HIVI HATUWEZI KUTUMIA MAJI YA MZINGA KWA MATUMIZI YA MAJUMBANI.

MWANAHARAMU

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2021
Posts
5,350
Reaction score
13,622
Dar es salaam imebarikiwa mito
Tunajua Kuna mto mzinga, uliopo kusini mwa Dar es salaam na kaskazini mwa wilaya ya mkuranga.
Hivi Kuna mkakati wowote wa kuyavuna maji ya moto huu ili upunguze hadha ya shida ya maji jijini Dar es salaam?

Huu mto unatokea milima ya kisarawe kule kazimzumbwi na Mkuranga halafu unatiririsha maji yake zaidi ya kilomita 50, kwenda kumwaga kwenye mlango bahari wa mtoni kijichi na vijibweni.

Mamilioni ya Tani za maji zinapotea kwa siku, huku adha ya huduma ya maji kwa wananchi wake ikiongezeka.

Kila mtu anakili wami haututoshi
Mto kizinga unatumika kidogo, na umesaidia kupunguza hadha kwa wilaya ya Temeke.

Vipi Sasa ukafikiriwa Mzinga au mpaka tusubiri wageni toka nje?

Wakati tunaongelea haya tusisahau pia kupiga marufuku watu kujenga ndani ya bonde hili.

Nawasilisha
 
Inawezekana mbona maji ya mto rufiji yapo yanatumika
 
Mradi huo ungekuwa na gharama nafuu kama ungefanyika miaka mingi sana iliyopita!
Kwasasa mto umesongwa na makazi ya watu kwa asilimia kubwa sana ya mtiririko wake kwenda baharini kiasi cha kufanya ujenzi wa bwawa la kukusanyia hayo maji iwe ni kazi ngumu sana kwa upande wa gharama za kufidia makazi ya raia!
 
Maji ya Mzinga yanavunwa kupitia Mtoni Water Treatment Plant ipo pale Tandika
Ndiyo oldest plant tangu enzi ya mkoloni
Ilijengwa 1950s na kuna bomba lilisambaza maji Dar yote miaka ya 60 mpka Ikulu
Kwa sasa wanatumia sana kiasi watu wa Temeke, Tandika na Mbagala

Tatizo kubwa Dar ni overpopulation ambayo haiendani na maendeleo ya miundombinu
Tatizo lingine ni source za maji
Wakazi wameongezeka ila sources za maji ni zile zile, Mto Ruvu, Mto Kizinga na visima ambavyo havitoshelezi mahitaji na Jiji limekuwa kubwa sana kila angle watu wamejenga
Athari za kimazingira (environmental impacts kama uchafuzi na kukata miti) na shughuli za kibinadamu mf kilimo, ufugaji, matumizi ya viwandani kuongezeka pia zinachangia kwenye kuyavuta na hatimaye usambazaji kisha uhaba wa maji
Kwa mtu anayejenga Dar afikirie zaidi kuvuna maji ya mvua (rain water harvesting) na kuweka storage ya kwake mwenyewe

Maji Dar yatapatikana kipindi cha mvua kuanzia March mpaka August ikizidi kidogo September, baada ya hapo ni kelele na ufafanuzi mwingi kutoka mamlaka kusubiria za Dec kidogo, ikikata kelele za maji zinaanza tena mpaka March
 
🎯
 
Back
Top Bottom