo waliyoyafanya imagine kusingekuwa na chama. Mfano, ukomo wa madaraka, mchakato wa kutawala milele ukiletwa ccm kunaweza kukakuwepo upinzani kutoka katika chama.
Wewe huoni ccm inavyounga mkono kila kitu anachofanya president?
Baada ya vikao vyao vya ndani na kukubaliana.
Tukiamua kuwa na mgombea binafsi maana yake lazima tutaona umuhimu pia wa president kuwa na mipaka na si kuwa mfalme.
Kabla ya mgombea binafsi kwanza nguvu ya raisi ipunguzwe mno. Tutaletewa mtu na matajiri huko nje mkija shtuka ni too late.
Kiongozi si lazima atoke ndani ya chama cha siasa.
Kwa sasa Tanzania bara na visiwani ni lazima.
Mazoea tu hayo.
Ni katiba na sheria zetu.
 
Hii sio kweli👉Jeshi lipo kwa ajili ya kulinda raia, amani, mipaka ya ardhi na mali za raia na si jambo lingine."
Jeshi lipo kwa ajili ya maslahi ya establishment,sio wananchi,msidanganye watu.
Soma Katiba ya nchi yako kuelewa majukumu ya Jeshi la nchi yako.
Finally,CCM is not indipensable,ila mmetengeneza mazingira ya kuifanya iwe indispensable,shame on you.
Unaonekana ni mtu unayependa nadharia au mambo ya kufikirika. Kupiga kura against CCM ni haki yako kama ilivyo haki ya watakao ipigia kura 2025.
 
Soma Katiba ya nchi yako kuelewa majukumu ya Jeshi la nchi yako.

Unaonekana ni mtu unayependa nadharia au mambo ya kufikirika. Kupiga kura against CCM ni haki yako kama ilivyo haki ya watakao ipigia kura 2025.
Aisee,so you believe Katiba ndio muarobaini wa matatizo ya nchi na ukweli wote,sio kweli.Katiba is just a tool for manipulating the unsuspecting masses and imposing the "wishes" of the establishment on the citizenry.That is what the Constitution is,mmelishwa matango, wake up.
 
Back
Top Bottom