Hivi hakuna kabisa uwezekano wa kuzungumza kuhusu Mungu nje ya msamiati wa kiyahudi?

Hivi hakuna kabisa uwezekano wa kuzungumza kuhusu Mungu nje ya msamiati wa kiyahudi?

Hiyo miungu yenu mabitozi wanaogopa hata kuku, wataanzaje kunipa kwa laana?
Sasa ninailaani hiyo miungu yenu, na madhabahu zake, na makuhani wake, na sadaka zote mlizozitoa, na ninayavunja na maashera yenu, na vyote nilivyokuwa chini ya miungu hiyo vimelaaniwa
unadhania haya ni masihara, kuna wenzio walikufa huku wamesimama, kutukana vitu wasivyovijua, endelea tu
 
Hapa na mimi napingana na wewe

Hakuna dhana Bora Duniani ielezayo habari za uungu kwa ubora wake kama ya kiyahudi

Katika kusoma kwangu vitabu napenda sana Mtunzi kitabu awe ni mtu mwenye kukiri madhaifu yake(sijui kitaalamu wanaitaje hii hali)

Iyo ndio sifa pekee inayofanya vitabu vya kiyahudi kuwa Bora na kutegemeka_havipendi kujipa Fagio kirahisi na kwa ushawishi.

Na namna yake ya uandishi inaamsha udadisi na ndio maana vinategemeka kwenye kufundishia_Mataahira yote yawe na utimamu(samahani kwa ukali wa neno_imebidi nilitumie)

Vitabu vyao vina mlango wa kuingilia na kutokea usipoona wa kutokea ujue Bado hujakwiva.

Naomba unipe faida hapo kidogo. Hivi wayahudi wanamuelezea vipi Mungu mpaka wewe ukawaona ni bora katika jambo hilo. Ukinipa na mifano utakuwa umenisadia sana mimi na wale mfano wangu.
 
Naomba unipe faida hapo kidogo. Hivi wayahudi wanamuelezea vipi Mungu mpaka wewe ukawaona ni bora katika jambo hilo. Ukinipa na mifano utakuwa umenisadia sana mimi na wale mfano wangu.
tunasubiria jibu
 
Nyapara wa yahudi,umekuja na humu pia???? Hebu tuacheni bana, sisi tumetumwa kwa wale wa nyumba ya Khemet, nyinyi mlishaukana ubini, damu, na asili zenu, mkawa wayahudi wa uongo, kaeni mbali nasi, tena onyo, bwana Mungu na miungu yetu itakupigeni kwa laana, hakika mkisimama katika njia yetu
Kumbe mmetumwa.... Ndio maana hizi thread za kumkana mungu zimekuwa nyingi. Kwa hiyo na nyinyi mliotumwa mmekuja kumtangaza mungu wenu??
 
Wazo chazo, Ama concept
Je unafikiri maana hiyo ni kamilifu ?

Dhana ni ni tamko litokanalo na kitendo "Dhania" ,kwa maana hiyo dhana ni jina lenye maana ya kutokuwa na uhakika juu ya kile unakizungumza au kufikiria,na mara nyingi humoelekea mtu katika kukosea.

Je kwa maana hiyo huoni unakosea katika matumizi ya hilo neno ?
 
Hapa nakubaliana na wewe kabisa. Mara nyingi watu wanaamini dhana ya Mungu waliyokuzwa nayo, na hawajishughulishi kutafuta ukweli zaidi.
Hivi kaka tutumie nyenzo gani au tupite njia gani ili tuupate huo ukweli ?
 
Kwanza kwa nini tumfate mungu Wa Israel wakati yeye atujui kabisaa Wa Israel awataki ata sikumoja kumsikia mtu mweusi wana tubagua vibaya mno hivi sis Wa Africa mbona atuyaoni wanao tufanyia awa watu. Papa mzungu kwa nini ajawai kuwa Mchina au muafrica.
 
Je unafikiri maana hiyo ni kamilifu ?

Dhana ni ni tamko litokanalo na kitendo "Dhania" ,kwa maana hiyo dhana ni jina lenye maana ya kutokuwa na uhakika juu ya kile unakizungumza au kufikiria,na mara nyingi humoelekea mtu katika kukosea.

Je kwa maana hiyo huoni unakosea katika matumizi ya hilo neno ?
Hapana, dhana ni fununu kuhusu maana, it's relative, but component and integral part of the absolute truth, Ama maana kuu, ingizo katika jumla kuu
 
Kwanza kwa nini tumfate mungu Wa Israel wakati yeye atujui kabisaa Wa Israel awataki ata sikumoja kumsikia mtu mweusi wana tubagua vibaya mno hivi sis Wa Africa mbona atuyaoni wanao tufanyia awa watu. Papa mzungu kwa nini ajawai kuwa Mchina au muafrica.
kila wanachokifannya wameiga
 
Wanadamu baada ya kukosa majibu ya baadhi ya vitu ndipo wakamuumba Mungu vichwani mwao.

Ndio! Wapo wachache wanaoujua ukweli lakini wakadhamiria kabisa kutengeneza Mungu wao wa kufikirika ili waipishanishe jamii ya wengi na ukweli halisi
 
Asante sana
 
Mimi siamini sana katika dini bali naamini katika MUNGU MMOJA TU MWENYE KUAMRISHA UPENDO, HAKI, WAJIBU NA HUKUMU. Ukiamini sana katika dini kunaleta utengano mkubwa sana maana waislam wanaabudu kivyao, wakristo kivyao na wayahudi kivyao lkn hizi dini tatu zina mzizi mmoja wa Ibarahim!!!

Ukiingia kwa wakristo nao wana madheheby chungu nzima, waislam pia sijui kwa wayahudi. Cha ajabu wao kwa wao utashangaa wanakufurishana mara huyu anakufuru mara yule anakufuru ili mradi kila mtu anataka kujitafutia wafuasi licha ya kuwa wote wana mzizi mmoja Ibrahim. Kwa mtu mwenye fikra huru ukisoma vitabu vyote vinavyotumiwa na dini hizo tatu utagundua Mwenyezi MUNGU hakuleta dini yoyote bali alileta mfumo wa maisha kwa ajili ya ustawi wa wanadamu duniani na baada ya mauti yao.
 
Back
Top Bottom