Maji ya Mzinga yanavunwa kupitia Mtoni Water Treatment Plant ipo pale Tandika
Ndiyo oldest plant tangu enzi ya mkoloni
Ilijengwa 1950s na kuna bomba lilisambaza maji Dar yote miaka ya 60 mpka Ikulu
Kwa sasa wanatumia sana kiasi watu wa Temeke, Tandika na Mbagala
Tatizo kubwa Dar ni overpopulation ambayo haiendani na maendeleo ya miundombinu
Tatizo lingine ni source za maji
Wakazi wameongezeka ila sources za maji ni zile zile, Mto Ruvu, Mto Kizinga na visima ambavyo havitoshelezi mahitaji na Jiji limekuwa kubwa sana kila angle watu wamejenga
Athari za kimazingira (environmental impacts kama uchafuzi na kukata miti) na shughuli za kibinadamu mf kilimo, ufugaji, matumizi ya viwandani kuongezeka pia zinachangia kwenye kuyavuta na hatimaye usambazaji kisha uhaba wa maji
Kwa mtu anayejenga Dar afikirie zaidi kuvuna maji ya mvua (rain water harvesting) na kuweka storage ya kwake mwenyewe
Maji Dar yatapatikana kipindi cha mvua kuanzia March mpaka August ikizidi kidogo September, baada ya hapo ni kelele na ufafanuzi mwingi kutoka mamlaka kusubiria za Dec kidogo, ikikata kelele za maji zinaanza tena mpaka March