Hivi hakunaga mipaka eeeh?

Evelyn Salt

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Posts
70,916
Reaction score
141,437
Huyu jamaa ana ndoa, ila pia ana mtoto mmoja aliyempata kabla hajaoa sijui nini kilitokea hadi hakumuoa huyo mama mtoto ila kwa umbea naweza kufatilia teh, mama mtoto alishaendelea na maisha yake akazaa watoto wengine wawili....jamaa anahudumia mwanae ila pia anahudumia hao watoto wengine analipa hadi ada....sio vibaya kusaidia kama kuna uwezo ila kuna haja gani ya kufanya hivo ilhali ana familia yake tayari kwanini yule asibaki tu mzazi mwenzie ahudumie tu mwanae full stop. Mkewe hayupo comfortable na hizo huduma ila pia naona hawezi kuuliza anakufa zake kijerumani tai shingoni.... Ila hata mi sioni sababu ya jamaa kubeba zigo la majukumu kama mme vile sijui nipo sawa au nna roho mbaya lol

Huyu jamaa mwingine ni schoolmate, kaoa muda si mrefu na hapa juzi juzi kapata mtoto, nikampa hongea kwa kuwa baba, akajibu anashukuru ila amekua baba kwa mara ya pili nikaguna Kimoyo moyo nikamuuliza mtoto mwingine,story zikaendelelea.....tukahamia kuwa hali ngumu hela ya manati, akasema hana kitu katoka kumnunulia mzazi mwenzie friji,nkamuuliza wife anajua akasema hapana mmmh nkabaki kutoa macho tu, hivi huo uzazi wenza hauna mipaka ya huduma? Hivi si hadi bra unaeza peleka? Mi naona kwa huduma hizo kifuatacho itv ni hiki



Mtazamo tu pendaneni mwayego......
💃🏻 💃🏻 💃🏻 💃🏻
 
ahaaa....haka ka picha kana maana ipi coz
"imagery" inayopatikana hapa duuu...

 
usipohudumia na wale wengie wasio wako mtoto wako hatapata care unazotaka ukituma ya wako tu yule itabid aigawanye kwa wote wale ambacho wewe hutaki mwanao aishi kwa tabu so inabid kuhudumia wote!!!! hakuna mwanaume ataekubali amchukue mtoto wake aje kwa mkewe weeeeee atateseka si kawaida ndo maana jamaa anaona bora ajikaze tu kuhudumia kule kule kwa sababu yuko kwa mama ake!!!
 
Mmh em ngoja tusikie leo kutoka kwa wababa zaidi. Maana kwa wanawake jinsi tulivyo hilo somo ni gumu sana, tutakimbilia tu kusema " mlete akae hapahapa home" (ili mume apunguze huduma za nje) .Katoto kakifika sasa mwee, ni watoto wachache watakaokuwa salama
 
Wasaidie wengine kila upatapo nafasi
 

Gelofriend kuna thread moja waliulizwa kuhusu kuoa mwanamke mwenye mtoto, walimiminika hao utadhani wamemwagiwa mayai wengi wakidai hawawezi kuhudumia damu ya mwanaume mwingine, ooh hawawezi kuishi na familia ya mtu(mtoto wa mtu) .....bila shaka leo upepo wao utabadilika mioyo yao itakua milaini kama viazi vitamu vilivoungwa na karanga
 
Kumsaidia mwanao tu huku wadogo zake wana shida ni kuwaumiza watoto kisaikolojia
ukisadia saidia watoto wote wanaocheza na mwanao
wakifurahi wote na mwanao atafurahi....
 
Kumsaidia mwanao tu huku wadogo zake wana shida ni kuwaumiza watoto kisaikolojia
ukisadia saidia watoto wote wanaocheza na mwanao
wakifurahi wote na mwanao atafurahi....

Ni zaidi ya kusaidia, kwani si baba yao yupo kwanini ukambebee majukumu yake....
Okay na huko kununua hadi friji ni kumfurahisha mtoto pia? Au friji ya kuhifadhia maziwa ya mtoto Hahaha ncheke mie
 

Yani nilikuwa naedit comment yangu hapa. Ingekuwa ni kuhusu single mother hapa ungewasikia tu " usioe single mother", Labda kama baba ake mtoto kafariki au kama anaweza mtoto akaishi na bibi yake. Ila wenyewe wakahudumie hadi na damu za wanaume wengine na mawasiliano ni fulluu mwee. Madai yao wao hawapashagi viporo ila single mothers tu
 
Ni zaidi ya kusaidia, kwani si baba yao yupo kwanini ukambebee majukumu yake....
Okay na huko kununua hadi friji ni kumfurahisha mtoto pia? Au friji ya kuhifadhia maziwa ya mtoto Hahaha ncheke mie

Sasa kinachokuchekesha nini hapo dada
 

Kusaidia ni sawa,mfano huwezi ukapeleka nguo za mwanao peke ake wakati kuna watoto wengine, utapeleka nguo, vitu vitu vya watoto, msosi ndio hadi na ada???
Okay na huyo jamaa anaepeleka hadi friji?
 

Teh kwa huduma hizi, siku ya kwenda kumuona mtoto ataachaje kupasha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…