Hivi hii harufu ya baadhi ya mitaa ya jijini Dar naisikia peke yangu tu?

Hivi hii harufu ya baadhi ya mitaa ya jijini Dar naisikia peke yangu tu?

Wakuu Kwema!

Aisee! Baada ya kutoka kuzurura huko Duniani, sitaki kupataja nisijeonekana najikosha hapa, na wenye nongwa zao na vijiba vya roho wasije nitolea mvuke wa ushubwada. Ila ifahamike tuu nimetoka huko Dunia ilipo.

Kwa kweli Dar inanuka vibaya mno. Inanuka vitu mfano wa mavi, sijasema ni mavi jamani Ila ni Kama hivyo.

Yaani Asilimia kubwa ya Maeneo yananuka chemba za maji taka. Nashindwa Kueleza hapa. Sitaki kugombana na wenye DAR Yao, sitaki kabisa. Maana najua wapo wanayoipenda, ikumbukwe siiongelei Jambo hili Kwa ni mbaya lakini naongea ili Jambo Fulani lifanyike.

Alafu ukiwaona wakazi wa Dar ni Kana kwamba hawaisikii hiyo harufu, pengine wamekuwa sehemu ya harufu yenyewe, sijasema watu wa DAR mnanuka chemba za maji taka 😃😃😃. Maana wenye hasira hamkosekani.

Hata hivyo akili yangu ikanambia sio rahisi watu WA DAR kuisikia hiyo harufu mbaya ya mavi Kwa maana maisha yao ni yataabu Sana. Taabu zimeua mishipa ya Nostril ndani ya pua. Hawezi kunususa tena.

Hasa watu masikini wapanda Daladala, hawa ndio wanaoonja joto ya jiwe,hata hivyo wenyewe ni Kama joto Hilo hawalisikii kwani taabu imewafubaza na kuwafanya waone kila kitu Kama kipo Sawa.

Kipindi nasoma pale Udsm wala sikuwa najua DAR inanuka, nimekaa zaidi ya miaka mitano Kama sio sita sikuwa naona hizo harufu. Labda Maeneo ya Tandale huko na viunga vya makazi ya WALIA NA MUNGU watu fukara apeche Alolo.

Najiuliza niliwezaje kuishi miaka mitano kipindi kile?

Nafikiri serikali ipitie tena miundombinu ya taka hasa mitaro ya maji taka ili mji usiwe jiji la harufu mbaya.

Wananchi wa Dar nanyi mjitahidi kuwa wasafi hata Kama mmezoea harufu yenu mbaya kumbukeni wageni Kama Sisi tunaotoka Duniani tunakujaga pia kuwasalimu.

Muwe na Haya hata kidogo.

Taikon nitakuwa DAR Kwa wiki tatu mfululizo kabla sijaenda kudhuru Zanzibar nikielekea kuchumbia Visiwa vya Comoro.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Nakushaur usifike maeneo haya utafia njian
Posta feri
Vingungut hasa hasa machinjion
Mbagala
Mazizin moshi bar uko ndan ndan huko
Tandika
Kijiwe samli
Bugurun

Tafadhari beba ns mitung ya oxygen
 
Nakushaur usifike maeneo haya utafia njian
Posta feri
Vingungut hasa hasa machinjion
Mbagala
Mazizin moshi bar uko ndan ndan huko
Tandika
Kijiwe samli
Bugurun

Tafadhari beba ns mitung ya oxygen

🤣🤣🤣🤣

Hili ni tishio sasa
 
Tena pale Makumbusho Stend ndio sitaki kupasikia.
Pananuka utadhani nini. Nusura Nitapike lakini ajabu ni kuwa Mimi pekee ndiye niliyeonekana kukerwa na harufu Ile watu wengine hata hawana habari
Uko sawa
 
Kwa wenye akili Utajiri unapatikana popote, hauko limited.

Nikefikia Mikocheni
Hata mikocheni pananuka tu, lakini sisi wenyewe tushatengeneza kinga kwa ajili ya hiyo harufu ndio maana hatuisikii kabisa, na wewe pia kwa kuwa kinga yako ilikuwa imeshuka baada ya kuishi huko duniani kwa muda sasa umerudi endelea kujichanganya tu kinga zako zitarudi kama zamani hutoisikia tena harufu mbaya kama ulivyokuwa zamani kabla hujaenda huko Duniani, karibu sana Dar
 
Hata mikocheni pananuka tu, lakini sisi wenyewe tushatengeneza kinga kwa ajili ya hiyo harufu ndio maana hatuisikii kabisa, na wewe pia kwa kuwa kinga yako ilikuwa imeshuka baada ya kuishi huko duniani kwa muda sasa umerudi endelea kujichanganya tu kinga zako zitarudi kama zamani hutoisikia tena harufu mbaya kama ulivyokuwa zamani kabla hujaenda huko Duniani, karibu sana Dar


Mimi nawaachia limji lenu
 
Yaani hapo hawawezi kukuelewa hata kidogo, watoto wengi wazawa wa Dar hawana adabu wala heshima kwa wakubwa zao, hili lipo wazi.

Wana kauli chafu na hawana maneno ya busara, haijalishi ni nani yupo karibu yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
DAR ES SALAAM NI CHAFU

DAR ES SALAAM INANUKA

Maeneo ya DAR ES SALAAM YALIOZA SIKU NYINGI

Umeandika Ukweli mtupu, wakazi wa Dar es salaam wengi hawasikii hiyo harufu ya mavimavi kwasababu wameizoea sana

Kuna harufu ya chemba za vinyesi na majalala
 
Asalamaleko Mzizima.
Asalamaleko DarSlum jiji la wavuja jasho.

-Kaveli-
 
DarSlum yote kwa ujumla, ventilation ni mbovu sana kutokana na mbanano wa watu na makazi, with very poor sewage systems around the city.

-Kaveli-
 
Back
Top Bottom