Kaka uko mbali sana na misingi ya kielimu. Kuna namna kadha wa kadha za kutoa ushahidi juu ya hilo ulilolidai,kuna ushahidi wa kiakili na kuna ushahidi wa kimaandiko (Ufunuo,sababu mimi ni muislamu huwa natumia Qur'an,sunnah na kauli za waja wema waliotangulia).
Mathalani kwa mulahiduun (Atheist),hoja za kiufunuo au maandiko matukufu huwa wanazikataa,huwa najaribu kutumia hoja za kiakili,sasa tatizo linakuja katika suala la kutumia akili,wakana mungu huwa wanafikiria kwa muelekeo mmoja daima dawamu na uelekeo huo ni HASI,kufikiri kwa mtindo huu ni kufikiri kitoto sana.Katika hili mifano iko mingi sana.
Watu hawa kwao wao wanaamini hisi na maada,kitu au jambo kama hulioni,hulishiki wala hulihisi kwao halipo na katu hawatokuelewa.
Maandiko kwetu sisi huwa ni thabati (Ukweli mtupu) na huwa ni njia madhubuti ya kuupata ukweli na ndio maana tumesisitizwa sana tutumie akili sana katika kuelewa maandiko kadhalika na kuzingatia.
Natamani hata walimu wao wangewafundisha namna ya kuzitumia akili zao,lakini maskini hata walimu wao hawakujua akili ni nini ? Mahala pa akili ni wapi,na uko wa akili ni wapi ?
Halafu mtu kama huyu anakuja kujitutumua kuhoji ? Laa ! Wallahi hawatoweza.
Nukta ya mwisho kaka nataka nikukumbushe kitu hasa mimi sishindani na mtu sababu najua ni maana ya kujadiliana na katika kujadiliana sio lazima tufike muafaka,muafaka ni matokeo tu wala si lengo. Hii kanuni chukua.