Ntakua tofauti na wengi ambao wao ni kukejeli kila jitihada za viongozi chini ya ccm.
Kweli samia aliingia pale machi 2021 kuchukua kijiti, na katika hotuba zake nyingi alisema alikabiliwa na miradi mingu sana mikubwa ya maendeleo aliachiwa na hayati, na akasisitizi ataiendeleza kwa manufaa ya wananchi na maendeleo ya nchi.
Ila nikirecall, nakumbuka chanjo ya uviko ile covax aliipambania kupunguza maambukizi na janga lile.
Kuvutia uwekezaji mpya, juzi nilikua naskia Kuna miradi zaidi ya 900 mipya kwa mwaka 2024 tu na haijawahi fikiwa. Almost dolla bilioni 120.
Also royal tour imeshoot sana tourism bongo.
Kuna ile barabara ya kaengesa mpaka chitete sumbawanga huko, aliweka jiwe la msingi.
Hospitali na vitu vya afya zaidi ya 1300 ni kati ya miradi yake.
Kuna ule mradi wa boost almost shule za msingi 400 zimesukwa. Mradi wa boost ulikua almost trilioni 1 vyumba vya madarasa 4000.
Mimi nafahamu hayo, na haya niliyashika last year, mzee wangu akiwa amelazwa pale gairo hospitali ya wilaya alokua akiizindua mwezi wa saba ule. Ile hospitali nzuri saaaaaana.
Baba yangu alikuja akafariki bochi lakini pale alikua attended vizuri sana tukatoka nae safi. So ana miradi mingi yake mwenyewe kama yeye. Kuachana ile ya magufuli ambayo mingi hata kama ameimalizia mingi imebaki kama ghost tu.