Mwana kondoo 2025
JF-Expert Member
- Apr 6, 2025
- 495
- 580
Chama ni mali ya umma. Ndio maana kinatumia rasilimali na ruzuku za umma.Mimi nimetafakari na kujiuliza je tatizo la chadema ni chama na sera zake au pengine ni Uwepo wa Tundu Lissu kwenye chama hicho na misimamo yake. Hili linahitaji mjadala mpana sana kwa sababu Chadema ni Taasisi inayoishi Lisu atakuwemo na kutoka pengine ataenda DP au ataacha siasa au kufariki nk. chadema kwa hali ya kawaida itakuwepo. Chama ni mali ya wananchi kama mimi ndiyo maana kwenye usajiri wake lazima kithibitishe kuungwa mkono Tanzania bara Tanganyika na Zanzibar. Ndiyo sifs kuu ya kukubaliwa usajiri. Kama ndivyo kwa kuifuta chadema haitasidia wanachama na wananchi kwa ujumla wake. Naamini leo kikifutwa wanachama watahamia kule Lissu atakohamia labda DP au UDP hivyo kama tatizo lilikuwa ni Lisu chadema kitaadhibiwa bure misili ya suala la Gwajima kwenye kanisa la ufufuko na uzima kwa wafuasi wake. Hii ni hatari kuliko kumshughulikia mtu. Yaani from instituonal /systems approach to individual approach. Hii itasaidia kuepukana na wananchi walio na tegemeo kwa taasisi husika kuadhibiwa na kujenga chuki kwa serikali yao. Tubane wigo wa chuki kwa kushughulika na watu binafsi wenye migongano na serikali. Pia tuangalie masuala ya kisiasa yashughulikiwe/ yajibiwe kisiasa kwenye majukwaa ili kuviacha vyombo vya dola kushughulika na majukumu ya ya kimsingi. Tujadili.
Huu ni upuuzi kama sheria hii ipo, kuna ulazima upi chama kinacho fanya siasa zake kwa asilimia 95 Tanganyika iwe lazima kikubalike Zanzibar??? Watu ambao hata ki utamaduni tupo tofauti??Chama ni mali ya wananchi kama mimi, ndiyo maana kwenye usajili wake lazima kithibitishe kuungwa mkono Tanzania Bara (Tanganyika) na Zanzibar.
Tujadili.
Subirini mabadiliko yapo njiani.Huu ni upuuzi kama sheria hii ipo, kuna ulazima upi chama kinacho fanya siasa zake kwa asilimia 95 Tanganyika iwe lazima kikubalike Zanzibar??? Watu ambao hata ki utamaduni tupo tofauti??
Wao ccm na wapuuzi wachache wa huko visiwani, kwa matakwa yao waliamua kuunganisha vyama vyao, kisha wakaitoa sadaka Tanganyika kwa wake zao ikaishia hapo.
Sasa iweje leo, mimi nina harakati zangu, nina pambania ndugu zangu wa damu, unakuja unasema eti ooh!!! Ili tupambane nilazima ukaowe nilipooa mimi.
sisi tunawajua hiyo familia uliyooa wewe ni wapuuzi na wajivuni, hatuwezi kuoa nyumba hiyo, wewe ulihonga shamba la familia(Tanganyika) inaatosha.
Chadema hakihitaji kuwa na kiongozi kutoka Zanzibar ili kuwa chama, na sio kiongozi tu, hakihitaji hata kuwa mwanachama kawaida kabisaaaa yule wa ngazi ya chini, achana na mwanachama, chadema hakihitaji nata kuwa na shabiki Zanzibar ili kuwa chama.
Waacheni hao wapuuzi wahangaike wao na wake zao, wakijua wenyewe watachaguanaje, sisi watanganyika tunahitaji chama kinacho jiendesha Tanganyika peke yake
Si mnaona wanatusaliti hawa, leo wamejaribu wamekipiga nyundo mahakamani chama, hakitakiwi kufanya chochote, hakuna mikutano, hakuna michango hakuna nini, leo wakifanikisha watatumia sheria hiyo kutukwamisha kila siku.
