Fantasia
JF-Expert Member
- Nov 19, 2017
- 1,071
- 832
Dhana ya Mungu ilikuweko tangu enzi na enzi, dhana hii ilijitokeza kukidhi mahitaji ya watu husika kutokana na mazingira na asili zao, wakati huo kabla ya Talmudi, biblia, Wala Qurani kuweko, ni staarabu kongwe Za Africa, Uajemi, Mesopotamia, Uchina na kusini mwa bara la America ndio dhana ya uungu, dini na imani zilikoshamiri, kukiwa na itikadi Za miungu wengi na Mungu mkuu wa Miungu, Ambayo hatimaye ikaazalisha dhana ya Mungu mmoja Ama ATEN kwa mara ya Kwanza kunako Misri ya kale hapa hapa bara la Africa katika utawala wa Farao Akhenaten. Hii namna ya Mungu mmoja, wa kiyahudi, kikiristo na wa Kiislamu ni tengenezo changa tu la karibuni, Ambalo agenda yake kimsingi ilikuwa ya kisiasa na utawala, na hivyo kwa mara ya kwanza kabisa na awali ustaarabu wa binadamu chini yake ukashuhudia majanga mkubwa ya ubaguzi wa rangi, utumwa, dhuluma ya kiuchumi na vita kote duniani..
*ikumbukwe pia wakati huo wakazi na wenyeji wa maeneo yote hayo walikuwa watu weusi, Bara la Africa likiwa limeungana na bara Asia, weusi walifika hadi uchina na kupandikiza staarabu Za awali huko, angalia wajenzi wa majengo ya kale wote walikuwa wa asili na mbari ileile. hadi Stonehenge, hadi Gautama Buddha alikuwa mtu mweusi. Fumbo la dunia liko hapo, mweusi amenyimwa nyumba ya ibada yake kwa makusudi, kwani wanajua akirejea ibada asilia hekaluni mwetu, dunia tutairudisha katika utaratibu asilia na sheria takatifu Za miungu.
ndugu msomaji, je una mchango gani, kukabiliana na hali hiii
Asanteni, na karibuni