Hivi hawa ndugu wanaosema mtu utume CV halafu wanakaa kimya, wanakuwa na maana gani?

Hivi hawa ndugu wanaosema mtu utume CV halafu wanakaa kimya, wanakuwa na maana gani?

AlphaMale

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2019
Posts
613
Reaction score
1,425
Kama Mtu hana uwezo wa kukufanyia connection ya kupata kazi si bora avunge tu kuliko yeye mwenyewe akwambie utume CV, halafu baada ya hapo anauchuna, sasa ndiyo nini?

Mambo ya kupeana false hopes si uungwana.
 
pole mkuu bt ujue ni wengi wanapitia situation kama yako, kila kitu hupangwa na muumba siku ikifika hutozungushwa hata sekunde
 
Hiyo ni tiba ya Kisaikolojia Mkuu, ndio maaana wamama wakati wa njaa ama dhiki huamua kuinjika sufuria na mawe ndani kwenye moto huku watoto wakisubiri masaa na masaa msosi uive mwishowe woote huishia kusinzia na kulala.

Hivyo unapoombwa CV wewe peleka naamini ipo siku itatokea kweli kweli ikatiki. Lkn unapopeleka CV pia inakupa hop na deni kwa yule uliyempelekea hivyo pambana usikate tamaa.
 
Wanatumia CV yako kwenye mambo yao ila wewe hunufaiki kwa lolote
 
Wakati unasubir wakujibu ingia shambani ulime nchi yetu imebarikiwa mapori manene yako kibwerebwerere
 
Nimeomba field mara mbili wakanambia nitume CV. Ikabidi niandike tu na hata wote hawajajibu. Huyo mmoja nikatumia njia nyingine nikajua nafasi washajichukulia wao ila nimejua ideology imenitenga nao. Nilipojaribu tena nikaambiwa na HR kuwa nafasi zitakuwepo tena mwezi wa 10 tarehe ambayo ni siku 5 tu kabla ya field yangu kuisha. Kwanza chuo gani kinafunga mwezi wa kumi.

Huyu mwingine kanambia nafasi ikipatikana atanambia. Wakati barua nishamwambia confirmation naomba mwisho iwe lini. Hivi wabongo hatuwezi sema direct kwamba hiki Hapana, hiki Ndiyo. Siamini kama ughaibuni wanasumbua hivi. Nafasi hakuna sema hakuna, vigezo mtu hana mwambie, hamna interest naye mwambie. Sasa haya mambo ya "suala lako tutalishughulikia" ni uchawi tu kama uchawi mwingine.
 
Back
Top Bottom