Hivi elimu na shule za Tanzania zimekumbwa na nini?

leoleo-tu

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2018
Posts
2,224
Reaction score
6,784
Kuna rafiki yangu ana mtoto anasoma shule moja ya private yuko kidato cha tatu. Shule yenyewe ni boarding hivyo mtoto ameanza kusoma pale toka kidato cha kwanza na sasa yuko kidato cha tatu.

Sasa jambo la kushangaza ni kwamba walimwita mzazi katika likizo hii na kumwambia kuwa mtoto wake siku hizi hafanyi vizuri shule. Likizo hii apambane naye na matokeo yake yakiendelea kuwa mabaya mtihani wa mwezi wa tisa basi watamwambia amtaftie shule nyingine wao hawataki kubeba watoto watakaofanya vibaya kidato cha nne.

Sasa mimi aliponieleza nikabaki najiuliza maswali kadhaa:

1. Kazi ya shule ni nini kama si kumfundisha mtoto ili apate kufaulu na kufanya vizuri ukizingatia yule mtoto anasoma boarding wako naye muda wote. Sasa kama mzazi angekuwa na uwezo wa kumfanya mtoto afaulu kwanini alipe mamilioni shuleni si angembakiza nyumbani amfunze mwenyewe ili afaulu.​
2. Walau ingekuwa yule mtoto alihamia shule hiyo lakini ameanza hapo kidato cha kwanza. Hivyo wanachokiona sasa ni matokeo ya ufundishaji wao sasa badala ya kutafuta shida wao wanataka kumtupia mzazi.​

Jambo hili ninaliona katika shule nyingi za private. Mtoto akiwa hana ufaulu mzuri basi wanamwambia mzazi amhamishe au wengine wanaenda mbali zaidi kumfanyisha mtihani wa kitaifa kwenye vituo vya mitihani si kwa namba ya shule husika.

Kugeuza elimu kuwa biashara 100% ambapo mashule yanashindana kwenye matokeo kuwa na DIV 1 tu kunaleta haya yote.

Mimi nadhani shule nzuri ni ile ambayo inaweza kumpokea mtoto ambaye alikuwa hayuko vizuri kimasomo na kumgeuza awe vizuri kimasomo.
Jamaa yuko anapambana na kumpeleka mtoto tuition ili aweze kufanya vizuri.
 
Maana yake,hao walimu wamekiri pasina shaka kwamba hawana jipya ku-offer kwa mtoto/mwanafunzi ili aenende na wenzake.Hawaiwezi hiyo kazi.Wameomba wasaidiwe na wenye kuweza.
NB;Mmechunguza na uwezo wa mtoto "wenu" ku-grasp maelekezo na mafundisho ya walimu wake?Isijekuwa mtoto ndiye changamoto kuu.
 
Maana yake,hao walimu wamekiri pasina shaka kwamba hawana jipya ku-offer kwa mtoto/mwanafunzi ili aenende na wenzake.Hawaniwezi.Wameomba wasaidiwe na wenye kuweza.
NB;Mmechunguza na uwezo wa mtoto "wenu" ku-grasp maelekezo na mafundisho ya walimu wake?Isijekuwa mtoto ndiye changamoto kuu.
Sina hakika juu ya uwezo wake ila kama alifaulu la saba government, akapelekwa hapo private akapewa interview ili ajiunge form 1 akafaulu, akasoma kidato cha pili akafaulu, sasa iweje sasa hivi ndipo waone kuwa kawashinda? Ndio maana nasema angekuwa kahamia hapo labda ingemake sense kidogo ila anasoma hapo toka kidato cha kwanza.
 
Kuna rafiki yangu ana mtoto anasoma shule moja ya private yuko kidato cha tatu. Shule yenyewe ni boarding hivyo mtoto ameanza kusoma pale toka kidato cha kwanza na sasa yuko kidato cha tatu.
Sasa jambo la kushangaza ni kwamba walimwita mzazi katika likizo hii na kumwambia kuwa mtoto wake siku hizi hafanyi vizuri shule. Likizo hii apambane naye na matokeo yake yakiendelea kuwa mabaya mtihani wa mwezi wa tisa basi watamwambia amtaftie shule nyingine wao hawataki kubeba watoto watakaofanya vibaya kidato cha nne.
Sasa mimi aliponieleza nikabaki najiuliza maswali kadhaa:
1. Kazi ya shule ni nini kama si kumfundisha mtoto ili apate kufaulu na kufanya vizuri ukizingatia yule mtoto anasoma boarding wako naye muda wote. Sasa kama mzazi angekuwa na uwezo wa kumfanya mtoto afaulu kwanini alipe mamilioni shuleni si angembakiza nyumbani amfunze mwenyewe ili afaulu.
2. Walau ingekuwa yule mtoto alihamia shule hiyo lakini ameanza hapo kidato cha kwanza. Hivyo wanachokiona sasa ni matokeo ya ufundishaji wao sasa badala ya kutafuta shida wao wanataka kumtupia mzazi.

