Hivi hiki ndicho Kiingereza cha Profesa Ndalichako?

Kama unashindwa kuona kosa lake liko wapi, sitoshangaa kuona na wewe ni propesa wa jalalani kama yeye tu
Acha porojo sema hapo alitakiwa ongea hivi kaongea hivi hapo ilitakiwa hivi ikawa hivi siyo unaakuja na maneno pinga kwa vigezo hapa ni JF siyo face book
 
Hakuna maneno wala utetezi wowote kwenye hili. Waziri huyu uwezo wake ni Mdogo sana hata ufanisi wa wizara yake haupo. Elimu ya makaratasi ndio hasa tunajua hatuwezi endelea. Pengine kuna degree za Mrisho Gambo hapo.
 

Tafakari sana tena sana utaelewa kitu..
 

Tafakari sana utaelewa kitu...
 
Kwa hiyo wote wanaoongea kiungereza kizuri tuwape uprofesa? Kiingereza ni lugha tu. Tembea uone.
 
One hundred and fifty million TZS.Kilikuja na meli. Pale Udsm mwalimu anaongea Kinge akiwa darasani tu. Mkitoka nje ni kiswahili mpaka nyumbani. Mtu Kinge anaongea asilimia 3 ,Kiswahili asilimia 97.
Kwan lugha yetu ya taifa ni IPI? Watanzania acheni uzwazwa
 
Labda kaongea makusudi namna hiyo ili asije onekana anajua zaidi ya boss wake.
Huoni mjadala kuhusu yeye umeshika kasi na watu wamesahau kuwa boss yeye akizungumza lazima panadol ziwe jirani? Watu wana mbinu za kulinda vyeo bwana! Unambebea mizigo muzee kuupa uhakika mkono kwenda kinywani.
Nilibahatika kuona clip ya muzee anazungumza na beberu mleta msaada akiwa kiranja wa njia zetu no hatari! Ilibidi Mimi ndio ninywe panadol na kutundikiwa drip!
 
You can not detect the problem when you are a problem yourself
 
"utakaa selo" you are going to stay in the cell, meaning "you will stay in custody". Hayo ni matatizo ya tafsiri ya moja kwa moja yaani direct translation. Mfano mbaya ni kama "you can't me" ukimaanisha "huniwezi"
 
Pia kingereza sio "mabomberstic" cha kuzungumza ni cha kawaida.
 
Hapa Waziri wa Elimu, Profesa Ndalichako akitoa maagizo ya kukamatwa Mhandisi Mchina.

View attachment 1315270

Sent using Jamii Forums mobile app
Watanzania acheni ulimbukeni, uzwazwa na ushamba. Lugha yako ya Taifa ni IPI? Haya hebu nambie wewe unaejua kingereza na huyu Professor asiyejua kingereza umemzidi nini cha msimanga hapa? Mwenzio kwenye rekod za vitabu vya dunia na dunia inamtambua, sasa wewe unaejifnya RAIA wa United Kingdom endelea kula kingereza chako.
 
Hujui inakuadhiri vipi? Halafu yupo sector nyeti ya elimu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwan lugha yetu ya taifa ni IPI? Watanzania acheni uzwazwa
Tatizo sio lugha kushindwa kuijua, Bali ulisomaje?
Imagine kijana aende China kisha akaanze sekondari kwa kichina hadi anapata PhD kwa kichina. Mwisho anatunukiwa Uprofesa kwa kufundisha kwa kichina.
Anakuja nyumbani anakutana na mchina yupo hapa na hakimudu kichina kuwasiliana naye vyema, jee hamuwezi kupata mshangao?
Hapa nyumbani sasa hivi watoto wetu wako shule za English medium ngazi ya chini kabisa na wanatiririka kiingereza hawa wenye PhD wanakwamia wapi? Mtu akisema vyeti vyao vya magumashi atakosea?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…