Hivi changamoto ni CHADEMA au Tundu Lissu? Wananchi wajue

Mwana kondoo 2025

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2025
Posts
495
Reaction score
580
Mimi nimetafakari na kujiuliza, je, tatizo la CHADEMA ni chama na sera zake au pengine ni uwepo wa Tundu Lissu kwenye chama hicho na misimamo yake?

Hili linahitaji mjadala mpana sana kwa sababu CHADEMA ni taasisi inayoishi—Lissu atakuwemo na kutoka; pengine ataenda DP, au ataacha siasa, au hata kufariki. Lakini CHADEMA, kwa hali ya kawaida, itaendelea kuwepo.

Chama ni mali ya wananchi kama mimi, ndiyo maana kwenye usajili wake lazima kithibitishe kuungwa mkono Tanzania Bara (Tanganyika) na Zanzibar.

Hii ndiyo sifa kuu ya kukubaliwa kwa usajili kamili. Kama ndivyo, basi kuifuta CHADEMA hakutasaidia wanachama na wananchi kwa ujumla wake.

Naamini kwamba leo kikifutwa, baadhi ya wanachama watahamia kule Lissu atakakohamia—labda DP au UDP. Hivyo, kama tatizo lilikuwa ni Lissu, basi CHADEMA kitakuwa kimeadhibiwa bure.

Mfano wa karibu ni suala la Gwajima kwenye Kanisa la Ufufuo na Uzima kwa wafuasi wake.

Hii njia ya kufuatilia mtu mmoja badala ya taasisi ni hatari na si nzuri. Ni kama kutoka katika mfumo wa kushughulikia taasisi (institutional/systems approach) hadi mfumo wa mtu binafsi (individualistic approach).

Ni muhimu tushughulikie watu binafsi wenye matatizo binafsi na serikali, tukiacha taasisi ziendelee na kazi zake kwa mujibu wa sheria.

Hatua hii itasaidia kuepuka kuwaadhibu wananchi walio na matumaini na taasisi husika, na pia kuepuka kuchochea chuki dhidi ya serikali yao.

Tubane wigo wa chuki kwa kushughulika na watu binafsi wenye migongano na serikali.

Pia, tuangalie kwamba masuala ya kisiasa yashughulikiwe au yajibiwe kisiasa kwenye majukwaa, ili vyombo vya dola vibaki na kazi yake ya msingi ya kulinda amani, usalama na sheria. Jambo hili liende sambamba na maridhiano kati ya hao watu binafsi au influencers, ili kuweza kujenga umoja wa kitaifa kwa njia ya kitaasisi.

Tujadili.
 
Mimi nimetafakari na kujiuliza je tatizo la chadema ni chama na sera zake au pengine ni Uwepo wa Tundu Lissu kwenye chama hicho na misimamo yake. Hili linahitaji mjadala mpana sana kwa sababu Chadema ni Taasisi inayoishi Lisu atakuwemo na kutoka pengine ataenda DP au ataacha siasa au kufariki nk. chadema kwa hali ya kawaida itakuwepo. Chama ni mali ya wananchi kama mimi ndiyo maana kwenye usajiri wake lazima kithibitishe kuungwa mkono Tanzania bara Tanganyika na Zanzibar. Ndiyo sifs kuu ya kukubaliwa usajiri. Kama ndivyo kwa kuifuta chadema haitasidia wanachama na wananchi kwa ujumla wake. Naamini leo kikifutwa wanachama watahamia kule Lissu atakohamia labda DP au UDP hivyo kama tatizo lilikuwa ni Lisu chadema kitaadhibiwa bure misili ya suala la Gwajima kwenye kanisa la ufufuko na uzima kwa wafuasi wake. Hii ni hatari kuliko kumshughulikia mtu. Yaani from instituonal /systems approach to individual approach. Hii itasaidia kuepukana na wananchi walio na tegemeo kwa taasisi husika kuadhibiwa na kujenga chuki kwa serikali yao. Tubane wigo wa chuki kwa kushughulika na watu binafsi wenye migongano na serikali. Pia tuangalie masuala ya kisiasa yashughulikiwe/ yajibiwe kisiasa kwenye majukwaa ili kuviacha vyombo vya dola kushughulika na majukumu ya ya kimsingi. Tujadili.
Chama ni mali ya umma. Ndio maana kinatumia rasilimali na ruzuku za umma.