Jambo hili ninaliona katika shule nyingi za private. Mtoto akiwa hana ufaulu mzuri basi wanamwambia mzazi amhamishe au wengine wanaenda mbali zaidi kumfanyisha mtihani wa kitaifa kwenye vituo vya mitihani si kwa namba ya shule husika.
Kugeuza elimu kuwa biashara 100% ambapo mashule yanashindana kwenye matokeo kuwa na DIV 1 tu kunaleta haya yote.
Mimi nadhani shule nzuri ni ile ambayo inaweza kumpokea mtoto ambaye alikuwa hayuko vizuri kimasomo na kumgeuza awe vizuri kimasomo.
Jamaa yuko anapambana na kumpeleka mtoto tuition ili aweze kufanya vizuri.
Tatizo wazazi tunakalili kuwa kila mtoto ili afanikiwe lazima afanye vizuri darasani! Sio kweli! Akishapata maarifa ya kujitambua yeye ni nani na kujua mazingira yanayomzunguka na kujua kusoma na kuandika baasi! Tafuta kipaji alichonacho au mfungulie biashara! Elimu ya darasani inahitaji kichwa kinachoshika na kuyatoa/kuyaandika katika karatasi au kwa mdomo (kujibu mtihani) vinginevyo unampotezea muda mtoto na wewe unapoteza rasilimali fedha!
 
Nakubaliana na wewe ila mtoto kusoma hadi walau form 4 ni jambo la msingi na si kila mtoto ana akili ya kuendelea hadi chuo kikuu nakubaliana na wewe.
 
Sina hakika juu ya uwezo wake ila kama alifaulu la saba government, akapelekwa hapo private akapewa interview ili ajiunge form 1 akafaulu, akasoma kidato cha pili akafaulu, sasa iweje sasa hivi ndipo waone kuwa kawashinda? Ndio maana nasema angekuwa kahamia hapo labda ingemake sense kidogo ila anasoma hapo toka kidato cha kwanza.
..."sina uhakika"...!Muutafute uhakika mapema kabla hajakataliwa "mbinguni" na "duniani"!Msichoke,wewe na "rafiki " yako.
 
Wamekula ada miaka mitatu yote kwann wasingemuondoa mapema hawa Private wamekuwa matapeli sana na kwenye vyuo ni hivyo hivyo yanadanganya watoto wa watu rudia mtihani utafaulu kila mwaka matokeo yake mtu anasoma diploma ya Pharmacy miaka mitano mpaka anakimbia mwenyewe bila hata cheti wapuuzi sana.
 
Mkuu sio mwanangu mimi mwanangu wa kwanza ndo kwanza yuko la nne. Ila alinishirikisha wakati akinieleza yanayomsibu ndipo nikashangaa jambo hilo. Sema mtoto mwenyewe namfahamu ila performance yake kwa kuona matokeo sijawahi zaidi ya kujua alifaulu la saba, akaenda hapo na sasa yuko kidato cha tatu bila shaka alifaulu form 2 pia.
 
Hilo laweza kuwa moja.Lakini,mtoto anakua kiumri,mwili na akili positively au negatively. Anapitia mabadiliko mbalimbali jumlisha kipindi cha balehe.Ni vema kwenda na mtoto wa aina hiyo kwa tahadhari na umakini mkubwa.Akili zinawezakuwa zimechangamka kupitiliza au zimedorola ajabu!Mabadiliko ya ukuaji huja na changamoto za kila aina.
 
Kitendo cha kushirikishwa tu,amekuwa mtoto wenu.Ndiyo maana umeguswa na kuanzisha mjadala.Kuwa sehemu ya msaada hata wa mawazo tu.
 
Kwa kweli sijui lina ukweli kiasi gani hili jambo. Ila najaribu kutafakari pasi na sababu tu uongozi wa shule wakuambie maneno kama hayo hata bila kujiuliza shida ni nini?!

Maana kama ni shule unayolipa milions of money sidhani kama wanaweza kufanya vitu kienyeji hivi.

Poleni.
 
Mkuu we shule za private huzijui. Siku hizi hazitaki kufailisha kama mtoto hafanyi poa kukurudishia au kukwambia umwamishe ni dakika 0. Nyingine zinakupa option ya kwamba ataendelea kusoma hapo ila watamhamisha kituo cha mtihani. It is all about business, matokeo yakitoka wasionekane wana mtoto ambaye akfail.
 
Hawawez nifanyia ujinga huo mimi. Yan jasho lingewatoka.
Mmekula pesa yangu miaka mi 3 na mnaona mtoto haend sawa mmekaa kimya ila mwisho wa siku jumba bovu mniangushie mimi?? Alooo, mrudishe oesa zangu za miaka yote niondoke na mtoto au mkomae na mtoto mpaka afaulu. Ndio options ninazowapa hao.

Mwambie huyo rafiki yake asilete unyonge.
Kwanza huko ni kum harras mtoto
 
Kwa kweli sijui lina ukweli kiasi gani hili jambo. Ila najaribu kutafakari pasi na sababu tu uongozi wa shule wakuambie maneno kama hayo hata bila kujiuliza shida ni nini?!

Maana kama ni shule unayolipa milions of money sidhani kama wanaweza kufanya vitu kienyeji hivi.

