Hivi hawa wasichana wa kazi wana nini?

Hivi hawa wasichana wa kazi wana nini?

haujambo shangazi yangu
habari za huko kwetu?
kwa kweli umepotea sana

unaona watu wanavyo wasimanga hawa madogo
wakati watoto wao wako mashule ya kimataifa
eti kwa nini walizaliwa kwenye familia masikini na kwenda kuomba kazi za ndani?????


nakugongea "like" mara tano,
moja ingekuwa ni demu au mshikaji kamwomba hiyo buku 5 asingekuja kuripot hapa
mbili inaelekea hakufurahishwa na kuondoka kwa huyo bint hata kama alimruhusu alimruhusu kwa shingo upande hivyo anavyoona huko alikoenda binti anapata shida jamaa ni kama anafurahia moyoni kuwa kapatikana
ushauri wangu kwako
kuwa na ubinadamu,kama mliishi vizuri na unahisi anapata shida msaidie na hata kama unaweza kumrudisha,mrudishe maadamu alikuwa mchapa kazi pia atakuwa amejifunza kitu .
jione kama mzaz, hakuna anayependa kuwa hg,hata mwanao hutapenda awe hg,but yote ni maisha,na ubinadamu ni kusaidiana na kuchukuliana. mtoa uzi utakuwa umenielewa,ndio maana wengine tunawaendeleza ili siku moja nao wawe na maisha yao.
 
Yaani sometimes inabidi tu tuwahurumie nahisi uelewa wao hauko sawa..kuna msichana nilimpeleka kwa mama yangu..akakaa nao karibu miaka 3 akiwa huru(jumapili the entire day anaruhusiwa kwenda kushinda kanisani-as according to yeye aliokoka) sasa nadhani sometimea uhuru unapowazia kuna tatizo..akaanza mara kununa ohvyo wakati mwingine bila sababu,tho ni mchapa kazi kwakweli..au akienda churc anazidi kuchelewa mmh...ghafla siku hiyo kaamka akamwambia mama ..kesho naomba niende..mama akamwambia ok but anipigie mimi kwanza..nikamuuliza vipi kuna tatizo akasema hapana bali tu amepata kazi kwengine-Buguruni(hope wanamlipa juu zaidi) nikamwambia fine..u may go hata leo,nikatoa baraka zote.sasa cha ajabu tangu aondoke huu ni mwezi wa pili...simu,msg kila mara..za ooh nimewamiss..sometimes najibu,zikinichosha nazichunia..jana ndo kaanza anaomba hata elfu 5..amechacha mno,maisha ni magumu..jamani sasa nimweleweje huyu?kwanini aliondoka kama hakuwa na uhakika na anakoenda?huwa kinawapata nini hawa wasichana?
kwimukaga che mwali?
 
Hata kama ukiwafanya zaidi ya wanao bado hawabadiliki kuwa HG/HB yaani tena ukiwadhamini sana wanaona una shida na huwezi kuwaacha wanaanza mashida.

kweli kabisa, me walivyo mfanyiaga mama angu sina hamunao kabisa

alikuwa na hg alimthamini kama mtoto wake japokuwa alikuwa ana mlipa mshahara wake kawaida ila bado alikuwa anamtimizia wajibu wake kama mzazi wa kumnunulia vitu kama nguo, viatu nk, hakuna mtu aliyekuwa anajua kama yeye ni hg, siku moja wazazi walisafiri kwenda mkoa mwingine akabaki hg na mdogo wangu ambaye yupo form4, wakati dogo yupo shule, sijui yule dada baadae aliingiwa na pepo gani, alikusanya baadhi ya nguo za dogo na pesa akasepa zake kwenda Dar kufika huko yule aliyempeleka huko akamtelekeza akawa hana mahali pa kukaa mwishoe akakamatwa na polisi usiku akiwa anazurula.

Katika kuhojiwa akasema kuwa nyumbani wamemfukuza then alikuwa apewi chakula na mateso kadha wa kadha.

Ndipo hapo Polisi wakamuomba na za mother nakuanza kupewa hizo tuhuma.

Kwakweli me sijui hawa watu wanataka waleleweje wakiwa kwenye kazi zao.... Kama mtu alikuwa anathaminiwa kiasi hicho lakini unaambulia kupakazwa ubaya usiokuwa na sababu ya msingi
Sometime huwa nawafananisha na moto ukicheza nao vibaya wanakuunguza hao, so kamwe usijaribu kumuamini hg 4 100%.
 
nakugongea "like" mara tano,
moja ingekuwa ni demu au mshikaji kamwomba hiyo buku 5 asingekuja kuripot hapa
mbili inaelekea hakufurahishwa na kuondoka kwa huyo bint hata kama alimruhusu alimruhusu kwa shingo upande hivyo anavyoona huko alikoenda binti anapata shida jamaa ni kama anafurahia moyoni kuwa kapatikana
ushauri wangu kwako
kuwa na ubinadamu,kama mliishi vizuri na unahisi anapata shida msaidie na hata kama unaweza kumrudisha,mrudishe maadamu alikuwa mchapa kazi pia atakuwa amejifunza kitu .
jione kama mzaz, hakuna anayependa kuwa hg,hata mwanao hutapenda awe hg,but yote ni maisha,na ubinadamu ni kusaidiana na kuchukuliana. mtoa uzi utakuwa umenielewa,ndio maana wengine tunawaendeleza ili siku moja nao wawe na maisha yao.

