Mkuu punguza ukali wa maneno umemwita punguani mara chizi. Hoja zako zisimame zenyewe zinaeleweka tu. Haina haja ya maneno makali
Sehemu ya maneno makali, maneno makali yanatakiwa.
Mtu anayeniita mimi nisiyeamini uwepo wa Mungu kwamba ni Mkristo, ametumia maneno makali dhidi yangu kwa kunipa kwa kulazimisha imani isiyo yangu kama chizi.
Nikimuita chizi, wala situmii maneno makali, natumia maneno stahili.
Tatizo letu si kwamba tunatumia maneno makali sana.
Tatizo letu hatutumii maneno makali vya kutosha.
Ndiyo maana viongozi wetu wanatukosea, hatutumii maneno makali.
Kutotumia maneno makali sehemu yanapotakiwa ni chanzo cha ujinga na umasikini.
Nakataa kutotumia maneno makali pale yanapostahili.
Nitaendelea kutumia hayo unayoyaita maneno makali pale yanapostahili.
Unaweza kujadiliana nami kama panastahili au hapastahili, lakini usinipangie maneno ya kutumia.
Uhuru wangu wa kujieleza ni kitu muhimu zaidi ya taswira yangu, kama uliniona mtu wa staha sana naomba uondoe hiyo taswira na unione mtu ninayeweza na ninayetaka kutumia maneno makali, pale ninapoona panastahili.
Na sijaona ambapo nimetumia maneno makali bila kustahili. Kila utakapoona maneno makali kutoka kwangu, kuna sababu ya msingi.
Inawezekana niko tofauti kidogo na staha za kwenu, lakini sijawahi kusema kwamba nataka kufuata staha za kwenu.