Hivi hii harufu ya baadhi ya mitaa ya jijini Dar naisikia peke yangu tu?

Hivi hii harufu ya baadhi ya mitaa ya jijini Dar naisikia peke yangu tu?

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Wakuu kwema!

Aisee! Baada ya kutoka kuzurura huko Duniani, sitaki kupataja nisijeonekana najikosha hapa, na wenye nongwa zao na vijiba vya roho wasije nitolea mvuke wa ushubwada. Ila ifahamike tuu nimetoka huko Dunia ilipo.

Kwa kweli Dar inanuka vibaya mno. Inanuka vitu mfano wa mavi, sijasema ni mavi jamani Ila ni kama hivyo.

Yaani Asilimia kubwa ya Maeneo yananuka chemba za maji taka. Nashindwa Kueleza hapa. Sitaki kugombana na wenye Dar yao, sitaki kabisa. Maana najua wapo wanayoipenda, ikumbukwe siiongelei Jambo hili Kwa ni mbaya lakini naongea ili Jambo Fulani lifanyike.

Halafu ukiwaona wakazi wa Dar ni Kana kwamba hawaisikii hiyo harufu, pengine wamekuwa sehemu ya harufu yenyewe, sijasema watu wa DAR mnanuka chemba za maji taka 😃😃😃. Maana wenye hasira hamkosekani.

Hata hivyo akili yangu ikanambia sio rahisi watu WA DAR kuisikia hiyo harufu mbaya ya mavi Kwa maana maisha yao ni ya taabu sana. Taabu zimeua mishipa ya Nostril ndani ya pua. Hawezi kunususa tena.

Hasa watu masikini wapanda Daladala, hawa ndio wanaoonja joto ya jiwe, hata hivyo wenyewe ni Kama joto Hilo hawalisikii kwani taabu imewafubaza na kuwafanya waone kila kitu Kama kipo Sawa.

Kipindi nasoma pale UDSM wala sikuwa najua Dar inanuka, nimekaa zaidi ya miaka mitano kama sio sita sikuwa naona hizo harufu. Labda Maeneo ya Tandale huko na viunga vya makazi ya WALIA NA MUNGU watu fukara apeche Alolo.

Najiuliza niliwezaje kuishi miaka mitano kipindi kile?

Nafikiri serikali ipitie tena miundombinu ya taka hasa mitaro ya maji taka ili mji usiwe jiji la harufu mbaya.

Wananchi wa Dar nanyi mjitahidi kuwa wasafi hata kama mmezoea harufu yenu mbaya kumbukeni wageni kama Sisi tunaotoka Duniani tunakujaga pia kuwasalimu.

Muwe na Haya hata kidogo.

Taikon nitakuwa DAR Kwa wiki tatu mfululizo kabla sijaenda kudhuru Zanzibar nikielekea kuchumbia Visiwa vya Comoro.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
 
Wahuni huku wanatembea na kiberiti kimejazwa nyaa(Kama ambavyo ulikua Zamani ukienda hosp. kupima choo unaenda umekiweka kwny kiberiti), kila akisikika handasi anakifunua ananusa full kudindisha,hii harufu ya nyaa itakuja kuwakera lini huko road?


Mkuu embu fafanua hiyo Teknolojia ya Nyaa ikoje
 
Kwa kweli Dar inanuka vibaya mno. Inanuka vitu mfano wa mavi, sijasema ni mavi jamani Ila ni Kama hivyo.
Ni kweli Dar ilikuwa hainuki hivi miaka michache iliyopita, nadhani baada ya ujenzi wa miundombinu, kuna vitu havijakaa sawa. Barabara ya kutoka Makumbusho hadi Mwenge hiyo harufu inasikika dhahiri, nahisi ni ule mtaro uliojengwa pembeni ya barabara hiyo
 
Ni kweli Dar ilikuwa hainuki hivi miaka michache iliyopita, nadhani baada ya ujenzi wa miundombinu, kuna vitu havijakaa sawa. Barabara ya kutoka Makumbusho hadi Mwenge hiyo harufu inasikika dhahiri, nahisi ni ule mtaro uliojengwa pembeni ya barabara hiyo

Tena pale Makumbusho Stend ndio sitaki kupasikia.
Pananuka utadhani nini. Nusura Nitapike lakini ajabu ni kuwa Mimi pekee ndiye niliyeonekana kukerwa na harufu Ile watu wengine hata hawana habari
 
Back
Top Bottom