#COVID19 Hivi hii dunia tutahangaika na huu upuuzi wa Corona hadi lini? Dawa ni kutunga sheria tu

#COVID19 Hivi hii dunia tutahangaika na huu upuuzi wa Corona hadi lini? Dawa ni kutunga sheria tu

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Ninachofahamu kwa uhakika wa 100% ni kwamba janga hutiliwa mkazo endapo tu kuna manufaa yanapatikana kwa kupitia Janga hilo, iwe ni magonjwa, matetemeko, mafuriko nk.

- Mfano kwa magonjwa, ukiona NGO inapigia sana kelele masuala ya Ukimwi kwa mfano, basi tambua kuna manufaa wanapata toka serikalini au kwingine kokote pale. Hali kadhalika kwa magonjwa mengine mengi tu.

- Huu ugonjwa wa Corona upo kweli na unaua, hilo halina ubishi, ila shida ni kwamba kuna magonjwa mengine hapa Tanzania yanayoua zaidi kuliko Corona, lakini husikii hizi kelele na msukumo mkubwa namna hii kutaka watu wachomwe chanjo. Ukiona Steve Nyerere anahamasisha chanjo jua kuna manufaa anapata, halikadhalika kwa wengine wote, wanamslahi na chanjo hizo, iwe kwa kuuza, kufanya udalali nk. Magonjwa kama Malaria yanaua zaidi lakini Steve Nyerere hajawahi kufanya kampeni ya kuhamasisha watu wavae neti usiku kabla ya kutoka nje, ni maslahi tu.

- Kwahiyo hapa dawa ni moja tu. Itungwe sheria kali ya kuzuia mtu kutamka au kuandika neno Corona popote pale na kwa namna yeyote. Hata tukihisi umewaza tu kitu kinachoitwa Corona, iwe ni kosa kisheria, na adhabu yake ikiwezekana iwe kunyongwa kabisa, nawapa siku 1 tu, Corona inaisha hapa Tanzania.

Ni hayo tu, na hayo ndio mawazo yangu, na ikatokea nimepata nafasi ya kufanya maamuzi katika hii dunia, nitatokomeza matatizo mengi sana kwa njia hiyo, maana matatizo huanzia kichwani, physical manifestation huja baada ya akili kukubali!

 
Ninamnukuu baba wa Taifa Mwl J.K. Nyerere

"Hatuwezi kupata suluhu ya matatizo yetu kwa kujidanganya kuwa hayapo"

Mwasho wa kunukuu.
Ni kweli, ila pia matatizo huwa amplified disproportionately kiasi hata kuzidi matatizo makubwa zaidi kwa kuyapa nafasi kubwa ya kututia hofu, na huo ndio msingi wa hoja yangu
 
Ninafikiri kwa wenye akili timamu waliona namna Magufuli alivyoishughulikia vizuri, kwa hekima na uzalendo tofauti na mama yetu ambaye ameamua kutuuza kwa wenye masilahi.
 
Ninafikiri kwa wenye akili timamu waliona namna Magufuli alivyoishughulikia vizuri, kwa hekima na uzalendo tofauti na mama yetu ambaye ameamua kutuuza kwa wenye masilahi.
Shida ni maslahi tu, hakuna mtu anaekupenda sana eti hataki uumwe corona, ni maslahi atakayopata ndio kikubwa kwao. Hata Steve Nyerere, utasikia kalamba bingo ndio maana anahamasisha chanjo, ila sio kwamba anakupenda sana
 
Shida ni maslahi tu, hakuna mtu anaekupenda sana eti hataki uumwe corona, ni maslahi atakayopata ndio kikubwa kwao. Hata Steve Nyerere, utasikia kalamba bingo ndio maana anahamasisha chanjo, ila sio kwamba anakupenda sana
Mkuu, mabeberu kama walivyo wanadamu wengine wanaangalia masilahi. Hata wanasiasa wetu wapo pale kwa masilahi yao binafsi. Hizi habari za utumishi kwa wananchi ni sera tu.
 
Ninachofahamu kwa uhakika wa 100% ni kwamba janga hutiliwa mkazo endapo tu kuna manufaa yanapatikana kwa kupitia Janga hilo, iwe ni magonjwa, matetemeko, mafuriko nk...
Mawazo ya akina Magufuli haya!
 
Dawa ya Corona ipo,Kuna mchanganyiko wa dawa Kama nne hivi ikiwemo aZuma , inasemekana unatibu Corona ,tena hatakama mgonjwa ni mahututi kabsa,

Nahis wameamua iwe black market ili wapge hela nyingi .....maana dozi ya sindank 16 ni Kama 2000000, pia sababu hawataki kubanwa na sheria in case mtu kafa, nahs hyo chemistry imegunduliwa tz, si unajua bongo ni watu wa magendo, bongo nyoso
 
🤣 mkuu unaupeo mdogo sana!
Wewe ndiye huna upeo. Unakariri na kusubiri watu wakaumbie cha kufanya na na kwa hyo no wonder mnalishwa censored iformation ili muwe
kama wanavyotaka manipulators.