Ni mwendelezo tu kama watu wanafuta kanisa watashindwa Chama?
 
Kinacho tokea ni matokeo ya kumulika mnyama au Lidude hatari ambalo liliamini hapa liko salama kwenye himaya yake sasa unapo lisogelea na kuweka mwanga ili wengine waone na muanze kulikabili ili kuliangamiza ndipo mtakumbana na athari kama za kutemewa mate yenye sumu mara vishindo vitasikika maana lina nguvu
Lkn pia ushindi ndio upo hapo hapo maana hili Lidude kuliona tu ni hatua kubwa sana maana huwa halionekani kirahisi kinacho onekana ni athari zake hivyo haya ni mapambano muhim na huu ndio wakati wa kushirikianna zaidi kama wawindaji maana likitutoka hapa wote tumekwisha hakuna atakakye baki salama
 
Hata mkiifuta CHADEMA! Bado hamtatua tatizo la msingi. Kutakako kuwepo na na viongozi wazalendo na wapigania nchi yao kama Lissu, Heche na wengineo; tutahamia huko huko.

Kimsingi wananchi tunataka mabadiliko ya kweli kwenye hii nchi. Tumechoka kutawaliwa na magenge ya wahuni.
 
Watahamia hicho chama atakachoenda Lissu na Heche baada ya chadema kufutwa itasumbua sana serikali labda kumwondoa kabisa vinginevyo tunakaribisha siasa za Kenya za hamahama viongozi kwa vyama vingine kwa convenience ya madara siyo kuhudumia wananchi kichama.
 
Chama ni mali ya wananchi kama mimi, ndiyo maana kwenye usajili wake lazima kithibitishe kuungwa mkono Tanzania Bara (Tanganyika) na Zanzibar.

Tujadili.
Huu ni upuuzi kama sheria hii ipo, kuna ulazima upi chama kinacho fanya siasa zake kwa asilimia 95 Tanganyika iwe lazima kikubalike Zanzibar??? Watu ambao hata ki utamaduni tupo tofauti??

Wao ccm na wapuuzi wachache wa huko visiwani, kwa matakwa yao waliamua kuunganisha vyama vyao, kisha wakaitoa sadaka Tanganyika kwa wake zao ikaishia hapo.

Sasa iweje leo, mimi nina harakati zangu, nina pambania ndugu zangu wa damu, unakuja unasema eti ooh!!! Ili tupambane nilazima ukaowe nilipooa mimi.

sisi tunawajua hiyo familia uliyooa wewe ni wapuuzi na wajivuni, hatuwezi kuoa nyumba hiyo, wewe ulihonga shamba la familia(Tanganyika) inaatosha.

Chadema hakihitaji kuwa na kiongozi kutoka Zanzibar ili kuwa chama, na sio kiongozi tu, hakihitaji hata kuwa mwanachama kawaida kabisaaaa yule wa ngazi ya chini, achana na mwanachama, chadema hakihitaji nata kuwa na shabiki Zanzibar ili kuwa chama.

Waacheni hao wapuuzi wahangaike wao na wake zao, wakijua wenyewe watachaguanaje, sisi watanganyika tunahitaji chama kinacho jiendesha Tanganyika peke yake

Si mnaona wanatusaliti hawa, leo wamejaribu wamekipiga nyundo mahakamani chama, hakitakiwi kufanya chochote, hakuna mikutano, hakuna michango hakuna nini, leo wakifanikisha watatumia sheria hiyo kutukwamisha kila siku.

