Hivi hii inakuwaje kwa sisi vibarua wa ujenzi

Msumb

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2022
Posts
3,452
Reaction score
5,372
Mambo vipi wakuu Natumaini mko poa kabisa, niende kwenye mada Moja kwa Moja, ni hivi toka jumatatu nilikuwa kama kibarua kwenye kumwanga zege baadhi ya maeneo,.

Kiasi tulichokubaliana ni kwa siku ni sh 13000 na kazi ilikuwa inatakiwa iishe Leo jumatano jioni, lakini cha ajabu tumelipwa jumatatu hiyo 13000 ila Jana na Leo ni chenga tu mara tuzungushwe tu majibu hayaeleweki ebu mnisaidie wadau nifanyeje na Ile hela imeisha toka jumatatu usiku,

Naomba msaada wenu tafadhali 🙏 🙏

Usiku huu Sina kitu
 
Duh ila kuna watu wana roho ngumu. Kazi ya zege unamlipa mtu 13,000 kwa siku?
 
Mzee mbona unalipwa 2x ya bei elekezi, mie najuaga ni buku 7 kwa siku unless uwe operator wa mashine ya zege ndo dau ni nono ila kwa wabeba mawe, cement, mchanga, sijui saidia fundi ni 6000 hadi 7000 shilingi za kitanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…