Awamu ya Magufuli (anayechukia anywe sumu afe), tulishinda corona kwa kishindo kwa sababu tulikuwa na kiongozi mwenye kuona mbali. Alihimiza kila mtu aombe kwa Mungu ambaye yupo tu, na hata walozi wanajua yupo. Alihimiza njia za matumizi ya mimea kwa namna anuai kitu ambacho ni murua kwa kuwa asilimia 90 ya madawa ni mimea iliyosindikwa na kutakatifishwa, na ndiyo sababu watu wetu waligundua na kutengeneza dawa za aina ambali mbali ambazo zilituvusha kwa kishindo. Mheshimiwa Magufuli alihllimiza kwa vitendo utekelezaji wa kanuni zilizoshauriwa na wataalam wa afya ambazo ni muhimu katika kujikinga dhidi ya maambukizi ya magonjwa yanayoenea kwa mfumo wa hewa

kama kunawa mikono, - kila sehemu kulikuwa na vifaa vyenye maji tiririka na sabuni - na jambo hili lilisimimamiwa nchi nzima.

Kuepuka misongamano, kwenye vyombo vya usafiri utakuwa kweli ni levo siti.

LEO HII HOLA. Eti chukueni tahadhari!. Regulatory authorities zipo lakini watu wanashonana kwenye usafiri hadi pa kukanyaga hakuna. Watu wanafurahia matunda ya kifo...

Magufuli aliidharau corona n akila mtu alikuwa na ujasiri wa kuidharau na watu waliishi salama.
Sasa hivi tuna mambo ya aibu. Viongozi ni waoga wanawaita watu hofu. Hofu inaua kuliko hata ugonjwa. Ugonjwa unaabudiwa na kujioni ni mfalme. Ukiwatia watu hofu watakufa hata kwa kitu ambacho hakikkuwa kinaua. Scientists na pschologists wanalijua hili.
Bahati mbaya mtaji wa ujinga wa watu, uliotunzwa miaka mingi ya ccm unatumika katika kila kampeni ya kuwadanganya watu.

Nani asiyejua kwamba hofu inaua? Watu wametiwa hofu, watu wote hawaongelei njia za kutibu imebaki chanjo kwa kuwa chanjo inapepelewa na mshiko wakutisha. watuwanafanya biashara kwa ujinga wa watu. Madhara ya chanjo, hayatakiwi kusikika, Mbinu mbadala hazitakiwi kusikika, wanasahau kwamba hiyo chanjo wala si tiba. Juhudi za kutibu kwa kutumia dawa zlizotuvusha hazisungmziwi tena. Ukizungmzia unakula ban. Watu wanakufa lakini hakuna anayeona hili. Wamekazania chanjo tu ili wajiandae kustaff
Who knows the Mindset of God?

Nani anajua madhara ya muda mrefu wahizo chanjo, zinazolazimishwa kwa nguvu kubwa hivy;?
Nani mwenye ufahamu wakujiuliza kwa nini waliochnjwa ndio wenye hofu kuliko wasiochanjwa?
HOfu yao ya kuambukizwa inatoka wapi wakati wamehakikisha kwamba hawawezi kufa kwa corona hata wakiambukizwa?
Kwamba sasa wamechanjwa wao Corona kwao haina madhara na wataishi milele, kwa nini waendelee kuwa na hofu na corona tena kama si wehu?
Wanazuia media watu wasione yanayowapata kwenye kampeni zao? Hata kujiuliza kwa nini hawaongelei chanjo za TB, Malaria, Sukari, BP, n.k, ambayo yanaua kuliko corona?
Hawana mpango wa kuwaza namna ya kuwalinda watu wanaoambukizwa huku wjaijua chnjo yao siyo tiba!.

NINAONA TIME MANGUNGA INAJIRUDIA PALE, WALIPOUZA RAIA WAO KWENDA UTUMWANI KWA BEI YA SHANGA NA MASHUKA MEUPE

HISTORIA INAJIRUDIA
 
Hoja yako ni ipi hapa?
"Kwahiyo hapa dawa ni moja tu. Itungwe sheria kali ya kuzuia mtu kutamka au kuandika neno Corona popote pale na kwa namna yeyote. Hata tukihisi umewaza tu kitu kinachoitwa Corona, iwe ni kosa kisheria, na adhabu yake ikiwezekana iwe kunyongwa kabisa, nawapa siku 1 tu, Corona inaisha hapa Tanzania."

Tafakari vizuri hapa then umekubali ugonjwa upo na unaua halafu itungwe sheria usizungumziwe au hata kuwazwa so hata hao watakaokuwa wanaumwa wataandikiwaje ripoti ya kuwa wanaumwa Corona..?? Unafikiri kulificha tatizo ndo kulitatua!
 
Wewe ndiye huna upeo. Unakariri na kusubiri watu wakaumbie cha kufanya na na kwa hyo no wonder mnalishwa censored iformation ili muwe
kama wanavyotaka manipulators...
Umeandika maelezo mengi hayana hata maana hapa! Nilichokuwa nakigusia nishamjibu mtoa mada angalia huko.
 
Kwahiyo hapa dawa ni moja tu. Itungwe sheria kali ya kuzuia mtu kutamka au kuandika neno Corona popote pale na kwa namna yeyote. Hata tukihisi umewaza tu kitu kinachoitwa Corona, iwe ni kosa kisheria, na adhabu yake ikiwezekana iwe kunyongwa kabisa, nawapa siku 1 tu, Corona inaisha hapa Tanzania.
Sheria zingine hamuwezi kuzisimamia ,mtaweza hili la korona ??? Nyie vijana wa lumumba hamjawahi kitu cha Mana kwa Taifa hili
 
Back
Top Bottom