Carlos The Jackal
JF-Expert Member
- Feb 6, 2017
- 25,725
- 78,589
MmhKutokukubalika Kwa Wagombea Hawa, hasa katika kizazi hiki Cha Gen Z , kizazi Cha wasomi , wenye kuishi mjini, kizazi chenye kuaminika Amani inaletwa na Chama chochote, Kizazi chenye ushindi dhidi ya wanaoishi kijijin wale wanaoamin Amani ni CCM tu.
Hivi Kwa hiki kizazi , Dola haitatumia nguvu kupitiliza kuhakikisha kwamba wasokubalika wanapita?.
Mkapa 1995 alikubalika, Kikwete 2005 alikubalika, JPM 2015 alikubalika hali ilofanya Dola kua na mtumizi kiduchu ya nguvu.
Huyu wa Sasa, ambaye hata kabla ya uchaguzi tu watu wanatakiwa, wanapotea, Vifo, Sasa kwenye Uchaguzi itakuaje?.
Mfano nani hauziki ?Kama Uchaguzi ni mbele huko, lakini tumeona na kusikia habari za utekaji, Upoteaji , Mauaji , matukio yanayoashiria kukosekana Kwa ustahimilivu na uvumilivu wa Kisiasa.
Vipi miezi Kadhaa kuelekea uchaguzi ? Wakati ambao CDM mpya inarudi kua Ile ya 2010, sio kwamba Dola imeburuzwa na kuingia kwenye mtego wa baadae kutumia nguvu kubwa kupitiliza ??.
Kuna wakati, CCM mnatakiwa kuchagua watu ambao tayari wenyewe wanakubalika na Raia, ili iwe nafuu kuwatetea na kupunguza matumizi makubwa ya nguvu.
MTU asouzika Wala kukubalika na akataman aendelee kubaki Madarakani, Huwa ni wa Hatari sana ,yupo radhi kumwaga damu za wale wanaowaona ni kikwazo .