Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Kila unapotembea hivi sasa katika nchi hii utayaona mabango kwa maelfu, ya wagombea wa CCM yakiwa yamebandikwa sehemu mbalimbali za kuwanadi wagombea wao kwa uchaguzi mkuu ujao.
Vile vile katika kila mkutano wao wa kampeni, utaona mashabiki wao, wakiwemo watoto wadogo wanaosoma shule za msingi, wakiwa wamevakishwa sare za chama chao, yaani T/shirt na kofia, ambazo huwa wanapewa bure.
Sasa swali ninalojiuliza hivi sasa, hivi chama ambacho kiongozi wao mkuu, John Magufuli, huwa anajitanabaisha kuwa yeye ni mtetezi wa wanyonge, inakuwaje kifuje pesa kiasi hiki, kwa "kuprint" mabango ya wagombea wao kwa maelfu na maelfu, huku watoto wa shule za msingi, wakiwa wanakaa chini sakafuni, kwa ajili ya kukosa madawati?
Hivi unawezaje "kuprint" maelfu kwa maelfu ya T/shirt na kuwagawia bure mashabiki wenu, wakati hospitali nyingi nchini zikiwa hazina dawa muhimu za panadol?
Vile vile chama cha CCM kinaewezaje kusambaza bendera nchi nzima, na kuzitundika kwenye barabara zote kuu, wakati wanafunzi wa shule za msingi, wakiwa hawana hata uniform za kuvaa mashuleni kwao?
Imenenwa kuwa kupanga ni kuchagua, hivyo wanaccm wako tayari kufuja pesa hizo kwa mabilioni.na mabilioni, kwa ajili tu ya "kuprint" mabango ya wagombea wao, ambayo yamewagharimu mabilioni ya shilingi, wakati wafanyakazi wa Umma, hawajawaongezea mishahara yao, ambayo ni kwa mujibu wa sheria, kwa miaka 5 mfululizo, katika serikali hii ya awamu ya tano!
Kazi tunaachiwa watanzania katika uchaguzi mkuu huu ujao, aidha kuchagua chama ambacho kitaendelea kutupa mateso zaidi, kwa miaka mingine, au kuchagua chama ambacho kimetangaza neema, kwa wananchi wote wa nchi hii, kutokana na sera yake ya Uhuru, Haki na maendeleo ya watu.