Hili tulipiganie Watanganyika woote bila kujali chama.

Tanu na hao wengine waliungana wao, kisha tanu, chini ya Nyerere wakahonga shamba la familia.

Tanganyika yetu nzuri ya kupendeza ikapotea mchana kweupeee peee!!!!

Hii nchi ya Tanganyika tuliachiwa urithi na babu zetu, wakoloni walipovamia, babu zetu walijitahidi sana kuipambania nchi yetu, ila kwa uduni wa silaha walishindwa(hatuwezi kuwalaumu) nchi ikaingia utumwani chini ya wakoloni.

Mzungu kanyonya weeeeee maziwa ya ng'ombe huyu Tanganyika mpaka kachoka, mwisho katupa uhuru, katukabidhi urithi wetu baada ya kuwaua babu zetu

Muda umefika, Nyerere kapewa nchi, nae sijui kilimsibu nini kaenda kuhonga nchi yetu nzuri kwa mkataba usio na uzani kabisa.

Hivi kulikua na ulazima upi wa Tanganyika kujitoa kiasi kile kwenye muungano???

kama muungano ingetosha kuunganisha chama chake cha tanu na kile cha huko upande wa pili, waendeshe mambo yao, ki vyao vyao.

Kuhusu kuchaguana bungeni watajuana wao, sisi tunaweza kuwapa nafasi moja tu ya huruma bungeni, wanakua na mtu mmoja tu anakua anaiwakilisha Zanzibaryoote kwenye bunge letu tena inabidi asiwe na sauti yoyote, ule muda wa kupiga stori bungeni ndio yeye anawashiwa mic atuchekeshe kidogo inaishia hapo.

sijuagi hata chama cha huko Zanzibar kilichoungana na tanu kinaitwaje, kuna wakati naendaga kukojoa baharini nikiamini wazanzibary wanapoogelea folozani watakua wanakunywa mikojo yangu)

Mimi nilipokuwa secondary, katika mtihani, maswali yoote yanayohusu Zanzibar nilikua siyajibu, yaani hata walete swali za Zanzibar kwenye maths, mie naliacha sijibu.

Hawa sio ndugu zetu.

NB.
Na nyie ma mods hapo jf, msijaribu kufanya chochote kwenye komenti yangu. Acheni ukweli usemwe
 
Huu ni upuuzi kama sheria hii ipo, kuna ulazima upi chama kinacho fanya siasa zake kwa asilimia 95 Tanganyika iwe lazima kikubalike Zanzibar??? Watu ambao hata ki utamaduni tupo tofauti??

Wao ccm na wapuuzi wachache wa huko visiwani, kwa matakwa yao waliamua kuunganisha vyama vyao, kisha wakaitoa sadaka Tanganyika kwa wake zao ikaishia hapo.

Sasa iweje leo, mimi nina harakati zangu, nina pambania ndugu zangu wa damu, unakuja unasema eti ooh!!! Ili tupambane nilazima ukaowe nilipooa mimi.

sisi tunawajua hiyo familia uliyooa wewe ni wapuuzi na wajivuni, hatuwezi kuoa nyumba hiyo, wewe ulihonga shamba la familia(Tanganyika) inaatosha.

Chadema hakihitaji kuwa na kiongozi kutoka Zanzibar ili kuwa chama, na sio kiongozi tu, hakihitaji hata kuwa mwanachama kawaida kabisaaaa yule wa ngazi ya chini, achana na mwanachama, chadema hakihitaji nata kuwa na shabiki Zanzibar ili kuwa chama.

Waacheni hao wapuuzi wahangaike wao na wake zao, wakijua wenyewe watachaguanaje, sisi watanganyika tunahitaji chama kinacho jiendesha Tanganyika peke yake

Si mnaona wanatusaliti hawa, leo wamejaribu wamekipiga nyundo mahakamani chama, hakitakiwi kufanya chochote, hakuna mikutano, hakuna michango hakuna nini, leo wakifanikisha watatumia sheria hiyo kutukwamisha kila siku.

