Hivi hii harufu ya baadhi ya mitaa ya jijini Dar naisikia peke yangu tu?

Hivi hii harufu ya baadhi ya mitaa ya jijini Dar naisikia peke yangu tu?

Wakuu Kwema!

Aisee! Baada ya kutoka kuzurura huko Duniani, sitaki kupataja nisijeonekana najikosha hapa, na wenye nongwa zao na vijiba vya roho wasije nitolea mvuke wa ushubwada. Ila ifahamike tuu nimetoka huko Dunia ilipo.

Kwa kweli Dar inanuka vibaya mno. Inanuka vitu mfano wa mavi, sijasema ni mavi jamani Ila ni Kama hivyo.

Yaani Asilimia kubwa ya Maeneo yananuka chemba za maji taka. Nashindwa Kueleza hapa. Sitaki kugombana na wenye DAR Yao, sitaki kabisa. Maana najua wapo wanayoipenda, ikumbukwe siiongelei Jambo hili Kwa ni mbaya lakini naongea ili Jambo Fulani lifanyike.

Alafu ukiwaona wakazi wa Dar ni Kana kwamba hawaisikii hiyo harufu, pengine wamekuwa sehemu ya harufu yenyewe, sijasema watu wa DAR mnanuka chemba za maji taka [emoji2][emoji2][emoji2]. Maana wenye hasira hamkosekani.

Hata hivyo akili yangu ikanambia sio rahisi watu WA DAR kuisikia hiyo harufu mbaya ya mavi Kwa maana maisha yao ni yataabu Sana. Taabu zimeua mishipa ya Nostril ndani ya pua. Hawezi kunususa tena.

Hasa watu masikini wapanda Daladala, hawa ndio wanaoonja joto ya jiwe,hata hivyo wenyewe ni Kama joto Hilo hawalisikii kwani taabu imewafubaza na kuwafanya waone kila kitu Kama kipo Sawa.

Kipindi nasoma pale Udsm wala sikuwa najua DAR inanuka, nimekaa zaidi ya miaka mitano Kama sio sita sikuwa naona hizo harufu. Labda Maeneo ya Tandale huko na viunga vya makazi ya WALIA NA MUNGU watu fukara apeche Alolo.

Najiuliza niliwezaje kuishi miaka mitano kipindi kile?

Nafikiri serikali ipitie tena miundombinu ya taka hasa mitaro ya maji taka ili mji usiwe jiji la harufu mbaya.

Wananchi wa Dar nanyi mjitahidi kuwa wasafi hata Kama mmezoea harufu yenu mbaya kumbukeni wageni Kama Sisi tunaotoka Duniani tunakujaga pia kuwasalimu.

Muwe na Haya hata kidogo.

Taikon nitakuwa DAR Kwa wiki tatu mfululizo kabla sijaenda kudhuru Zanzibar nikielekea kuchumbia Visiwa vya Comoro.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Hamia mkoani mkuu utuachie dar yetu
 
Ungekuja dar wakati wa jk ikiwa na majalala kila pahala hata pale fire njia panda ya muhimbili ilikuwepo jalala, hapo ungesema je?

Pua zako ziko over smell hata mkeo awe msafi sana unless yatamkuta ya yule alisemekana anapika hovyo hovyo.
 
Mleta mada wewe ni Kiduko Lilo au mkewe?
Naona uandishi wenu unafanana kwa 98%!!
 
Ungekuja dar wakati wa jk ikiwa na majalala kila pahala hata pale fire njia panda ya muhimbili ilikuwepo jalala, hapo ungesema je?

Pua zako ziko over smell hata mkeo awe msafi sana unless yatamkuta ya yule alisemekana anapika hovyo hovyo.


🤣🤣🤣

Mimi napenda Usafi kuliko Kula.

Mke wangu naenda kuchumbia Comoro, Karibu kwenye msafara.

Tukitoka Comoro tutapandisha mpaka Madagascar tutakaa siku tano, kisha mwezi wa kumi tutakuwa Kwa Madiba, hapo utarudi DAR yenu inayonuka Mimi nikielekea Dunia ilipo
 
Sisi watu wa Dar tunapenda harufu ya Mavi Mavi hivi, Sasa we Heriel na wenzio mna option mbili maana Dar ni Jiji la wewe Kuchagua,either urudi huko masulumbwikunyisho au ubaki Dar..nakuhakikishia ukibaki Dar na ww utaipenda tu...Dar Hatupangiwagi...Hasa na nyie wa Mkoa...Kamuulize Mzee wa Kolomije 😅😅😅
 
Back
Top Bottom