Salam wakuu. Hakika nimepata mgagasiko WA nafsi na roho katika hili. Dada zetu na mama zetu mmekua mkitumia miili yenu kama sehemu ya ahsante pale mnapo tendewa jambo Fulani jema au haya kusaidiwa matatizo madogomadogo. Nayazungumza haya kwa uchungu kwa hili lililo nikuta mei mosi ya leo. Kuna ndugu ninafanya nae kazi alikua na tatizo kubwa katika ndoa yake kiasi alikua hana raha kabisa na akaniomba msaa da wa kusuluhisha mgogoro wao, nilikubali na kwa kuanza ilibidi aniunganishe na bibie ambaye ndio mwenza wake nami nikazungumza nae kwa kina nisiwachoshe sana nilifanikiwa kusuluhisha mgogoro na kuwafanya warudiane.Jana asubuhi bi dada akanipigia cm na kuniomba tuonane baada ya mid a ya kazi mi muhimu nikamuuliza kwema akasema mi kwema.Kwakua jamaa hayupo wiki sasa nikamtaarifu kuwa bibie kanambia nionane nae akasema poa. Baada ya kazi nikampigia akanambia niende kwake sikuona tatizo ni mitaa kadhaa kutoka kwangu.Baada ya stori mbili tatu bibie akaanza kulia sana kiasi nilipatwa na mshangao na bumbuwazi nini NASA chanzo cha kilio kile, nikajaribu kimbembeleza mpaka ikabidi no mkumbatie na kumbembeleza zaidi.Hakika sijui ilikuwaje mpaka sasa siamini nilicho kifànya na jamaa kanitext this morning anauliza niliitiwa kitu gani? Hivi Hanna ahsante nyingine zaidi ya mwili maana kwa Maelezo yake nikua amenipa ahsante kwa kuwafanya wawe pamoja. Wasalam!