Hili tulipiganie Watanganyika woote bila kujali chama.
Tanu na asp waliungana wao, kisha tanu, chini ya Nyerere wakahonga shamba la familia(Tanganyika yetu nzuri ya kupendeza) inatosha hapo. Kuhusu kuchaguana bungeni watajuana wao, sisi tunaweza kuwapa nafasi moja tu ya huruma bungeni, wanakua na mtu mmoja tu anakua anaiwakilisha Zanzibaryoote kwenye bunge letu tena inabidi asiwe na sauti yoyote, ule muda wa kupiga stori bungeni ndio yeye anawashiwa mic atuchekeshe kidogo.
sijuagi hata chama cha huko Zanzibar kilichoungana na tanu kinaitwaje, kuna wakati naendaga kukojoa baharini nikiamini wazanzibary wanapoogelea folozani watakua wanakunywa mikojo yangu)
Mimi nilipokuwa secondary, katika mtihani, maswali yoote yanayohusu Zanzibar nilikua siyajibu, yaani hata walete swali za Zanzibar kwenye maths, mie naliacha sijibu.
Hawa sio ndugu zetu.
NB.
Na nyie ma mods hapo jf, msijaribu kufanya chochote kwenye komenti yangu.
Kiongozi mkuu ndio taasisiMimi nimetafakari na kujiuliza, je, tatizo la CHADEMA ni chama na sera zake au pengine ni uwepo wa Tundu Lissu kwenye chama hicho na misimamo yake?
Hili linahitaji mjadala mpana sana kwa sababu CHADEMA ni taasisi inayoishi—Lissu atakuwemo na kutoka; pengine ataenda DP, au ataacha siasa, au hata kufariki. Lakini CHADEMA, kwa hali ya kawaida, itaendelea kuwepo.
Chama ni mali ya wananchi kama mimi, ndiyo maana kwenye usajili wake lazima kithibitishe kuungwa mkono Tanzania Bara (Tanganyika) na Zanzibar.
Hii ndiyo sifa kuu ya kukubaliwa kwa usajili kamili. Kama ndivyo, basi kuifuta CHADEMA hakutasaidia wanachama na wananchi kwa ujumla wake.
Naamini kwamba leo kikifutwa, baadhi ya wanachama watahamia kule Lissu atakakohamia—labda DP au UDP. Hivyo, kama tatizo lilikuwa ni Lissu, basi CHADEMA kitakuwa kimeadhibiwa bure.
Mfano wa karibu ni suala la Gwajima kwenye Kanisa la Ufufuo na Uzima kwa wafuasi wake.
Hii njia ya kufuatilia mtu mmoja badala ya taasisi ni hatari na si nzuri. Ni kama kutoka katika mfumo wa kushughulikia taasisi (institutional/systems approach) hadi mfumo wa mtu binafsi (individualistic approach).
Ni muhimu tushughulikie watu binafsi wenye matatizo binafsi na serikali, tukiacha taasisi ziendelee na kazi zake kwa mujibu wa sheria.
Hatua hii itasaidia kuepuka kuwaadhibu wananchi walio na matumaini na taasisi husika, na pia kuepuka kuchochea chuki dhidi ya serikali yao.
Tubane wigo wa chuki kwa kushughulika na watu binafsi wenye migongano na serikali.
Pia, tuangalie kwamba masuala ya kisiasa yashughulikiwe au yajibiwe kisiasa kwenye majukwaa, ili vyombo vya dola vibaki na kazi yake ya msingi ya kulinda amani, usalama na sheria. Jambo hili liende sambamba na maridhiano kati ya hao watu binafsi au influencers, ili kuweza kujenga umoja wa kitaifa kwa njia ya kitaasisi.
Tujadili.