Poleni.
Ndiyo kwa kujiuliza;-
-ni mtoto huyo peke yake ana changamoto hapo darasani kwao?
-imeanza hivi karibuni au toka zamani?Mzazi alishirikishwa?
-juhudi gani zilioneshwa kutoka kwa wazazi na walimu kumkwamua?
-kuna changamoto nyingine kutoka kwa mtoto zaidi ya hiyo ya kitaaluma?
-imewahi kuwatokea watoto/wanafunzi wengine hapo shuleni?
-zilichukuliwa hatua kama hizo zinazotaka kuchukuliwa sasa?
 
Kuna watu wana akili ya taratibu nadhani huyo mtoto ni mmojawapo achunguze fani apendayo amkazanie hapo atafanya makubwa ashangae, mfano mzuri ni wacheza mpira wengi darasani ni akili nzito
 
Mkuu we shule za private huzijui. Siku hizi hazitaki kufailisha kama mtoto hafanyi poa kukurudishia au kukwambia umwamishe ni dakika 0. Nyingine zinakupa option ya kwamba ataendelea kusoma hapo ila watamhamisha kituo cha mtihani. It is all about business, matokeo yakitoka wasionekane wana mtoto ambaye akfail.
Mkuu Leo,

Mimi namsomesha mwanangu private, nakumbuka mara ya mwisho kwenda kwenye kikao na mama yake ikaonyesha mtoto matokeo ya nyuma alifanya vibaya lakini ya mbele yake alifanya vzuri.

Ilipofika wakati wa maswali kuna mzazi ali-notice hicho kitu akauliza. Sababu kubwa walituambia kwamba mtaala umebadilika na mtoto anahitaji kusoma vitu vingi katika ndani ya somo moja.

Na hata zana za kufundishia baadhi ya shule walikuwa hawana na mtihani utatungwa kulingana na mtaala huo.
Hapo sasa watoto wanapitia kipindi cha Translation(mpito) katika kipindi kama hicho si watoto wote wanafanana kiuwezo, kuna wale ambao watashuka kiuwezo kuna wale watakaoendelea sababu ya uwezo kutofautiana.

Walimu walitupa sababu nyingi sana ambazo kama wazazi tulizikubali na wakashauri ni kwa namna gani ya kurudisha uwezo wao na masuala ya saikolojia nzima ya mtoto.

Ndio maana nimeshangaa kwa hiyo shule kufanya mambo kienyeji kiasi hicho, huku mzazi akiumia kulipa milioni za pesa.

Binafsi siwezi kulizungumzia hili sababu mesoma huko, na sasa namsomesha mwanangu huko na hata kwenye kamati za shule huwa tunaitwa sana wadau na kusikilizwa kwa namna gani ya kuboresha zaidi.

Siwezi kulizungumzia hili na limenishangaza kiasi chake binafsi.
 
Ndiyo kwa kujiuliza;-
-ni mtoto huyo peke yake ana changamoto hapo darasani kwao?
-imeanza hivi karibuni au toka zamani?Mzazi alishirikishwa?
-juhudi gani zilioneshwa kutoka kwa wazazi na walimu kumkwamua?
-kuna changamoto nyingine kutoka kwa mtoto zaidi ya hiyo ya kitaaluma?
-imewahi kuwatokea watoto/wanafunzi wengine hapo shuleni?
-zilichukuliwa hatua kama hizo zinazotaka kuchukuliwa sasa?
Mkuu Moise,

haya ni maswali muhimu sana uliyoyaandika hapa. Labda kama kuna watu wameelewa mtoa mada vzuri anachosema.

Mimi binafsi sijaelewa, kuna muda kama wazazi huwa tunahitimisha kulaumu shule bila ya sisi wenyewe kujifanyia tathmini kwanza.

Na kwa shule makini lazima maongezi kati ya mzazi na mwalimu yangehusisha haya maswali muhimu.

AhsaNte sana.
 
Shule za private zina upumbavu mwingi sana. Naomba niishie hapa.
Watasema hatuna hela labda tunajitetea. Kwanza siamini Kama kupata elimu ni mpaka uwe na hela Bali mie naamini ni kuwa na njaa Kali mno yaani unatengeneza vacuum in your heart to seek a certain knowledge ambayo ipo available everywhere at internet etc.

Nimepitia government schools nimekomaa kiasi kikubwa ni uwezo wangu yaani nikapata wani Kali o&a na wanangu wanasoma government.

Labda Hawa private wangekuwa Wana uhakika wa kutoa ajira kwa wahitimu.

Nimekutana na hao walisoma English medium mpaka somo la English nawaburuza Kuna mmoja alisomea Uganda full English aka disco pale CoET udsm second year
 
Hilo laweza kuwa moja.Lakini,mtoto anakua kiumri,mwili na akili positively au negatively. Anapitia mabadiliko mbalimbali jumlisha kipindi cha balehe.Ni vema kwenda na mtoto wa aina hiyo kwa tahadhari na umakini mkubwa.Akili zinawezakuwa zimechangamka kupitiliza au zimedorola ajabu!Mabadiliko ya ukuaji huja na changamoto za kila aina.
Well said
 
Back
Top Bottom