Hivi hawa ambao kila siku wanaporomosha Maghorofa ya Kupangisha DSM hali hii ngumu hawaioni au watapangisha Kuku?

Baadhi tu ya sekta ndo vyuma vmekaza mfano wakulima lakini kwenye sekta ya ujenzi na usafirishaji mizigo havijakaza hata kidogo,wenye pesa bado wanajenga coz wanajua kesho itakuwa poa tu kuliko kuweka pesa bank
Afu startup na wenye biashara vidogo ndo hali tete sio waliokuwa kwenye game pia kukaza kwa vyuma kunatiwa chumvi sana
 
Mwaka jana mwanzoni nilikuwa nina mtazamo huo huo.

Ila nimezunguka sana miezi hii 19 hivi, nikagundua kuwa usimzungumzie mwenzako.

Pili, majengo na ardhi ni investments na assets zinazopanda thamani hata usipozitumia.
 
Suala la vyuma kukaza ni personal sana. Ile dhana ya "ukiona kwako kunaungua,ujue kwa mwenzako kunateketea" sio universally correct.
 
Ni maandalizi tu, JIWE akiondoka kunakua na ''business as usual''!
 
Hivi utajisikiaje ndugu mwandishi, kama atatokea mtu kukupa ushauri kuhusu matumizi ya "pesa" ulioitolea jasho mpaka la meno, bila hata wewe kuomba huo ushauri??? Hajui hata jinsi ulivyosaga rumba mpaka kuipata.[emoji120] [emoji120]

Nahisi unaweza ukampiga mtu kichwa kama cha Zidane (diving head). Au chupuchupu hata ukamkosa na rungu la kisogoni akatoka mbio nyingi sana brake ya kwanza anasimamia tunduma border ya kwenda Zambia.[emoji18]

Waache tu na hela zao, hata wakitaka kuhonga shauri yao.
 
TATIZO TULIZOEA KUISHI MAISHA YASIYO YETU HALISI. SASA NDIYO TUNAISHI MAISHA HALISI. HALI INAKUWA NGUMU KWA SABABU TULIZOEA KUISHI KWA MTELEMKO NA BILA BAJETI. TUNAISHI ISHI TU BILA MIPANGO INAYOELEWEKA.

Wakati wa JK hela nyingi iliyokuwa kwenye mzunguko ilikuwa ni hela ya dili sasa kaja John amebana dili zote ile hela ya dili yote imepotea kwenye mzunguko ndiyo maana watu wanalalamika kwamba vyuma vimekaza kwa maana walishazoea kupata hela kiurahisi bila kuitolea jasho sana.

Hela ipo tatizo tunataka kuendelea kunaishi kwa mazoea na kutaka kulazimisha kuishi maisha ya wakati wa JK. Kama Zimbabwe wameweza ku-survive kipindi chote hicho cha high inflation rate in Africa sisi Tz tutashindwaje kuishi? Tuache kulalamika tuishi kwa mipango na pia tuwe creative kutafuta vyanzo vingine vya mapato.

MIMI BINAFSI HUWA NAAMINI KWAMBA HATA KAMA NITAKUTANA NA HALI NGUMU KULALAMIKA HAKUTANISAIDIA BALI KUTAFUTA UFUMBUMBUZI WA TATIZO NDICHO KITAKACHONISAIDIA KUONDOKANA NA HIYO HALI NGUMU!
 
Mi nahisi wanajipa matumaini kuwa awamu hii ikipita mambo yatakuwa kama kule tulikokuwa...
 
Kuna plot nilishuhudia hapa Kibada haizidi sqm 650 ikiuzwa 40m aliyekuwa ananunua akanirushia USD 250 kama ganji la kuona
Plot kama hiyo sasa hivi hata 10m hupati mtu kabisa. Ingawa nature ya Property huwa hai Depreciate lakini ukiona hivyo ujue hali sio nzuri kiuchumi
Kuna watu ambao walikuwa vzuri saana kiuchumi mizunguko yao Kibiashara ilikuwa mizuri saana katika hali kama hii kuna strategy huwa wanaitumia inaitwa " Wait and see" yaani wanasubiria kuona nini kitatokea wakati wanafanya hivyo kuna ma cash mengi yapo iddle kwa hiyo wanayapeleka huko kwenye longterm investment with Slow But Sure Returns
Ukienda kama maeneo ya Mbagala au Tandale watu wanaendelea na maisha kama kawaida ingawa sio kama yale ya mwanzo lakini hawajaathirika sana kama watu wa Sinza, Mbezi Beach, Masaki na mitaa mingine kama hiyo

Bei za apartments hazikuwa realistic hivi sasa zinaanza kuwa realistic na baadhi ya watu wanaanza kuona umuhimu wa kuishi karibu na Makazini kuliko hapo mwanzo
Miaka ya 1998-2000 nilikipendelea kupata dinner mitaa ya Jamhuri, Zanaki, Libya, Chaga, Mchafukoge siku hizo ilikuwa ni aghlabu saana kukutana na mtu mweusi maeneo hayo, ulikuwa ukikutana na mweusi atakuwa askari, bawabu au mtumishi aliyechelewa kutoka kibaruani na ukiingia kwenye migahawa ndio kabisa humkuti mweusi
Mambo yamebadilika hivi sasa kuna weusi wengi wanaoishi maeneo hayo na wengi unawakuta mitaa hiyo wakitafuta dinner tunaweza kusema wanapita ile idadi ya wahindi/waarabu
 
Kipindi hiki cha vyuma vya jiwe, wakopeshaji wanapiga mpunga mrefu kupitia kutaifisha property za wakopaji wanaoshindwa kulipa madeni. Kuna jamaa aliponea chupuchupu nyumba yake anayokaa kwenda na maji kwa balance ya just 1,5m. Alirudi jioni akakuta ishabandikwa matangazo ya mnada kesho yke asbh!
 
Hawaangalii hapa...wananaangali kuleeee
Kweli kabisa hiyo ndo tofauti ya maskini na tajiri...Maskini ataangalia hali ya sasa na kujitengenezea changamoto na vijisababu elfu moja ya kutofanya kitu lakini tajiri yeye anaangalia future opportunities...Real Estate ni cyclical business( kuna kupanda nakushuka) within two years or soko litapanda tu
 
Km kuna walionauwezo wakujenga bas wapo pia wenyeuwezo wakupangisha! Sema nakufa usiseme tunakufa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…