Hivi hii harufu ya baadhi ya mitaa ya jijini Dar naisikia peke yangu tu?

Maeneo ya sinza ndio balaa mkuu unaeza kudhani Uko chooni halafu mbaya zaidi wamamantilie wanauza chakula hapo hapo, wauza kahawa dah ni balaa hii dasalama yetu ..
 
Ni kweli...
Ile barabara ya Sinza kijiweni kuelekea kwa mtogole inanuka mavi..nadhani wanapitisha maji ya chooni kwenye mtaro wa maji. Ndo Sinza kwa wajanja hiyo
Dah kama Uko kwenye kichwa changu ..pale sinza kijiwe asikuambie mtu ..halafu masela na mamantilie hawana noma wala nini ..njo sasa huku karibu na ubungo mawasiliano Uko ndio balaa kwenye ile mitaro wanapitisha sijui nini ...kuna hewa nzito plus joto plus matatizo wooii..
 
Ukiingia guest ndio balaa ..choo kipo huko huko room hakina mlango unaeza dhani umelala chooni ...dar ni tabu tupu ila ndo kuna mzunguko wa ngawira sasa...
 
Pembeni kuna chips tamu kinoma na chachandu ya ukwaju
Hahahaha ukichanganya na matunda ..bora ivyo vya kupikwa ..hayo matunda yanavyokatwa katwa halafu chini ya mitaro umo mizigo inapita tu kama kawaida unakula zako na harufu yako maisha yanaendelea.
 
Mkuu mimi nimekuelewa, na sina tatizo na hiyo observation yako, kwa sababu ni kweli once unapotoka nje ya Africa na kama umekaa kwa muda mrefu kidogo, ukishuka na kutoka tu hapo JNIA mfumo wako wa upumuaji unapata taarifa.

Hao wa hapo DSM washazoea kwa sababu hiyo harufu wako karibu nayo kwa muda mrefu kwa hiyo wamesha - merge nayo na hawahisi harufu yoyote tofauti tena.

Sisi tunaoishi huku Mikoani tuna harufu zetu pia kwa level za huku[emoji23], lakini uzuri wa huku hakuna misongamano
 


Mikoani nimepita huko hakika hewa yake imetulia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…