Kuna plot nilishuhudia hapa Kibada haizidi sqm 650 ikiuzwa 40m aliyekuwa ananunua akanirushia USD 250 kama ganji la kuona
Plot kama hiyo sasa hivi hata 10m hupati mtu kabisa. Ingawa nature ya Property huwa hai Depreciate lakini ukiona hivyo ujue hali sio nzuri kiuchumi
Kuna watu ambao walikuwa vzuri saana kiuchumi mizunguko yao Kibiashara ilikuwa mizuri saana katika hali kama hii kuna strategy huwa wanaitumia inaitwa " Wait and see" yaani wanasubiria kuona nini kitatokea wakati wanafanya hivyo kuna ma cash mengi yapo iddle kwa hiyo wanayapeleka huko kwenye longterm investment with Slow But Sure Returns
Ukienda kama maeneo ya Mbagala au Tandale watu wanaendelea na maisha kama kawaida ingawa sio kama yale ya mwanzo lakini hawajaathirika sana kama watu wa Sinza, Mbezi Beach, Masaki na mitaa mingine kama hiyo
Bei za apartments hazikuwa realistic hivi sasa zinaanza kuwa realistic na baadhi ya watu wanaanza kuona umuhimu wa kuishi karibu na Makazini kuliko hapo mwanzo
Miaka ya 1998-2000 nilikipendelea kupata dinner mitaa ya Jamhuri, Zanaki, Libya, Chaga, Mchafukoge siku hizo ilikuwa ni aghlabu saana kukutana na mtu mweusi maeneo hayo, ulikuwa ukikutana na mweusi atakuwa askari, bawabu au mtumishi aliyechelewa kutoka kibaruani na ukiingia kwenye migahawa ndio kabisa humkuti mweusi
Mambo yamebadilika hivi sasa kuna weusi wengi wanaoishi maeneo hayo na wengi unawakuta mitaa hiyo wakitafuta dinner tunaweza kusema wanapita ile idadi ya wahindi/waarabu