Umenena Mkuu!
 
haujambo shangazi yangu
habari za huko kwetu?
kwa kweli umepotea sana

unaona watu wanavyo wasimanga hawa madogo
wakati watoto wao wako mashule ya kimataifa
eti kwa nini walizaliwa kwenye familia masikini na kwenda kuomba kazi za ndani
?????

Kama kweli kuna mtu anawaza hivo basi..Dah!...ama kweli mtu anaweza kwenda madarasa mengi tu lakini bado asielimike!
 
Ngoja JOYCE KIRIA aje atoe expirience yake hapa ,au ni mwana mmu yupi mdada aliyewahi kuwa housegirl atueleze kunani?
 
kweli kabisa, me walivyo mfanyiaga mama angu sina hamunao kabisa

alikuwa na hg alimthamini kama mtoto wake japokuwa alikuwa ana mlipa mshahara wake kawaida ila bado alikuwa anamtimizia wajibu wake kama mzazi wa kumnunulia vitu kama nguo, viatu nk, hakuna mtu aliyekuwa anajua kama yeye ni hg, siku moja wazazi walisafiri kwenda mkoa mwingine akabaki hg na mdogo wangu ambaye yupo form4, wakati dogo yupo shule, sijui yule dada baadae aliingiwa na pepo gani, alikusanya baadhi ya nguo za dogo na pesa akasepa zake kwenda Dar kufika huko yule aliyempeleka huko akamtelekeza akawa hana mahali pa kukaa mwishoe akakamatwa na polisi usiku akiwa anazurula.

Katika kuhojiwa akasema kuwa nyumbani wamemfukuza then alikuwa apewi chakula na mateso kadha wa kadha.

Ndipo hapo Polisi wakamuomba na za mother nakuanza kupewa hizo tuhuma.

Kwakweli me sijui hawa watu wanataka waleleweje wakiwa kwenye kazi zao.... Kama mtu alikuwa anathaminiwa kiasi hicho lakini unaambulia kupakazwa ubaya usiokuwa na sababu ya msingi
Sometime huwa nawafananisha na moto ukicheza nao vibaya wanakuunguza hao, so kamwe usijaribu kumuamini hg 4 100%.

Ukweli mtupu my sist.
 
Hayo mambo ya kuharibiana wasichana wa kazi ni ya kawaida sana kwenye nyumba za kupanga/za msalagambo. Hata mimi yaliwahi kuikuta nyumba yangu wakati huo naishi kwenye nyumba za kupanga. Sio wote wanaoona unakaa vyema na kwa amani na masichana wako wa kazi wakati yeye kila siku anabadilisha. Lazima ukitoka asubuhi wamlishe maneno maneno.

Mimi wa kwangu baada ya kuishi naye miaka 3 aliniomba aende nyumbani kwao Songea akasalimie wazazi. Tulimruhusu kwa moyo mmoja pamoja na kumfungashia zawadi na pesa za kujikimu mpaka atakaporudi. Kinyume chake tulipata ttarifa toka kwa watu wanaomfahamu kuwa ameonekana maeneo ya Kimara akiishi na dada mmoja. Baada ya mke wangu kufuatilia kwa karibu akabaini kuwa alidanganywa na kijana mmoja wa mtaaani kuwa angemuoa lakini baada ya kumchezea alimuacha kwenye mataa. Hivyo akaamua kujiunga na kundi la wasichana wakaa geto waliokuwa wakijiuza usiku kwenye mabaa.

Tofauti yake huyu hakurudi wala kusumbua kuomba msaada lakini kulingana na taarifa tulizozipata mitaani alikuwa anaishi maisha magumu mno.
 
mim hapa mama mkwe wangu na wifi walimrubuni binti hadi wakamchukua, mateso kuzidi huko kaomba kurudi kwangu nikakata.
 
ndugu hao watu ni wasumbufu kweli, nadhani ni upeo unachangia, ingekua vema kama kungekua na college ya wafanyakazi wa majumbani ili wajue majukumu yao na haki zao pia
Je umefikiria itabidi uwalipe sh ngapi hao watakao kuwa wametoka chuo????
 
Kuna jamaa yangu mmoja ana mahusiano na hg kwa muda wa miaka 7 na mpaka leo wako pamoja sana, huyo jamaa alimpata huyo hg kwa dadake kabisa, na uhusiano ulianzia huko! Kwa muda wote wameishi kama wachumba na wana mpango wa kufunga ndoa...

Hii imenifundisha kwamba si wote wana matatizo, kuna wengine wana upeo zaidi kuliko wale waliofika mbali kielimu na hata kuwazidi upeo walio wakubwa kwake...

Kwa sasa anasoma chuo kimoja kizuri sana na performance yake iko safi kabisa hadi raha. Omba tu Mungu akupe hg mzuri na utaishi naye vizuri tu akikupa, usiende hivi hivi bila msaada wa Mungu wakati wa kuwatafuta hawa hg!
 
Je umefikiria itabidi uwalipe sh ngapi hao watakao kuwa wametoka chuo????

Hahahaha, nadhani Masuo hajui kwamba HG waliosoma wapo, hata akitaka mwenye Masters ya Housekeeping au Food Production anapata!
 
Last edited by a moderator:
Sioni ajabu ya yeye kukuomba kitu kidogo, kwa kuwa ameokoka
a)anamaanisha kuwa ana shida kweli,
b)salamu anazotuma ni kuonyesha bado anao upendo kwenu.
 
Back
Top Bottom