Hivi elimu na shule za Tanzania zimekumbwa na nini?

Hivi elimu na shule za Tanzania zimekumbwa na nini?

Tatizo wazazi tunakalili kuwa kila mtoto ili afanikiwe lazima afanye vizuri darasani! Sio kweli! Akishapata maarifa ya kujitambua yeye ni nani na kujua mazingira yanayomzunguka na kujua kusoma na kuandika baasi! Tafuta kipaji alichonacho au mfungulie biashara! Elimu ya darasani inahitaji kichwa kinachoshika na kuyatoa/kuyaandika katika karatasi au kwa mdomo (kujibu mtihani) vinginevyo unampotezea muda mtoto na wewe unapoteza rasilimali fedha!
Uneta habari za kina Bill gates bongo?

Peleka mtoto shule acha ujuaji
 
Maa
Kuna rafiki yangu ana mtoto anasoma shule moja ya private yuko kidato cha tatu. Shule yenyewe ni boarding hivyo mtoto ameanza kusoma pale toka kidato cha kwanza na sasa yuko kidato cha tatu.

Sasa jambo la kushangaza ni kwamba walimwita mzazi katika likizo hii na kumwambia kuwa mtoto wake siku hizi hafanyi vizuri shule. Likizo hii apambane naye na matokeo yake yakiendelea kuwa mabaya mtihani wa mwezi wa tisa basi watamwambia amtaftie shule nyingine wao hawataki kubeba watoto watakaofanya vibaya kidato cha nne.

Sasa mimi aliponieleza nikabaki najiuliza maswali kadhaa:

1. Kazi ya shule ni nini kama si kumfundisha mtoto ili apate kufaulu na kufanya vizuri ukizingatia yule mtoto anasoma boarding wako naye muda wote. Sasa kama mzazi angekuwa na uwezo wa kumfanya mtoto afaulu kwanini alipe mamilioni shuleni si angembakiza nyumbani amfunze mwenyewe ili afaulu.​
2. Walau ingekuwa yule mtoto alihamia shule hiyo lakini ameanza hapo kidato cha kwanza. Hivyo wanachokiona sasa ni matokeo ya ufundishaji wao sasa badala ya kutafuta shida wao wanataka kumtupia mzazi.​

Jambo hili ninaliona katika shule nyingi za private. Mtoto akiwa hana ufaulu mzuri basi wanamwambia mzazi amhamishe au wengine wanaenda mbali zaidi kumfanyisha mtihani wa kitaifa kwenye vituo vya mitihani si kwa namba ya shule husika.

Kugeuza elimu kuwa biashara 100% ambapo mashule yanashindana kwenye matokeo kuwa na DIV 1 tu kunaleta haya yote.

Mimi nadhani shule nzuri ni ile ambayo inaweza kumpokea mtoto ambaye alikuwa hayuko vizuri kimasomo na kumgeuza awe vizuri kimasomo.
Jamaa yuko anapambana na kumpeleka mtoto tuition ili aweze kufanya vizuri.
na ya kuwa private school ni nini hasa kama hawawezi kujitofautishia majukumu yao sawa na shule za jumuiya?
 
Shule za private zina upumbavu mwingi sana. Naomba niishie hapa.
Na ndiyo maana kuna government, peleka mtoto wako Yusuph Makamba,kule hakuna mambo ya ajabu yaliyopo private.
Wew unakuta toto haliandiki notes
Halimalizi maswali kwenye mtihani
Linasumbuq shule nzima
Halafulinafeli.
Unataka tuliue muanze kutukana walimu mtandaoni? Hamisha mzigo huo ili shule ipate wateja wengine.
 
Back
Top Bottom