GE2025 Hivi haya maandamano ya tarehe 29 ni ya CHADEMA au mbona sielewi?

GE2025 Hivi haya maandamano ya tarehe 29 ni ya CHADEMA au mbona sielewi?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Arsenal Gunner

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2022
Posts
10,891
Reaction score
17,718
Unajua kuna jambo silielewi. Haya maandamano ya tarehe 29 ni ya CHADEMA au wananchi wote tujue kabisa maana kila sehemu hawa wahamasishaji wanatamtaja mwenyekiti wa CHADEMA Lissu

Ina maana tunaenda kufa kwa ajili ya Lissu au nchi sielewi ujue wazee

Naomba tueleweshane kwa watu kama sisi tusio na vyama Ili tusiingie kwenye mambo yasiyotuhusu tulale nyumbani siku hiyo
 
Sema kwenye hili wanafeli sana, wangetakiwa kutokuhusisha haya maandamano na Chama chochote ili Mtanzania aliye hata CCM aweze kuunga juhudi, siunasikia hata CCM huko nako nao wanataka reforms lakini sasa hapa wakija na sijui Chadema mara sijui nini kuna baadhi ya wananchi wataona miyeyusho
 
licha ya wa ccm sisi ambao hatuna vyama wanatufanya turudi nyuma maana lisu amekua ajenda Kila sehemu mpaka huyo mange kimambi anaehamasisha Kila mda kutaja lissu kama vile watanzania wote tunamkubali lissu
 
Ingia tu barabarani kiongozi ajenda zitapatikana mbele ya safari.Uongozi mbaya,rushwa kuonekana jambo la kawaida,utekaji wa raia,matumizi mabaya ya madaraka,katiba isiyoendana na wakati tuliopo sasa.Ajenda nyingine tutaongeza tukiwa barabarani.Mungu akubariki ukifanya hivyo hiyo tarehe
 
Lazima uhoji sio unaingia barabarani bila kujua vitu unavyopigania maana ni kuchezea uhai je kitendo Cha lissu na chadema kuwekwa kwenye ajenda ni tunaenda kufa Kwa ajili ya chadema au nchi
 
Kama mpaka sasa haujui lengo la maandamano ni nini na yanakuhusu vipi, kaa nyumbani.
Lissu alishasema hataki huruma ya mtu. Wanaomtetea labda hawakumsikia vizuri.
Wananchi wanadai ushirikishwaji katika maamuzi pamoja na uduma bora..
 
Lazima uhoji sio unaingia barabarani bila kujua vitu unavyopigania maana ni kuchezea uhai je kitendo Cha lissu kuwekwa kwenye ajenda ni tunaenda kufa Kwa ajili ya chadema au nchi
Ajenda ya Lissu nimetaja kwenye matumizi mabaya ya madaraka.Leo Lissu kesho mwanafamilia wako(utajisikia vipi watu wanaingia barabarani kutetea mwanafamilia wako anayefanyiwa ukatili na wenye mamlaka.Ingia tu barabarani kiongozi tunakufa mara moja tu na hatutaishi milele.Ubarikiwe ukifanya hivyo)
 
Kama mpaka sasa haujui lengo la maandamano ni nini na yanakuhusu vipi, kaa nyumbani.
Lissu alishasema hataki huruma ya mtu. Wanaomtetea labda hawakumsikia vizuri.
Wananchi wanadai ushirikishwaji katika maamuzi pamoja na uduma bora..
Jibu swali kwanini anatajwa lissu na chadema kwenye ajenda za maandamano kwanini zisitaje shida zinazotuhusu watanzania tu
 
Unajua Kuna jambo silielewi haya maandamano ya tarehe 29 ni ya chadema au wananchi wote tujue kabisa maana Kila sehemu Hawa wahamasishaji wanatamtaja mwenyekiti wa chadema lissu inamaana tunaenda kufa Kwa ajili ya lissu au nchi sielewi ujue wazee naomba tueleweshane Kwa watu kama sisi tusio na vyama Ili tusiingie kwenye mambo yasiyotuhusu tulale nyumbani siku hiyo
Bila shaka wewe ni miongoni mwa Wapinga maandamano.Husitahili kujibiwa chochote
 
M
Ajenda ya Lissu nimetaja kwenye matumizi mabaya ya madaraka.Leo Lissu kesho mwanafamilia wako(utajisikia vipi watu wanaingia barabarani kutetea mwanafamilia wako anayefanyiwa ukatili na wenye mamlaka.Ingia tu barabarani kiongozi tunakufa mara moja tu na hatutaishi milele.Ubarikiwe ukifanya hivyo)
msitufanye hatuna akili Kuna vipeperushi vimeandikwa lissu aachiwe wakati huyo ni mwenyekiti wa chadema Sasa hiyo ya lisu inahusiana vipi na sisi wananchi
 
M

msitufanye hatuna akili Kuna vipeperushi vimeandikwa lissu aachiwe Sasa hiyo ya lisu inahusiana vipi na sisi wananchi
Hiyo tarehe unaweza kwenda kituoni ulipojiandikisha ukapige kura au kama hujatimiza vigezo vya kupiga kura unaweza kuendelea na majukumu yako ya kila siku.Wanahitajika watu mia tu kuleta ukombozi na idadi hiyo tayari imetimia kuwa na amani kiongozi
 
Ukombozi wa chadema huo sio wa tanzania full stop yaani ajenda lissu aachiwe halafu Mimi nikafe kisa mjinga mmoja sifanyi kazi hiyo
 
Back
Top Bottom