Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
- Thread starter
-
- #141
Nenda Dodoma ndio utashangaa,yaani mitaro ya maji machafu inatoa balaa halafu kama vile kila kitu kipo sawa,hakuna Mamlaka inayojishughulisha kuondoa hali hiyo,hayo ni baadhi ya maeneo machache tu huenda asilimia kubwa ya mikoa mingine nayo ipo hivyo hivyo pia,nchi yetu kwa kweli bado sana
Utakua mgeni wa huu mji,wenyeji hawaisikii hii harufu hataWakuu Kwema!
Aisee! Baada ya kutoka kuzurura huko Duniani, sitaki kupataja nisijeonekana najikosha hapa, na wenye nongwa zao na vijiba vya roho wasije nitolea mvuke wa ushubwada. Ila ifahamike tuu nimetoka huko Dunia ilipo.
Kwa kweli Dar inanuka vibaya mno. Inanuka vitu mfano wa mavi, sijasema ni mavi jamani Ila ni Kama hivyo.
Yaani Asilimia kubwa ya Maeneo yananuka chemba za maji taka. Nashindwa Kueleza hapa. Sitaki kugombana na wenye DAR Yao, sitaki kabisa. Maana najua wapo wanayoipenda, ikumbukwe siiongelei Jambo hili Kwa ni mbaya lakini naongea ili Jambo Fulani lifanyike.
Alafu ukiwaona wakazi wa Dar ni Kana kwamba hawaisikii hiyo harufu, pengine wamekuwa sehemu ya harufu yenyewe, sijasema watu wa DAR mnanuka chemba za maji taka [emoji2][emoji2][emoji2]. Maana wenye hasira hamkosekani.
Hata hivyo akili yangu ikanambia sio rahisi watu WA DAR kuisikia hiyo harufu mbaya ya mavi Kwa maana maisha yao ni yataabu Sana. Taabu zimeua mishipa ya Nostril ndani ya pua. Hawezi kunususa tena.
Hasa watu masikini wapanda Daladala, hawa ndio wanaoonja joto ya jiwe,hata hivyo wenyewe ni Kama joto Hilo hawalisikii kwani taabu imewafubaza na kuwafanya waone kila kitu Kama kipo Sawa.
Kipindi nasoma pale Udsm wala sikuwa najua DAR inanuka, nimekaa zaidi ya miaka mitano Kama sio sita sikuwa naona hizo harufu. Labda Maeneo ya Tandale huko na viunga vya makazi ya WALIA NA MUNGU watu fukara apeche Alolo.
Najiuliza niliwezaje kuishi miaka mitano kipindi kile?
Nafikiri serikali ipitie tena miundombinu ya taka hasa mitaro ya maji taka ili mji usiwe jiji la harufu mbaya.
Wananchi wa Dar nanyi mjitahidi kuwa wasafi hata Kama mmezoea harufu yenu mbaya kumbukeni wageni Kama Sisi tunaotoka Duniani tunakujaga pia kuwasalimu.
Muwe na Haya hata kidogo.
Taikon nitakuwa DAR Kwa wiki tatu mfululizo kabla sijaenda kudhuru Zanzibar nikielekea kuchumbia Visiwa vya Comoro.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Bila kusahau honi za magari kila sehemu.
Kiduku lilo alioongea sana humu kwamba watu wa Dar wamebanana sijui wanapumuaje watu walimcheka.
Ukikaa nje kwa mda siku unafika Dar utashangaa makelele,wenzetu ukienda sokoni pako na utulivu ,ukiingia zile malls na supermarket kubwa kubwa unakuta mziki tulivu watu wanafanya shopping. Siku ukiingia dar upo kama club inayopigwa miziki zaidi ya 100 tofauti ,hapa mwuza sumu ya mende spika inapiga kelele ,mbele mwuza CD anapiga mziki wake kwa nguvu ,hapa mwuza nyama anapasua mifupa ,kule mwuza sim card anatangaza ,pembeni gari ya promotion ya tigo inapiga mziki ,makonda wanapiga debe ,piki piki na bajazi zinapiga honi na mziki, mno visu naye anachanganya baiskeli. Mwinjilisti naye kashika bible na mic pembeni ya barabara anahubiri . Ili mradi vurugu mtindo mmoja.
Munye nyie afu tuzoe sisi? Tuliwatuma kuishi huko Dar?Tusaidieni Ndugu zenu
Munye nyie afu tuzoe sisi? Tuliwatuma kuishi huko Dar?
Umesema kweli kabisa yani ukiingia Dar cha kwanza ni harufu za hovyo za uchafu mitaro michagu imekua kero watu wanachuruzisha maji machafu yanayotuama kwa muda mrefuYaaa ni kweli..hata ukiwa unatoka mkoani ukiwa unaingia tu dar unaanza kusikia harufu za ajabu ajabu...ni harufu mbaya
htrππKumezidi
sawa sawaSiwezi kukaa uswahilini Mkuu.
Hapa nazungumzia DSM Kwa ujumla
Utakua mgeni wa huu mji,wenyeji hawaisikii hii harufu hata
Ila kuna maeneo dar yanatia kinyaa....hasa maeneo ya kkoo, sometime utakuta chemba zinatoa mavi kama chemchem yanatiririka kwenda pasipo julikana na watu wapo wamepanga bidhaa zao wanauza bila aibu....sema dar kuna pisi za kila sampuli
Ni kweli daslm ukiwa unaingia tuu kutoka mkoani lipo joto na harufu fulani sio ya kawaida ila wenyeji wameizoea hata uonges vip watakushangaa maeneo mengi harufu sio nzuri kabisa mimi mwanzo nilijua kwa sababu ya msongamano wa watu wengi katika eneo dogo na umwagaji wa maji taka toka viwandani..