Hivi hawa jamaa.. Ni Wa Kimataifa "Kweli" au Wa Kimataifa "Uchwara"?

Hivi hawa jamaa.. Ni Wa Kimataifa "Kweli" au Wa Kimataifa "Uchwara"?

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Hawa wakuitwa "Wa Kimataifa" hebu tuchunguze matokeo yake tangu ligi ianze.. lengo ni kuona, "je yaliyomo yamo??''

28/08/2016: Young Africans 3 - 0 African Lyon
07/09/2016: Ndanda 0 - 0 Young Africans
10/09/2016: Young Africans 3 - 0 Majimaji

Na matokeo ya hao aliopambana nao yakoje?
1. African Lyon
20/08/2016: Azam 1 - 1 African Lyon
28/08/2016: Young Africans 3 - 0 African Lyon
03/09/2016: Ruvu Stars 0 - 0 African Lyon

2. Ndanda
20/08/2016: Simba 3 - 1 Ndanda
27/08/2016: Mtibwa Sugar 2 - 1 Ndanda
07/09/2016: Ndanda 0 - 0 Young Africans

3. Maji Maji
20/08/2016: Maji Maji 0 - 1 Tanzania Prisons
27/08/2016: Azam 3 - 0 Maji Maji
03/09/2016: Maji Maji 1 - 2 Mtibwa Sugar
10/09/2016 Young Africans 3 - 0 Maji Maji

Mategemeo ya wengi ni kwakua hawa jamaa wametoka kupambana na miamba ya barani Africa juzi juzi [wako moto].. Ingekua kila wakiingia uwanjani katika hii ligi yetu ya mchangani, timu pinzani zingekua zinaondoka na kapu la magoli.. Lakini imekua kinyume chake.

Mfano:
1. Timu ambayo imegongwa mechi zake zote, eti ina draw nanyi??! Hivi ninyi ni wa kimataifa kweli au wakimataifa uchwara??
2. Timu ambayo imefungwa mechi zake zote za ligi ya mchangani, leo wazee wa kimataifa mnaifunga goli 3 kweli??
3. Timu ambayo imetoka ligi ya mchanganiest miezi michache tu iliyopita mnaifunga goli 3 kwa mbinde?? Alafu mnadiriki kujiita wa kimataifa!??!

Kinachoniuma ni kuendelea kuaibika kwa mwaka mmoja mbele katika uwanda wa soka la Africa.. Maana navyoona mtatuaibisha zaidi Msimu ujao.. Ndo hivyo hatuna jinsi..

Mola tuepushe na hii aibu nayoiona... Sijui itakua ni kwa jinsi gani maana hawa jamaa hawabebeki, ila wewe wajua Baba.




 
Kinachonifanya niwaze ni, kama hawa jamaa wanadraw na Ndanda.. Je wakikutana na Etoile Du Sahel au Ally Ahly Msimu ujao itakuwaje???

Watanzania wenzangu tuongeze dua.. Ili hii aibu ipungue, maana vipigo vipo pale pale.
 
1473540296591.jpg




Hapo vipi ndo mana soka letu ni la uchwara toka kwa wachambuzi uchwara
 
Kinachonifanya niwaze ni, kama hawa jamaa wanadraw na Ndanda.. Je wakikutana na Etoile Du Sahel au Ally Ahly Msimu ujao itakuwaje???

Watanzania wenzangu tuongeze dua.. Ili hii aibu ipungue, maana vipigo vipo pale pale.
1473540407084.jpg
 
Kwahiyo Mkuu mnajilinganisha na wa kimataifa wenzenu?


Mpira ni dakika 90 kuna kushinda,suluhu na kufungwa na kila mechi ina game plan yake ujeruman bingwa wa dunia katolewa na france
 
Sijui ni simba sijui ni yanga kila walipokuwa wanakwenda sokoine kuna timu hapo lazima iache point hata kama imetimia kias gan
 
Mpira ni dakika 90 kuna kushinda,suluhu na kufungwa na kila mechi ina game plan yake ujeruman bingwa wa dunia katolewa na france

Kwahiyo tuwape muda,.. sawa.
 
tumia akili wewe uliyepost hapa

we unashangaa yanga kutoka dro na ndada, mbona inaweza kutoka droo na matofali yasiyocheza mpira, we fikiria kama ukijengwa ukuta golini hata hao barcelona wanaweza kufunga goli.
 
Nakumbuka kipindi kile Wamatopeni walipotuwakilisha hatua ya makundi barabi Afrika. Hapa Bongo walikuwa wanashinda si chini ya tano kila mechi. Teh teh teh
 
Back
Top Bottom