Hivi hawa mbwa aina ya Pitbull ni mbwa halisi?

Hivi zile zimefana na 🐺 Wolf nazo zinatabia gani mana naona kama ndo vichaa zaidi.
 
Hivi dude linamkalisha mnyama mtata kama nyati afu eti lije likalishwe na mbwa.. huyu mbwa watu wanampa sifa sio zake.

Yani awekwe simba mmoja na huyo mbwa halafu simba akalishwe sio kweli hiyo battle mbwa lazima alambishwe mchanga
Hata Mimi sikubali mkuu.
 
Yani kwa hizo crossbreeding zote, rottweiler na hao pitbull ndio vichaa. Hawafai kabisa kufugwa, kwanza wanamtindo wa kupoteza kumbukumbu.

Kuna clip niliona hao pitbull wamemshambulia mbwa wa aina nyingine na kumla
OK, kwa hilo yawezekana cross breeding yake ilichanganywa na simba! Kwa 30%.
 
Hao mbwa hawataki kukaa njaa, wanataka kila muda uliowekwa (waliouzoea) kwa ajili ya kula basi chakula kiende na kwa wastani utakao wafanya waridhike.

Sasa wabongo wengi budget hizo hatuna, yai tunataka kufuga mbwa kwa kumlisha kile tulichobakiza sisi, hapo ni lazima wakubadilikie tu maana wanakuwa na hasira.


Pitbull kama wanakula vizuri na una wahandle vizuri huwa hawana matukio ya hovyohovyo.

NB: Hao mbwa wakiamua kufanya tukio basi linakuwa ni tukio haswaa, wana nguvu hatari.
 
Hivi dude linamkalisha mnyama mtata kama nyati afu eti lije likalishwe na mbwa.. huyu mbwa watu wanampa sifa sio zake.

Yani awekwe simba mmoja na huyo mbwa halafu simba akalishwe sio kweli hiyo battle mbwa lazima alambishwe mchanga
Simba mmoja hawezi kuua nyati mkubwa mwenye utimamu wa mwili, labda awe anaumwa au ni mzee.

Simba mmoja hawezi kumchukua nyati mkubwa, unless waende kama pride (kundi la Simba wasiopungua watano).
 
Hakuna mbwa anayeweza kupambana na Simba achilia mbali nyati umewahi kumuona Simba kweli?
Lakini pia Simba mmoja hafanyi chochote kwa nyati aliyetimamu kimwili, labda kama ulimaanisha nyati mtoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…