nakushukuru sana mzee anagalau wewe umeona kitu.... najua ukipenda sana hata chongo utaona kengeza, ni makosa makubwa sana kuruhusu vidosari vidogovidogo hata kama hakuna pingamizi ndani ya chama, lakini vinaweza kutumiwa na wapinzani wa chadema kwenye kampeni, kumbuka chama hiki kinazongwa na uzushi wa aina nyingi kama ukabila, sasa udini na tena mnataka kuongeza udikteta wa kamatikuu!!
jamani siasa zina mbinu nyingi..... bado sijaridhika na majibu, ina maana pamoja na chadema kushabikiwa sana hapa jamvini, hakuna mtu anayejua utaratibu wa kumteua mgombea uais ndani ya chama unasemaje? ni ajabu na kweli!!
bado nasubiri anayejua utaratibu ukoje anisaidie....