...........acha hizo ndugu yangu...............kuuliza si ujinga...............jibuni maswali basic.........itasaidia sana.....kuonyesha kuwa Chadema mko makini...............sitaki kukumbuka wakati ule wa uchaguzi ambapo Zitto alitaka kugombea Uenyekiti......na ile mizengwe ya uchaguzi wa Vijana.........tuwe responsible............tusikwepe maswali........wauliza maswali ndio wapiga kura wenyewe ........au?
asante kwa link...kwa wale amabo watashindwa kufungua hiyo link maelezo nikama ifuatavyo
RATIBA NA MAANDALIZI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2010
TUKIO TAREHE
1 Kuchukua na kurudisha fomu za kugombea Udiwani, Ubunge na Uwakilishi Mei 3 mpaka Agosti 9
2 Kura za Maoni kwa wagombea nafasi za Udiwani, Uwakilishi, Ubunge na Urais Juni 1 mpaka Agosti 1
3 Uteuzi wa Awali wa wagombea Udiwani (Kamati Tendaji za Kata) Julai 1 mpaka Agosti 1
4 Uteuzi wa Awali wa wagombea Ubunge na Uwakilishi (Kamati Tendaji za Majimbo) Agosti 2 mpaka Agosti 9
5 Uteuzi wa Awali wa wagombea Ubunge wa Viti Maalum (Halmashauri Kuu ya Baraza la Wanawake wa CHADEMA - BAWACHA) Agosti 8
6 Kuthibitisha Uteuzi wa wagombea Ubunge na Uwakilishi (Kamati Kuu) Agosti 10
7
Kupendekeza wagombea Urais na Makamu wa Rais wa Muungano na Rais wa Zanzibar (Baraza Kuu la Chama) Agosti 11
8 Uteuzi wa wagombea Urais na Makamu wa Rais wa Muungano na Rais wa Zanzibar na kuthibitisha Ilani ya Chama (Mkutano Mkuu) Agosti 12
Angalizo
- Tarehe za uchukuaji fomu kwa nafasi ya Urais zitatangazwa katika hatua ya baadaye.
- Kwa mujibu wa azimio la Mkutanao Mkuu wa chama 2005, Kamati Kuu ilipitisha mfumo wa kura za maoni (primaries) kabla ya vikao vya uteuzi wa awali na kuthibitisha uteuzi kufanyika kwa mujibu wa katiba. Kura za maoni za udiwani zitafanyika kwenye ngazi ya Tawi, za Ubunge kwenye eneo la Tarafa na za Urais kwenye ngazi ya Majimbo (Kanda). Maelekezo kuhusu namna kura husika zitakavyofanyika pamoja na wajumbe wataoshiriki yatatolewa kwa ngazi husika za chama.
- Majimbo yamepewa fursa ya kuandaa ratiba za maeneo husika kwa idhini ya Sekretariati kwa kuzingatia mipaka iliyotolewa.
- Kamati Kuu iliyofanya kikao chake tarehe 26, Aprili 2010 imeridhia ushirikiano wa kimkakati na vyama vingine vya upinzani na kuruhusu ushirikiano wa ngazi ya chini kama utakavyoainishwa na vikao vya juu vya chama. Pale ambapo pataonekana panafaa.
Makadirio ya Bajeti ya Uchaguzi Mkuu 2010
CHADEMA inakadiria kwamba kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 itatumia kiasi
kisichozidi bilioni tano; kiwango ambacho kitahusisha kampeni zote za chama kwa ujumla wake kuanzia kwenye udiwani, ubunge na urais kwa matumizi yote ya uteuzi ndani ya chama pamoja na kampeni zenyewe.
Hata hivyo, Chama hakina kiasi hicho cha fedha na mikakati inaendelea kuandaliwa na kutekelezwa kwa ajili ya kukusanya fedha kwa wanachama na wapenzi.