Hili tulipiganie Watanganyika woote bila kujali chama.

Tanu na asp waliungana wao, kisha tanu, chini ya Nyerere wakahonga shamba la familia(Tanganyika yetu nzuri ya kupendeza) inatosha hapo. Kuhusu kuchaguana bungeni watajuana wao, sisi tunaweza kuwapa nafasi moja tu ya huruma bungeni, wanakua na mtu mmoja tu anakua anaiwakilisha Zanzibaryoote kwenye bunge letu tena inabidi asiwe na sauti yoyote, ule muda wa kupiga stori bungeni ndio yeye anawashiwa mic atuchekeshe kidogo.

sijuagi hata chama cha huko Zanzibar kilichoungana na tanu kinaitwaje, kuna wakati naendaga kukojoa baharini nikiamini wazanzibary wanapoogelea folozani watakua wanakunywa mikojo yangu)

Mimi nilipokuwa secondary, katika mtihani, maswali yoote yanayohusu Zanzibar nilikua siyajibu, yaani hata walete swali za Zanzibar kwenye maths, mie naliacha sijibu.

Hawa sio ndugu zetu.

NB.
Na nyie ma mods hapo jf, msijaribu kufanya chochote kwenye komenti yangu.
Subirini mabadiliko yapo njiani.

🚶🚶🚶
 
Mimi nimetafakari na kujiuliza, je, tatizo la CHADEMA ni chama na sera zake au pengine ni uwepo wa Tundu Lissu kwenye chama hicho na misimamo yake?

Hili linahitaji mjadala mpana sana kwa sababu CHADEMA ni taasisi inayoishi—Lissu atakuwemo na kutoka; pengine ataenda DP, au ataacha siasa, au hata kufariki. Lakini CHADEMA, kwa hali ya kawaida, itaendelea kuwepo.

Chama ni mali ya wananchi kama mimi, ndiyo maana kwenye usajili wake lazima kithibitishe kuungwa mkono Tanzania Bara (Tanganyika) na Zanzibar.

Hii ndiyo sifa kuu ya kukubaliwa kwa usajili kamili. Kama ndivyo, basi kuifuta CHADEMA hakutasaidia wanachama na wananchi kwa ujumla wake.

Naamini kwamba leo kikifutwa, baadhi ya wanachama watahamia kule Lissu atakakohamia—labda DP au UDP. Hivyo, kama tatizo lilikuwa ni Lissu, basi CHADEMA kitakuwa kimeadhibiwa bure.

Mfano wa karibu ni suala la Gwajima kwenye Kanisa la Ufufuo na Uzima kwa wafuasi wake.

Hii njia ya kufuatilia mtu mmoja badala ya taasisi ni hatari na si nzuri. Ni kama kutoka katika mfumo wa kushughulikia taasisi (institutional/systems approach) hadi mfumo wa mtu binafsi (individualistic approach).

Ni muhimu tushughulikie watu binafsi wenye matatizo binafsi na serikali, tukiacha taasisi ziendelee na kazi zake kwa mujibu wa sheria.

Hatua hii itasaidia kuepuka kuwaadhibu wananchi walio na matumaini na taasisi husika, na pia kuepuka kuchochea chuki dhidi ya serikali yao.

Tubane wigo wa chuki kwa kushughulika na watu binafsi wenye migongano na serikali.

Pia, tuangalie kwamba masuala ya kisiasa yashughulikiwe au yajibiwe kisiasa kwenye majukwaa, ili vyombo vya dola vibaki na kazi yake ya msingi ya kulinda amani, usalama na sheria. Jambo hili liende sambamba na maridhiano kati ya hao watu binafsi au influencers, ili kuweza kujenga umoja wa kitaifa kwa njia ya kitaasisi.

Tujadili.
Kiongozi mkuu ndio taasisi
 
Back
Top Bottom