#COVID19 Hivi hii dunia tutahangaika na huu upuuzi wa Corona hadi lini? Dawa ni kutunga sheria tu

#COVID19 Hivi hii dunia tutahangaika na huu upuuzi wa Corona hadi lini? Dawa ni kutunga sheria tu

Steve Nyerere hajawahi kufanya kampeni ya kuhamasisha watu wavae neti usiku kabla ya kutoka nje, ni maslahi tu.

Hebu fafanua kidogo hapa pa kuvaa net usiku kabla ya kutoka nje...
 
Ninamnukuu baba wa Taifa Mwl J.K. Nyerere

"Hatuwezi kupata suluhu ya matatizo yetu kwa kujidanganya kuwa hayapo"

Mwasho wa kunukuu.
Wale wanaodhani bunduki na mahakama ni suluhisho la kila tatizo. Bado nchi yetu inashida sana mahali fulani pa uelewa
 
Dah....huo upeo wako mrefu uko wapi mkuu?🤣🤣🤣🤭
Mkuu hivi mnajua kusoma kweli..?
Mbona nilishamjibu kitambo Sana!
Hivi kwa hoja yake ya kukubali ugonjwa upo halafu mtu akiwaza tu anyongwe unaona hilo lipo sawa!..🤣 so mtu anaenda hospital anapimwa anagundulika anahuo ugonjwa so daktari aandike anaumwa gono na sio korona maana akiandika korona ananyongwa!.. what a fucking idea!😂
 
Ninachofahamu kwa uhakika wa 100% ni kwamba janga hutiliwa mkazo endapo tu kuna manufaa yanapatikana kwa kupitia Janga hilo, iwe ni magonjwa, matetemeko, mafuriko nk.

- Mfano kwa magonjwa, ukiona NGO inapigia sana kelele masuala ya Ukimwi kwa mfano, basi tambua kuna manufaa wanapata toka serikalini au kwingine kokote pale. Hali kadhalika kwa magonjwa mengine mengi tu.

- Huu ugonjwa wa Corona upo kweli na unaua, hilo halina ubishi, ila shida ni kwamba kuna magonjwa mengine hapa Tanzania yanayoua zaidi kuliko Corona, lakini husikii hizi kelele na msukumo mkubwa namna hii kutaka watu wachomwe chanjo. Ukiona Steve Nyerere anahamasisha chanjo jua kuna manufaa anapata, halikadhalika kwa wengine wote, wanamslahi na chanjo hizo, iwe kwa kuuza, kufanya udalali nk. Magonjwa kama Malaria yanaua zaidi lakini Steve Nyerere hajawahi kufanya kampeni ya kuhamasisha watu wavae neti usiku kabla ya kutoka nje, ni maslahi tu.

- Kwahiyo hapa dawa ni moja tu. Itungwe sheria kali ya kuzuia mtu kutamka au kuandika neno Corona popote pale na kwa namna yeyote. Hata tukihisi umewaza tu kitu kinachoitwa Corona, iwe ni kosa kisheria, na adhabu yake ikiwezekana iwe kunyongwa kabisa, nawapa siku 1 tu, Corona inaisha hapa Tanzania.

Ni hayo tu, na hayo ndio mawazo yangu, na ikatokea nimepata nafasi ya kufanya maamuzi katika hii dunia, nitatokomeza matatizo mengi sana kwa njia hiyo, maana matatizo huanzia kichwani, physical manifestation huja baada ya akili kukubali!

Duh!
Kwa hiyo tufuate sera ya mbuni kuzika kichwa kwny mchanga ili kutatua matatizo?!
 
Shida ni maslahi tu, hakuna mtu anaekupenda sana eti hataki uumwe corona, ni maslahi atakayopata ndio kikubwa kwao. Hata Steve Nyerere, utasikia kalamba bingo ndio maana anahamasisha chanjo, ila sio kwamba anakupenda sana
Una dini mdogo wangu?
Kama una dini basi nenda ukatubu.
Nimeona huamini kama binadamu anaweza kumpenda binadamu mwenzake.
Kingine umetaja adhabu za kuua watu kwasababu wamekukosea.

Una roho ya mauti. Au wewe siyo binadamu.

Duniani pana mengi.
 
Una dini mdogo wangu?
Kama una dini basi nenda ukatubu.
Nimeona huamini kama binadamu anaweza kumpenda binadamu mwenzake.
Kingine umetaja adhabu za kuua watu kwasababu wamekukosea.

Una roho ya mauti. Au wewe siyo binadamu.

Duniani pana mengi.
Jikite kwenye hoja, sio kutafuta huruma sentimentally
 
Mkuu hivi mnajua kusoma kweli..?
Mbona nilishamjibu kitambo Sana!
Hivi kwa hoja yake ya kukubali ugonjwa upo halafu mtu akiwaza tu anyongwe unaona hilo lipo sawa!..🤣 so mtu anaenda hospital anapimwa anagundulika anahuo ugonjwa so daktari aandike anaumwa gono na sio korona maana akiandika korona ananyongwa!.. what a fucking idea!😂
Unampiga mgonjwa placebo, kisha unampa dawa stahiki. Maana kujua tu una Corona, tayari unaweza ukafa, kwa kujua tu
 
Back
Top Bottom