Hivi hii kitu mmeshwai kupata experience nacho

Unamlaumu chinga ambaye hahusiki na malezi ya mwanao. Hivi wazazi wa kisasa mwanao anapata wapi ujasiri wa kulilia kitu toka kwa strangers? Wa kwangu hata mgeni tu akifika nyumbani kwangu anaheshimika na hawezi kusumbuliwa kwa namna yoyote ile.

Mtoto lazima afundishwe mipaka ya kumiliki, ajue kutofautisha zawadi na mahitaji ya lazima. Mpe mahitaji ya lazima kwa wakati lakini zawadi mpe pale anapofanya jambo zuri ili kumuhamasisha kuwa mzuri kwenye jambo husika (sio mara zote. Mfano mtoto umemtuma akaenda, akirudi unampa pesa ya pipi/chocolate. Unamuharibu kwasababu ataamini hiyo ni haki yake na kila ukimtuma lazima umlipe) au wakati unaoona unafaa kumnunulia zawadi. Mfundishe kwamba hata akiona kitu kizuri asikitake kwa lazima, ni either akuombe au asubirie umnunulie mwenyewe. Na iwapo ataomba na ukamwambia asubirie, sharti atii.

Wa kulaumiwa ni wewe kwa kumdekeza mtoto, na sio chinga ambaye ametumia udhaifu wa mwanao kukuuzia bidhaa. Umetenda kosa kumlipa fedha pungufu bila makubaliano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…